Rished Bade ateuliwa kuwa Kamishna Mkuu Mpya TRA

Rished Bade ateuliwa kuwa Kamishna Mkuu Mpya TRA

frema120

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2012
Posts
5,098
Reaction score
1,341
Rais JK kamteua Bwn RISHED BADE kuwa kamishina mkuu wa TRA Tanzania leo
===========================================================

1a0dRished-Bade.jpg

Rished Bade


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana
Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, uteuzi huu umaanza tarehe 06 Mei,
2014. Bwana BADE anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu
tarehe 14 Desemba,2013.

Kabla ya uteuzi huo, Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
tangu Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangia Bwana Kitilya alipostaafu.

Kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi kufanya kazi
katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa kwenye mambo ya fedha na mapato
kama ifuatavyo:-

Oktoba, 1995 – Mei, 2000 – Mkaguzi wa Benki za Biashara, Benki Kuu ya Tanzania.

Juni, 2000 – Juni, 2001 – Credit Manager, Akiba Commercial Bank.

Juni, 2001 – Septemba,2001 – Chief Financial Officer, Akiba Banking Corporation.

Septemba, 2001 – Machi, 2006 – Chief Operating Oficer, Barclays Bank (Uganda).

Januari, 2007 – Desemba, 2009 – Chief Executive Officer, Barclays Bank (Tanzania)

Desemba, 2009 – 2012 – Chief Financial Officer, (East and West Africa Cluster) Barclays Bank
Plc Emerging Markets.

Novemba, 2010 – Septemba, 2012 – Chief Executive Officer, Tanzania Mortgage Refinance
Company.

Bwana Rished BADE ana Shahada ya Kwanza ya Bachelor of Commerce and Management ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (1995); Shahada ya Master of Commerce in Banking and Finance ya Chuo
Kikuu cha Sydney (1999), na ni Certified Public Accountant (CPA).

Katika kumteua kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mheshimiwa Rais ana
imani kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished Bade kwa kushirikiana na
watumishi wenzake, atatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwa kuzidi kuimarisha Mamlaka hiyo na
kuboresha utendaji wake na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa faida ya Taifa.


Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
Salute to all JF Great Thinkers..

Naamini waheshimiwa wengi tu wanakuja kuchungulia hapa JF na kujua yanayojiri ndani ya jamii.

Taarifa iliyopo ni kuwa TRA wamepata boss mpya, pasi na kujali elimu na ujuzi alionao, kamwe hawezi kujua kero zote zinazowakabili walipa kodi..ikiwezekana tumpe inputs,kero,ushauri ili kama ataweza kuzitafutia ufumbuzi well and good, kama hataweza basi ajue kuwa zipo na zinakera...huwezi kujua, kila mtu ana style ya utendaji kazi wake, wengine wanapenda ushauri na kuzifanyia kazi na wengine hawaambilikiz, jukumu letu ni kupiga mayowe tunapohisi the game is not fair..

1. Nimeona watu wengi humu wanalalamikia sana ushuru wa ku import gari nchini uko juu sana.
2. Andaa njia rahisi ya watu kulipa kodi,ushuru i.e online payments kadiri iwezekanavyo kuokoa muda na usumbufu wa kutoa rushwa..watu hawapendi kwenda TRA offices kukwepa usumbufu wa kubambikiziwa unfair taxes.etc
3. Annual motor vehicle licence fees inatuua Mr. Bade (you can not enrich poor people by making rich people poor - Ex U.S President A. Lincoln)
4. Viwango vya kodi na ushuru viwe reasonable na realistic ili zisiforce watu kukwepa kulipa that leads to tax evasion..fair taxes encourage taxpayers to pay voluntarily.
5. Tengenezeni website/blog yenu watu wapost complains zao humo.

Nawapisha wadau wengine muongeze hapo, nitarudi tena.

However, tunakutakia kila la heri Mr Bade.
 
ni Rished Bade na anamuapisha leo juu kwa juu akiwa Lagos
 
Huyu anastahili kabisa nafasi hiyo,toka ameingia tra binafsi nimeshuhudia mabadiriko makubwa ya kiutendaji katika taasisi hiyo.

Naamini uzoefu wake huko nyuma haukuwahi kumpa fursa ya kujifunza mazoea ya rushwa,hivyo sababu kapewa rungu kabisakabisa nategemea kuanza kuona tra inayojiweka mbali na rushwa.

Ile collection target anazowapa manager zitakuja kuleta matatizo huko mbeleni,yaani unakutana na ofisa wa tra akiwa yuko nyuma sana ya target mpaka anampigia magoti mlipa kodi alipe tu hata azididhe kidogo next quarter watabalasinsha. I like the pessure.
 

New+Picture+(5).bmp

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, uteulzi huu umaanza tarehe 06 Mei, 2014. Bwana BADE anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu tarehe 14 Desemba,2013.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangu Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangia Bwana Kitilya alipostaafu.

Kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi kufanya kazi katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa kwenye mambo ya fedha na mapato kama ifuatavyo:-

 Oktoba, 1995 – Mei, 2000 – Mkaguzi wa Benki za Biashara, Benki Kuu ya Tanzania.
 Juni, 2000 – Juni, 2001 – Credit Manager, Akiba Commercial Bank.
 Juni, 2001 – Septemba,2001 – Chief Financial Officer, Akiba Banking Corporation.
 Septemba, 2001 – Machi, 2006 – Chief Operating Oficer, Barclays Bank (Uganda).

 Januari, 2007 – Desemba, 2009 – Chief Executive Officer, Barclays Bank (Tanzania)
 Desemba, 2009 – 2012 – Chief Financial Officer, (East and West Africa Cluster) Barclays Bank Plc Emerging Markets.
 Novemba, 2010 – Septemba, 2012 – Chief Executive Officer, Tanzania Mortgage Refinance Company.

Bwana Rished BADE ana Shahada ya Kwanza ya Bachelor of Commerce and Management ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1995); Shahada ya Master of Commerce in Banking and Finance ya Chuo Kikuu cha Sydney (1999), na ni Certified Public Accountant (CPA).

Katika kumteua kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mheshimiwa Rais ana imani kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished Bade kwa kushirikiana na watumishi wenzake, atatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwa kuzidi kuimarisha Mamlaka hiyo na kuboresha utendaji wake na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa faida ya Taifa.

“Mwisho”
Imetolewa na:

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
08 Mei, 2014

Maoni binafsi: Mwandishi ajaribu kuangalia upya uandishi na matumizi ya lugha katika Habari kutoka Ikulu.Kwa mfano,hakuna Shahada ya Bachelor of..........
 
Mods unganisheni thread hii na ile nyingine ili iwe rahisi kufuatilia hasa jamaa mteuliwa atatulisha majani ama ni neema ?
 
Hongera Bw Bade , una kazi kubwa ya kufanya kuondokana na rushwa TRA, Lakini pia kodi zimekuwa nyingi sana kwa mtanzania, yaani mtanzania wa kawaida kununua Gari ni dhambi kuubwa sana, atatotozwa kodi mpaka basi, walau mkae chini mrekebishe format ya matozo ya magari mnawaibia sana watanzania.
 
Back
Top Bottom