Hawa CHADEMA na Slaa wao kwa kweli sasa wafahamu wanajishushia credibility na hizi tired, cheap stunts zao zisizoisha. Sasa kuongeza nobodys kama Bharati Goda na John Kato, au Wanasiasa wazee waliokwisha achia ngazi kama Philipi Mangu'la na John Malecela kwenye orodha ya Mafisadi, kutasaidia nini this time around wakati wale waliotajwa awali hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yao, na in fact, bado wana vyeo vyao na mali zao intact. Kulialia "Wolf!" "Wolf!" kila mara mwisho wake watu wataacha ku-pay attention. Lengo kubwa nadhani wanategemea kuwa kwenye continuous public spotlight ili waonekane bado wako relevant, lakini wafahamu wanapoteza muda na resources nyingi kuelekea 2015, ambazo wangezitumia kujizatiti at grassroots level haswa kupitia kura za Vijana kwenye rural areas.
Hata mimi nimepata tabu na timing, individuals waliotajwa na uharaka wa kujata "mafisadi" wapya. Itakumbukwa lengo la ziara za mikoani ilikuwa ni maandamano ya issue za rasimu ya katiba. Lakini Serikali ime-preempt kwa kuutoa ili ukarekebishwe, nadhani hapa ndio ikabidi kutafuta cha kusema na sbb ya mabadiliko ndani ya CCM ikabidi waangukie ghafla kwenye kutaja mafisadi. Matokeo yake yametajwa majina ambayo aidha hayapo tena kwenye active politics za CCM (part-timers) pia na kashfa ambazo zimeshakuwa kama nyimbo eg nyumba za serikali na EPA. Wakati mwingine inabidi kuwa realistic kuisaidia CHADEMA tusiwe rigid.
Ikumbukwe wanamtandao baada ya JK kushinda walimshambulia sana Maghufuli kwa kilichoitwa "kumuuzia" nyumba ndogo yake nyumba ya Serikali. Na inavyoonekana watz walishapuuzia hilo na iman yao kwa maghufuli bado iko juu.
Mangula na Malecela ndo kabsa. Mangula ashajichokea na inawezekana wkt mwngne husahau hata kama alishakuwa mwanachama wa CCM achilia mbali ukatibu mkuu.
Malecela naye mara ya mwisho kuhusishwa na EPA ilikuwa na mtetezi Mkuu wa mafisadi Sophia Simba ambapo alimshauri akapimwe akili Mirembe.
Sijajua mantic ya kutaja underdogs wa Kagoda. Eti kina Goda. Wafanyakazi wa Caspian ukimuacha bosi wao.
Mi nadhani Slaa angejita kwanza ktk kushinikiza kwanza akina Nape Nauye wawataje hadharani wanaowaita mafisadi badala ya kudai wajitoe wajitoe (hawajulikani na haijulikani wanajitoa kwenye uongozi na ktk chama). Pili angewataka kama kweli wanajivua gamba basi serikali ya CCM iwapeleke mahakamani hao inaowaita mafisadi (sio tena watuhumiwa wa ufisadi). Vinginevyo sijaona jipya hapo!
Kuna ufisadi mwingi unafanyika kila leo kwenye ujenzi wa mabarabara, pembejeo za kilimo, vitambulisho vya taifa, mashirika ya umma, miradi ya ujenzi, noti mpya, you name it. Zile ambazo zilishafumuliwa tudai hatua zichukuliwe kwa wahusika.
Sina hakika kama mafisadi ndio walioandaa hiyo hotuba ya Tabora. Lakini nina imani kubwa kuwa kwa mara ya kwanza hotuba ya Slaa ya jana imewafariji mafisadi kwa kiasi kikubwa!