ng'wanankamba
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 346
- 120
Hii nafasi kwa nini haikutangazwa kupitia Tume ya ajira ili kila mwenye sifa akaomba ili kupata mtu mwenye ujuzi na uzoefu sahihi?
Rished Bade, ni msomi anastahili kuchukuwa nafasi hiyo.
CV yake alikuwa chuo kikuu cha Dar mwaka 1992 hadi 1995 akisomea B.com alipata masomo yote daraja A kwa miaka yote mitatu kwa masomo yote hakuwahi kupata hata B+ ni rekodi ya kutukuka. Baada ya hapo aliajiriwa na Benki Kuu, Baadaye alikwenda Akiba commecial benki kama mmoja wa wakurugenzi wake, Baclays akawa afisa mtendaji mkuu na alisoma Masters katika vyuo vya nje sina hakika kama amesoma PHD lakini ni kichwa na mzalendo kupita kiasi.
Kuna kusoma na kuelimika. Unaweza kuwa na kundi kubwa la wasomi nchi nzima lakini hawajaelimika. Hawana maarifa. Hawana uwezo wa kutumia elimu waliyoipata kwa faida ya jamii yao.
Elimu ni changamoto kubwa sana katika suala zima la mikataba kama ilivyo kwa uroho, tamaa, ulafi, wizi, uwongo, uzushi, kutokuwa makini, ulalamishi, ufisadi uliokithiri, kutotosheka nk.
Kuwa na rundo la wenye vyeti sio kuwa na wasomi. Wasomi ni wale wenye uwezo wa kutafsiri elimu zao walizopata ndani na nje ya Darasa kubadili maisha ya jamii zao.
Nitakupa mfano wa wasomi walioshindwa kutumia elimu zao na hivi sasa wanaonekana kama tumaini kwa serikali ya CCM. Prof. Muhongo - alikuwa mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO mwaka 2005. Aliruhusu Kiwira kuuzwa kwa Mkapa, Yona na wenzake. Alikuwa mshauri mtaalamu kwa kampuni ya Sutton Resources ilipokuwa inauza mgodi wa Bulyanhulu kwa Barrick. Alikuwa kwenye timu iliyoandika sera ya madini ya mwaka 1997 na sheria ya madini ya mwaka 1998 ambayo ndio chanzo cha mikataba ya sasa ya madini ambayo imeligharimu sana Taifa.
Huyu ni msomi lakini at the hour of need hakusaidia jamii yake. Hata tulipokuwa tunahangaika (ukiwemo wewe MwanaKijiji) kuleta mabadiliko katika sekta ya madini hakupaza sauti yake. Hawa ndio wasomi wetu.
Ninapingana na hitimisho lako ambalo ndio ulianza nalo kwenye kichwa, mikataba mibovu inatokana na elimu mbovu. Elimu ambayo inaangalia maslahi binafsi badala ya maslahi ya Umma.
NDIO TATIZO
![]()
kwa hiyo CV,jamaa anatisha....big up mr bade,we are expecting more changes with few ufisadi...
Naijua sana hii familia na namjua sana huyu kijana.
Ni mdogo wake Iliasa na mdogo wake Gale. dada yao alisoma na mke wangu. Ni watoto wa kinondoni hawa.
Kijana ni mzuri sana na alisomea Forodhani sec alipata Point 7.
Wakti naondoka Tz alikuwa BOT.
Hichi ni kichwa sana na pasi na shaka yoyote atawasaidia sana kukuza uchumi wenu uliodorola.
Watu hawa ni hazina kwa aifa la wenye mapenzi na nchi yao
Hongera sana Rished Mohamed Bade
Kuhusu performance yake Bacrays kwa harakaharaka naweza kusema ni mbaya, sababu ndio alisambaza vibranch vingi sana ambavyo vimeshindwa kupay off kiasi kwamba sasa bacrays inafanya downsizing.
Barubaru hakuna anayepinga hayo uliyosema na issue hapa wala si uwezo wa darasani mkubwa, mimi pia nilisoma Forodhani na ni mtoto wa Temeke. Je umepata muda wa kupitia yaliyosemwa kuhusu uongozi wake Barclays? Mungu bariki jk si JK Nyerere otherwise Rished asingepata huo uteuzi, niko na hard facts kwenye hili. Wote tunajua namna ambavyo uadilifu si kigezo tena cha mtu kuteuliwa kwenye nyadhifa sensitive kama hii katika awamu hii ya uongozi na sababu ni obvious kwamba hao wanaoteua pia si waadilifu hivyo ni vigumu kuteua waadilifu.
Mkuu naona unaijua vizuri hiyo stori. Watoto wa mujini walianzisha kampuni na kuajiri wafanyakazi hewa kisha kupeleka payroll hewa na kupewa mikopo ambayo haikulipwa!! Kwani baada ya pale alienda Nairobi au alienda Mortgage Finance?Kimbunga,
Mpango wa Retail Expansion haukuwa mpango wa Rished Bade.Huo mpango ulikuwa wa Barclays Emerging Markets (Kutoka Dubai makao makuu) , kina Rished waliletewa tu wautekeleze. Sasa tatizo kubwa lilitokea pale ni kwenye Personal Loans maana wabongo kama unavyowajua. Walitaka kuiga Barclays Kenya wakati kule wenzetu wana system nzuri za identification. Nadhani kama ingekuwa ni failure ya Rished kama yeye binafsi wasingempa kazi nyingine kule Nairobi wangemtimua tu!
![]()
Mr. Rished Bade
Rished started his career in banking in 1995 with Bank of Tanzania as Bank Examiner where he worked for five years. He then joined Akiba Commercial Bank (ACB) in June 2000 as a Credit Manager. A year later, he joined the Barclays Bank as Director of Finance at Barclays Bank Tanzania, a position he held for five years before moving to Barclays Bank Uganda. At Barclays Bank Uganda, Rished was the Chief Operating Officer for 2 years before he was appointed Country Managing Director for Barclays Bank Tanzania in January 2007. In December 2009 he was appointed Group Chief Finance Officer for Barclays East and West Africa Cluster stationed in Nairobi Kenya, the position he held until he joined Tanzania Mortgage Refinance Company in November 2010
kitilya kajaza wakina mangi TRA,utadhani mtu uko kibosho kumbe ni TRA,hii nchi bana