Riwaya - Balaa

Riwaya - Balaa

Sheeeda ni kwamba ndio yapikwa now ipo sehemu ya 94 so nasubir isogee kdg...mkitaka niweke moja moja
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU: 0757633010

SEHEMU YA TISINI NA TATU

Mbili pale aliposimama, ingawa alimpa kisogo Daniel Mwaseba lakini alikuwa anahisi kila kitu kilichokuwa kinatokea nyuma yake. Kumbuka vijana hawa walikuwa ni nusu makomandoo, makatili na wanaoweza kucheza na hisia. Ingawa Daniel Mwaseba hakutoa ukelele wowote ule wa kuweza kumstua mtu hadi anafika pale, lakini Mbili wa Six Killers alikuwa anasikia makelele makubwa sana, ndio alikuwa anapigiwa makelele hisiani. Na ile ngumi ya nguvu toka kwa Daniel Mwaseba kwenda katika uti wake wa mgongo alikuwa ameshaihisi tangu inakunjwa hadi wakati inarushwa. Kazi ya Mbili ilikuwa ndogo sana, kuruka mbele kwa haraka kwa mtindo wa sambasoti na alipotua chini walikuwa wanaangaliana na Daniel Mwaseba uso kwa uso!

Balaa!

Daniel Mwaseba alistaajabu sana umahiri mkubwa uliooneshwa na yule jamaa. Lakini alishangaa kwa sekunde i mbili ilipotimia sekunde ya tatu naye akajipanga vyema, akajua anapambana na mtu asiye wa kawaida.

Daniel Mwaseba alijirusha juu huku mguu wake wa kulia ukitangulia mbele kuelekea katika kifua cha yule jamaa. Mbili sasa alikuwa amejipanga vizuri, alirudi nyuma kidogo na kubonyea kwa chini, Daniel alipitiliza jumla na kudondoka vibaya sana baada ya teke lake kukosa wa kumpiga. Daniel alinyanyuka kwa kusuasua huku yule jamaa akiwa anamcheka kwa kebehi na dharau. Daniel Mwaseba alijipanga tena, safari hii akiwa makini zaidi alishachoka dharau za yule jamaa. Lakini kwa bahati mbaya kabisa hakufanikiwa kufanya alichotaka kukifanya!

Ghafla! Taa zenye mwanga mkali ziliwashwa na uwanja mzima ulikuwa na nuru mithili ya mchana!

Balaa!

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
Mwandishi; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA TISINI NA NNE

Baada ule mwanga mkali wa taa. Ulioleta nuru mahali pote pale, vikafata vicheko vya karaha toka mahali ambako Daniel Mwaseba hakuwa anapajua, yeye alisikia sauti tu. Lakini Mbili wa Six Killers alipatambua vizuri sana mahali ambako vikipotokea vicheko hivyo.
Wakati Daniel Mwaseba akishangaashangaa kutafuta mahali sahihi vikipotoka vicheko hivyo mara mlango mkubwa wa nyumba iliyokuwa mbele yake ulifunguliwa.
Walitoka watu watatu walioshiba. Miili imara iliyojengeka vizuri kimazoezi. Vifua wazi huku wakiwa wamevaa pensi za kijeshi zilizo katika mtindo wa timberland, na T-shirt nyeusi za mpira zilizowabana vyema. Jamaa walimsogelea Daniel Mwaseba kwa mwendo wa taratibu huku Daniel nae akijihadhari kwa kusogea nyuma, kinyumenyume. Kwa kasi ya haraka Daniel Mwaseba alichomoa bastola yake iliyokuwa upande wa kulia wa kiuno chake. Akawa anawaelekezea wale jamaa kwa zamu, mara kamuelekezea yule jamaa akiyepambana nae kabla, mara akiwaelekezea wale majamaa watu waliokuwa wanamfata. Wale majamaa hawakujari, walikuwa wanamsogelea tu Daniel Mwaseba bila uwoga wowote ule. Daniel alirudi nyuma mpaka aliufukia ukuta, akauegemea ukuta huku bastola yake akiwa kaielekeza mbele. Bila kusita wale majamaa watatu walikuwa bado wanamsogelea, bila kusema neno lolote lile. Ilikuwa kama hawaioni ile bastola aliyoishika Daniel Mwaseba. Au labda walikuwa wanaona Daniel Mwaseba kashika kijiti tu kidogo.
Hali ilikuwa ya hatari sasa!

Jamaa walisogea hadi wakafika pale ukutani, alipokuwa Daniel Mwaseba. Daniel hakutaka kupiga risasi alijua madhara ya kurusha risasi kwa watu ambao asiowajua wamejipanga vipi. Maana kujiamini kwao ilimaanisha wamejipanga vizuri kwa hali ile. Ilibidi asubiri aone watu wale wana nia gani huku akitafuta mpenyo wa kujitoa katika kisanga kile kibaya...

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
Umeweka sehemu fupi sana!

QUOTE=mapengo junior;12381561]Balaaa lipo mbele huko yaaan ucje ukamis kabisaaa[/QUOTE]
 
riwaya kama hii inafaa kuisoma mwanzo mwisho,hv unavyoweka kamojamoja hv unapoteza kabisa radha ya mchezo,kwa nn usiweke kuanzia mbili au tatu kwa siku?
 
riwaya kama hii inafaa kuisoma mwanzo mwisho,hv unavyoweka kamojamoja hv unapoteza kabisa radha ya mchezo,kwa nn usiweke kuanzia mbili au tatu kwa siku?

Munanchanya wengine isipite siku wengine tatu wengine moja...nimeshasema hii riwaya inapikwa now..au niache mpka iishe kuandikwa ndo niilete humu:what::what:
 
Mapengo wewe ndio dereva sisi abiria tu so unavyopanga ndio hivyo hii unatufanyia ihsani kwa hiyo endelea na utaratibu ulioupanga.
 
SIMULIZI; BALAA
Mwandishi; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA TISINI NA TANO

"Karibu sana kwenye nyumba ya kifo mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel Mwaseba!" Jamaa mmoja kati ya wale watu watatu waliokuwa wanatoka kule katika mlango wa ile nyumba ndogo alisema kwa nyodo na dharau kubwa sana.
Daniel Mwaseba hakujibu kitu chochote alikaa kimya huku akitafuta mbinu ya kutoka salama mahali pale, alitafuta kwa haraka namna ya kujiokoa sehemu ile ya hatari, lakini hakuipata!

Ghafla jamaa wale, wote watatu kwa pamoja waliruka juu na huku wakitanguliza mguu wa kulia mbele.
Yalikuwa mateke matatu kwa mpigo! Yaliyorushwa kwa ufundi mkubwa sana.
Mateke matatu yenye uzito tofauti toka kwa watu watatu tofauti yalitua katika kifua cha mtu mmoja, Daniel Mwaseba. Nguvu ya mateke yale yalimsukuma kwa nguvu Daniel Mwaseba katika ukuta na alijibamiza vibaya sana ukutani! Alisota katika ule ukuta na kudondoka chini taratibu.
Kabla hajainuka wale majamaa watatu walisogea kwa kasi pale alipokuwa amedondokea Daniel Mwaseba. Jamaa aliyekuwa amesimama upande wa kulia alirusha teke lengine kwa mguu wake wa kulia, na yule aliyekuwa amesimama upande wa kushoto nae alirusha teke kwa mguu wake wa kushoto, wakati yule wa kati alikuwa amesimama tu akiangalia ujuzi wa wale wenzake. Mashavu yote mawili ya Daniel Mwaseba yalikutana na shurba. Mateke yote mawili yale yalitua katika mashavu ya Daniel Mwaseba. Damu ziliruka toka katika mdomo wa Daniel Mwaseba. Daniel sasa aliona hakuna tofauti, kufa na kuishi vyote ni sawa, akiwa amelegea kidogo kutokana na mapigo ya wale jamaa aliinyanyua bastola yake tayari kwa kufyatua. Alimuelekeza yule mtu aliyesimama katikati ya wenzake, hakuwa na mzaha sasa Daniel, macho yake yalionesha hivyo. Alikuwa tayari kwa lolote!
Kwa bahati mbaya kabisa hakuwahi kufanya alichokuwa anataka kukifanya.
Yule jamaa aliyekuwa kati aliufyatua mguu wake kwa kasi ya haraka sana na kuupiga ule mkono wa Daniel Mwaseba ulioshika bastola. Kwa macho yake yote mawili Daniel Mwaseba aliishuhudia bastola yake ikiruka angani na kutua katika mikono ya yule jamaa wa kati.

E bwanaa wee!

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
Back
Top Bottom