Riwaya - Balaa

Riwaya - Balaa

Sawa ungetupia hata mbili za bonus for the long wait
 
mkuu unanikumbusha willy gamba Jinsi alivomfatilia kijana jimmy (James) ambaye kazi yake ilikua ni kuwabadilisha waonyesha mavazi pale "city hall" ili LULU binti mrembo awapagawishe watazamaji na genge la akina benny lifanye yao, HIYO NI KUFA NA KUPONA
 
Jana hola, leo hola, anyway tutaendelea kuchoma tu mahindi,haina kwere!
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI! HALFANI SUDY
SIMU; 0757633010

SEHEMU YA THEMANINI NA SABA

Kule kwa nje mpelelezi Daniel Mwaseba aliizunguka kwa umakini mkubwa ule ukuta mrefu uliokuwa umezunguka eneo lile. Pamoja na kuzunguka kwake lakini Daniel Mwaseba hakuipata sehemu muafaka ya kuweza kumruhusu kuingia katika nyumba ile. Ukuta ulikuwa imara na mrefu sana, kiasi kwamba Daniel Mwaseba pamoja na ujasiri wake wote lakini hakuona namna ya kuweza kuupanda ukuta ule. Daniel Mwaseba alikaa chini na kutafakari, akaona bora arejee wakati mwengine ili aweze kuvamia kambi ile na kuumaliza kabisa mchezo unaofanywa na watu wale. Daniel Mwaseba alirejea mjini kwenda kujipanga vizuri tayari kwa kuja kuifanya shughuli mzito atakaporejea tena.

Kule ndani kiongozi wa kundi la Six killers, Don Genge alikuwa anamuuliza maswali Tano, na Tano aliyajibu maswali yote kwa ufasaha na umakini mkubwa. Kwa jinsi Tano alivyowasimulia jinsi alivyotoka katika mdomo wa mamba watu wote walibaki midomo wazi. Walimpongeza Tano kwa ushujaa wake.

Pamoja na kumsifia sana Tano lakini taarifa za kuwepo kwa Daniel Mwaseba katika mji wa Kilwa Masoko zilomstua kila mmoja mle ndani. Katika watu waliokuwemo mle ndani hakuna aliyekuwa haijui habari ya Daniel Mwaseba. Walikumbuka vizuri sana jinsi alivyoangamiza na kuteketeza mpango hatari wa angamizo katika mji wa Iringa..

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA THEMANINI NA NANE

Huko mkoani Mtwara katika hospitali ya misheni ya Ndanda, hali za wagonjwa wa Dokta Yusha zilikuwa kidogo zinaendelea vizuri. Angalau Nasra Mpaukha, mke wa Dokta Yusha na Hasina Omary, mpambe wa Bi harusi na rafiki kipenzi wa Nasra sasa hali zao zilikuwa zinaleta matumaini.
Kwa upande wa Nasra sasa alikuwa anaweza kupumua mwenyewe bila ya msaada wa mashine. Sasa alikuwa anaweza kuongea kwa kupapasia ingawa hakuwa na kumbukumbu yoyote ya mambo yaliyotokea nyuma.
Hali ya Hasina ilikuwa mzuri zaidi. Alikuwa anakula na kuongea kama kawaida na kidogo alianza kurejewa na kumbukumbu ya yaliyotokea nyuma. Kutengamaa kwa hali za watu hao wawili zilimtia faraja sana Dokta Yusha, maana aliona dhamira yake ya kwenda Kilwa, kuwakomboa watu wa Kilwa juu ya sakata lile la kutisha ilikuwa inaelekea kutimia, tena matumaini yaliongezeka siku baada ya siku.

Dokta Yusha aliendelea kukaa hospitalini Ndanda, kuziangalia hali za wagonjwa wake kwa siku tatu zaidi. Siku ya nne Dokta Yusha alikuwa ndani ya basi la Nsungia akielekea Kilwa Kivinje. Aliamua kwenda kuanzia kilwa Kivinje akiamini ndipo mahali sahihi lilipoanzia suala hili na ndipo ataenda kulimaliza.

Gari lilipofika Kilwa Kivinje. Dokta Yusha alikuwa abiria wa wa tatu kushuka katika basi la Nsungia. Moja kwa moja alianza kutafuta nyumba za mahasimu wake.
Saa nane mchana ilimkuta Dokta yule kijana, Dokta Yusha akigonga bila wasiwasi wowote katika mlango wa nyumba ya dokta katiri wa kike, Dokta Sharifa Juma...

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757633010

SEHEMU YA THEMANINI NA TISA

Dokta Yusha aligonga hodi mara tatu mlango wa Dokta Sharifa Juma, alisimama kidogo baada ya kugonga ile mara ya tatu akisikilizia ndipo alisikia kelele za miguu ya mtu ikielekea pale mlangoni ishara kuwa kuna mtu alikuwa anaenda kufungua ule mlango. Dokta Yusha alijipanga vizuri pale mlangoni, tayari kwa lolote kitakachotokea pale mlangoni. Mlango ulifunguliwa, msichana mmoja mdogo mwenye umri kati ya miaka kumi na sita na kumi na nane ndio alienda kufungua ule mlango.

"Shikamoo kaka" Yule msichana alimsalimia Dokta Yusha pale mlangoni.
"Marhaba hujambo binti" Dokta Yusha aliitikia ile salamu huku macho yake yakiangalia moja kwa moja hadi ndani ya nyumba ile.
"Sijambo kaka" Msichana aliitikia kwa sauti yake ya upole.
"Dokta Sharifa nimemkuta?" Dokta Yusha alitupa karata yake kwa kumuulizia adui yake. Alijitahidi kuuliza kwa sauti ya kawaida kuficha hasira zake kwa Dokta huyo.
"Hapana, dada hayupo" Yule msichana alijibu.
"Kaenda wapi?" Dokta Yusha aliendelea kumuhoji yule dada.
"Dada siku ya tatu leo hajarejea nyumbani, na simu yake haipatikani sijui hata yuko wapi?" Yule msichana alielezea kwa kirefu.
Dokta Yusha akajua mambo sasa yameiva. Kwa vyovyote Dokta Sharifa na wanaharam wenzie watakuwa sehemu fulani, wakiwa wanapanga mambo yao, na pengine kuamua kuzima simu kabisa ili kupunguza bugdha toka kwa watu.
Dokta Yusha aliwaza hayo kwa haraka kichwani mwake, huku mdomoni mwake akitoa jibu.
"Sawa binti"
"Akija dada nimwambie alikuja nani?" Msichana yule aliyeonesha dalili ya uwerevu mkubwa aliuliza.
"Mwambie alikuja Dokta makini, Dokta mwadilifu, Dokta mchapakazi, utakumbuka hilo jina?"
"Ndo jina lako hilo? Nitalikumbuka" Msichana alisema huku akitabasamu.

Dokta Yusha alimuaga yule msichana mwerevu anayefanya kazi kwa Dokta katili sana na kuondoka zake. Sasa alielekea nyumbani kwa Dokta mwengine katili, Dokta Zaidi Kilumba. Huko alikutana na kijana wa kiume mlangoni. Mdogo wake na Dokta Zaidi Kilumba, naye alimpa taarifa zilezile kama alizozipata nyumbani kwa Dokta Sharifa Juma, habari za kutoonekana Dokta Zaidi Kilumba nyumbani kwake kwa siku tatu..

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA TISINI

Kengele ya hatari ikagonga kichwani kwa Dokta Yusha. Iweje dokta Zaidi Kilumba na Dokta Sharifa Juma wote wasirejee nyumbani kwao kwa siku tatu? Kuna nini kinachoendelea. Dokta Yusha alitamani apafahamu kule katika kambi ya mateso alikopelekwa kabla, lakini hakuwa anajua kabisa njia ya kumfikisha kule.
Dokta Yusha aliamua kutembelea katika nyumba za wale manesi watano waliokuwemo katika mpango huu hatari. Aliowaona siku ile na aliwakumbuka vizuri sana. Ingawa kwa shida lakini alizipata nyumba zao kwa kuulizia kwa watu, nako ujumbe ulikuwa uleule. Wahusika wote wa mauaji yale ya kikatili walitoweka majumbani mwao kwa takribani siku tatu.

Dokta Yusha aliamua kwenda Kilwa Masoko alihisi labda huko atapata kitu cha kumsaidia kujua chochote juu ya sakata hili hatari.

Siku hiyo usiku ulivyoingia ndio Daniel Mwaseba alikuwa anarejea tena kule porini, Ngome. Kuona jinsi ya kulisambaratisha kundi hatari la Six Killers. Mchana wa siku ile alienda katika kituo cha polisi Masoko na kupewa baadhi ya vitu akivyovihitaji, ikiwemo na pikipiki kwa ajili ya kumfikisha kule porini.

Sasa Daniel Mwaseba akiwa katika chumba chake katika hoteli ya Kimbilio, alivaa suruali nyeusi aina ya jeans pamoja na T-shirt nyeusi yenye matirio ya mpira iliyombana vizuri katika mwili wake. Chini alivaa raba nyeusi vyepesi maalum kwa ajili ya mapambano. Upande wa kulia na wa kushoto kiunoni mwake alikuwa na bastola, moja kila upande. Huku mgongoni akiwa na begi dogo jeusi alimoweka kamba pamoja na zana zingine kwa ajili ya kwenda kukamilisha kazi yake hii hatari.
Nyuma ya pikipiki lake aina ya Kawasaki ambalo lilikuwa linamsubiri kwa nje aliweka chuma kikubwa na kizito maarufu kama nanga pamoja na kama ngumu ya mwani. Saa sita ya usiku aliwasha pikipiki yake kwa mwendo wa taratibu na kuelekea porini ngome...

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY.
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA TISINI NA MOJA

Alipofika karibu na ile nyumba Daniel Mwaseba aliipaki pikipiki yake pembeni mbali kidogo na lile eneo la kambi ya kundi la Six Killers. Akihofia kelele za pikipiki yake kuwastua watu waliokuwepo ndani ya kambi ile hatari. Daniel Mwaseba aliifungua ile nanga nyuma ya pikipiki yake. Aliibeba ile nanga hadi pembezoni mwa ukuta mrefu wa kambi ile.

Daniel Mwaseba akafikiria namna sahihi ya kuingia mle ndani kwa kutumia ile nanga, lakini aliikosa, alichokuwa anafikiria kuja kukifanya na ile nanga ilikuwa sivyo. Daniel Mwaseba alipiga mahesabu yake vibaya.
Akaiacha ile nanga pale chini. Akaamua kupiga hatua za kimyakimya kwenda katika geti la mlango ule. Alihisi labda hapo nd'o patakuwa sehemu sahihi patapomuwezesha kuingia ndani ya kambi ile hatari.
Alichunguza kwa makini kama dakika kumi pale getini ili kupata namna ya kuingia mle ndani, lakini bado hakupata sehemu sahihi ya kuingia mle ndani. Six Killers walikuwa wamejipanga vizuri sana kiulinzi na usalama.

Daniel Mwaseba aliamua kurejea tena upande wa kushoto alikoiacha ile nanga yake. Alifika hadi pale alipoiacha ile nanga, akaipita tu kama hajaiona na kuelekea mbele zaidi. Alitembea hafi akafika nusu ili aumalize ule ukuta. Aliangalia pembeni, akauona mti mrefu pembezoni zaidi ya ule ukuta. Akili za Daniel Mwaseba zikafanya kazi kwa kasi ya haraka. Mithili ya nyani aliupanda ule mti hadi juu. Kwa kutumia taa zao zenye mwanga hafifu sasa alishuhudia ramani nzima ya ile kambi. Kwa kutumia macho yake Daniel alipima umbali toka pale kwenye mti alikokuwepo hadi kwenye ule ukuta. Ulikuwa umbali mkubwa, lakini aliona inawezekana. Daniel Mwaseba alipitisha uamuzi wa kujirusha toka kule mtini ili adondokee mle ndani. Haikuwa kazi rahisi kama unavyoweza kufikiria. Ilikuwa kazi ngumu sana inayohitaji mtu wa kufanya hivyo awe na roho ya kijasiri, roho ya kikomando, roho ya paka! Ambayo bila shaka Daniel Mwaseba alikuwa na roho ngumu zaidi ya hizo....

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
Mwandishi; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA TISINI NA MBILI

Daniel Mwaseba alijirusha bwana toka kule mtini. Alielea hewani mithili ya samaki mkizi. Alipofika ndani ya ile kambi, Daniel Mwaseba alipata maumivu ya mguu kutokana na umbali ule mrefu aliojirusha. Daniel alisimama kivivu, alijinyoosha kidogo viungo vyake ili kujiweka sawa. Kabla hajafikiria chochote cha kufanya alisikia sauti ya ukelele wa miguu kuelekea pale alipokuwa. Ishara kwamba kuna mtu alikuwa anaelekea pale alipokuwa. Daniel Mwaseba alijibana ukutani akisaidiwa kwa kiasi kikubwa na giza la usiku. Huku akizishukuru taa za mle ndani kwa kutoa mwanga hafifu. Akatulia kidogo, akaangaza huku na huko
Alikiona!
Daniel Mwaseba alikiona Kivuli cha mtu kikielekea pale alipoangukia awali, akajua bila shaka alikuwa amesikia kishindo chake kile cha kuchumpa. Daniel Mwaseba akasimama imara, akijua muda muafaka wa kupambana umefika.
Yule jamaa, ambaye alikuwa Mbili wa Six Killers alisimama pale alipoangukia awali Daniel Mwaseba, huku akiwa kampa kisogo Daniel. Daniel Mwaseba akaona ile ndio nafasi pekee ya kuitumia. Alimsogelea Mbili kwa mwendo wa taratibu sana, mwendo wa kunyata, hakuruhusu kelele yoyote katika msogeo wake, alimkaribia sana Mbili. Mbili alikuwa kasimama vilevile. Daniel Mwaseba alikunja ngumi, akaurudisha nyuma mkono wake, mkono ule ambao alikuwa amekunja ngumi aliuleta mbele kwa nguvu sana, usawa wa uti wa mgongo wa Mbili wa Six Killers. Daniel Mwaseba alivyotegemea haikuwa hivyo. Ule mkono uliokunjwa ngumi ulikosa wa kumpiga....

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
Mapengo unanpa presha na vdonda vya 2mbo kwa ajl ya subra.hujui kuwa riwaya hii n nzur na haikupaxwa icpte hata ck 1 bla kuxomwa?
 
Back
Top Bottom