Rished Bade kumsaidia Kitillya TRA

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished Bade kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).​

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Septemba 19, 2012 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais - Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo umeanza Jumatatu wiki hii, Septemba 17, 2012.​

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Bade alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Mortgage Finance Co. Ltd.​

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Septemba, 2012
 
Hongera sana "dogo" halafu Kichwa Rished.........sitoshangaa huyu kijana kuja kuteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu.....watch!
 
Huyu jamaa alikuwaga MD wa Barclays. So anakwenda kuchukua nafasi iliyokuwa imeachwa na Bw Luoga. Labda ndio maandalizi ili Kitillya akistaafu yeye ndo achukue hiyo post.

Sina CV yake kwa kirefu zaidi, mwenye nayo atumwagie hapa tuichambue jamani!
 
Rished-Bade.jpg

Mr. Rished Bade
Rished started his career in banking in 1995 with Bank of Tanzania as Bank Examiner where he worked for five years. He then joined Akiba Commercial Bank (ACB) in June 2000 as a Credit Manager. A year later, he joined the Barclays Bank as Director of Finance at Barclays Bank Tanzania, a position he held for five years before moving to Barclays Bank Uganda. At Barclays Bank Uganda, Rished was the Chief Operating Officer for 2 years before he was appointed Country Managing Director for Barclays Bank Tanzania in January 2007. In December 2009 he was appointed Group Chief Finance Officer for Barclays East and West Africa Cluster stationed in Nairobi Kenya, the position he held until he joined Tanzania Mortgage Refinance Company in November 2010
 
Hongera sana Kichwa Rished.........
Tunapigaga hizi-hizi, mara kichwa, mara miguu badae kinatuwakia

cha maana ni kujua qualities.......... kusifia bila substance haina maana yoyote

Sijui performance yake jamaa, ila najua akiwa Barclays walipanda, lakini mwishoni walipigwa-pigwa sana, na majungu yakashika njia

hongera
 
Mkuu the heading doesn't match with content.
Amrithi na naibu kamishna mkuu wa TRA ni vitu viwili tofauti.
Kitilya na comission general TRA sio naibu.
Alafu hii sio ya jukwaa la siasa.
Be greater thinker.
 
Halisi
futa maneno yako famillia ya kitillya itakumaliza kumstaafisha mzee wao kabla muda aujaisha loh
 
Mapungufu ya katiba haya, uteuzi kila kukicha nyadhifa kibao. Hapa integrity ya anaeteuliwa ni kwa discretion ya Rais na si utendaji wa aliepewa nafasi hii.
 
Rished-Bade.jpg

Mr. Rished Bade
Rished started his career in banking in 1995 with Bank of Tanzania as Bank Examiner where he worked for five years. He then joined Akiba Commercial Bank (ACB) in June 2000 as a Credit Manager. A year later, he joined the Barclays Bank as Director of Finance at Barclays Bank Tanzania, a position he held for five years before moving to Barclays Bank Uganda. At Barclays Bank Uganda, Rished was the Chief Operating Officer for 2 years before he was appointed Country Managing Director for Barclays Bank Tanzania in January 2007. In December 2009 he was appointed Group Chief Finance Officer for Barclays East and West Africa Cluster stationed in Nairobi Kenya, the position he held until he joined Tanzania Mortgage Refinance Company in November 2010

Excellent resume.... with sprinkles of very short life spans in the executive positions:wacko:
 
Rished-Bade.jpg

Mr. Rished Bade
Rished started his career in banking in 1995 with Bank of Tanzania as Bank Examiner where he worked for five years. He then joined Akiba Commercial Bank (ACB) in June 2000 as a Credit Manager. A year later, he joined the Barclays Bank as Director of Finance at Barclays Bank Tanzania, a position he held for five years before moving to Barclays Bank Uganda. At Barclays Bank Uganda, Rished was the Chief Operating Officer for 2 years before he was appointed Country Managing Director for Barclays Bank Tanzania in January 2007. In December 2009 he was appointed Group Chief Finance Officer for Barclays East and West Africa Cluster stationed in Nairobi Kenya, the position he held until he joined Tanzania Mortgage Refinance Company in November 2010
kwa hiyo CV,jamaa anatisha....big up mr bade,we are expecting more changes with few ufisadi...
 
Tunapigaga hizi-hizi, mara kichwa, mara miguu badae kinatuwakia

cha maana ni kujua qualities.......... kusifia bila substance haina maana yoyote

Sijui performance yake jamaa, ila najua akiwa Barclays walipanda, lakini mwishoni walipigwa-pigwa sana, na majungu yakashika njia

hongera

janjaweed, umenena bhana,,,,,then baadae kauli zinakanwa
 
Hongera sana "dogo" halafu Kichwa Rished.........sitoshangaa huyu kijana kuja kuteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu.....watch!

Ogah una uhakika na hicho ulichoandika? Je unajua sababu ya yeye kupelekwa Nairobi baada ya kuondolewa uMD Barclays TZ? Waulize aliofanya nao kazi, ninahakika jamaa ni kipanga wa darasani kupata first class n.k but sina hakika kama ni kipanga pia kiutendaji.
 
Back
Top Bottom