Ripoti zote za CAG, siuoni ufisadi wa Lowassa

Ripoti zote za CAG, siuoni ufisadi wa Lowassa

Tunawangoja viongozi wetu wa CHADEMA watuambie kuwa ule uzushi wa kusema Lowasa fisadi waliutoa wapi......

Na ule ushahidi waliosema kuwa wanao juu ya ufisadi wa Lowasa umeyeyukia wapi.....??

Au waitishe mkutano wa waandishi wa habari wakiri kuwa walimsingizia mzee wa watu....na wamuombe msamaha kwa kumchafulia jina lake.......
Mmh! Lakn kweli, cdhan kama watafanya ivoo
 
Tunawangoja viongozi wetu wa CHADEMA watuambie kuwa ule uzushi wa kusema Lowasa fisadi waliutoa wapi......

Na ule ushahidi waliosema kuwa wanao juu ya ufisadi wa Lowasa umeyeyukia wapi.....??

Au waitishe mkutano wa waandishi wa habari wakiri kuwa walimsingizia mzee wa watu....na wamuombe msamaha kwa kumchafulia jina lake.......
Mimi nangoja ushahidi wa kitaalamu wa CAG na sio maneno ya wanasiasa.
Lowasa fisadi.....teheteheteheeeee.......thibitisha
 
Unajua sababu za kutimuliwa kwake na Mwl Nyerere, asigombee urais mwaka 1995? Je unajua alitimuliwa kazi ya uwaziri wa ardhi enzi za Mwinyi?

Umdogo sana kwenye siasa
Yeyote aliye mwizi na apelekwe mahakamani!
kama ushahidi haupo na mnyamaze kimya milele. Maneno maneno hayasaidii...
 
lowasa ameifisadi sana hii nchi Richmond kwa siku analipwa tsh milioni 152 na tanesco pesa zake ameinunua Chadema hatimiliki ya Chadema ipo nyumbani kwake Monduli
kwani CAG hakuliona hilo?
Mbona kwenye rport yake halimo?
 
Lowassa tapeli tu kama matapeli wengine.

We Chakaza hebu jiulize. Endapo huyo tapeli angegombea kupitia CCM, na akajisafisha kuwa mwenye ushahidi aende mahakamani, bado mngemtetea?

Magufuli tu huyu mnamwandama kwa kesi ya nyumba za serikali, kesi ambayo lilishawahi kufafanuliwa vizuri na Sumaye (campaign manager wa Lowassa) lakini mnajisahaulisha na kurudia rudia kila uchwao, seuze huyo mamvi?

Ni wenu tu huyo, pigeni nae picha!
 
Tatizo unafiki tu.

Fine! Tuseme Lowassa siyo fisadi,sasa huoni kwamba wewe ni mpumbavu kwa kuendelea kuwaamini hao waliokukaririsha Lowassa Ni fisadi kwa miaka 8? Huoni kwamba unatutangazia kwamba hujitambui?

Kipindi bwana zenu wanatangaza list of shame mbona mlikuwa hamuwapingi badala yake mlikuwa mnakenua tu.

Kama mmeamua kushikiwa akili basi tafuteni watu wenye akili timamu ndiyo muwape otherwise kila siku mtakuwa mnaonekana wapumbavu tu.

Msiojielewa ndiyo mtaji kwa wanasiasa maanake mnakaririshwa tu kama kasuku wala hamhoji halafu mnakimbilia huku kututangazia viwango vyenu vya umbumbumbu.
Mwakyembe na genge lake ndiyo walimchafua, na kuuaminisha umma kuye Lowassa ni Fisadi.. Na hata kwenye kampeni za kumpigania magufuli alimtaja Lowassa kwamba ndiye mmiliki wa Richmond ..
 
Duuu isije ikawa Magufuli ana mlia timing Lowasa ,si unajua tena kumchinja kobe ,labda miaka miwili mbele kesi yake itanguruma ,kwa influence aliyo nayo Lowasa sasa naona inamuwia vigumu ,vinginevyo ni majungu tu ya wanasiasa hakuna asiyekula keki ya taifa hili akimgusa Lowasa Mkwere ajiandae
 
Tatizo unafiki tu.

Fine! Tuseme Lowassa siyo fisadi,sasa huoni kwamba wewe ni mpumbavu kwa kuendelea kuwaamini hao waliokukaririsha Lowassa Ni fisadi kwa miaka 8? Huoni kwamba unatutangazia kwamba hujitambui?

Kipindi bwana zenu wanatangaza list of shame mbona mlikuwa hamuwapingi badala yake mlikuwa mnakenua tu.

Kama mmeamua kushikiwa akili basi tafuteni watu wenye akili timamu ndiyo muwape otherwise kila siku mtakuwa mnaonekana wapumbavu tu.

Msiojielewa ndiyo mtaji kwa wanasiasa maanake mnakaririshwa tu kama kasuku wala hamhoji halafu mnakimbilia huku kututangazia viwango vyenu vya umbumbumbu.

Weka kumbu kumbu sahihi Mwakyembe ndiye alizuka na hoja hii tena kwenye mkutano wa hadhara (BUNGE) na kuhusu kuwa mtaji wa wanasiasa ni team Lumumba ndiyo imejitoa akili na kuamua kushabikia chochote kinachofanywa na watawala hata kama ni cha kishenzi e.g. KUZIMA MIJADALA YA BUNGE LIVE
 
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malumbano ya kisiasa huku jina la Lowassa likitumika kama mtu fisadi na aliyehujumu sana uchumi wa nchi hii.
Kauli hizi zimetumika sana sio kwa wapiga debe na mavuvuzela tuu bali hata viongozi wa vyama na serikali.
Lakini wakati Lowassa akiomba kujiunga na Chadema alijieleza kuhusu kashfa zake anazopewa ikiwemo ya Richmond na mwisho alijitoa muhanga kwa kusema yuko radhi kwa yeyote au taasisi yeyote yenye ushahidi impeleke mahakamani. Huo ni ushujaa.
Sasa tuwaombe na wengine ambao kwa bahati mbaya wanalindwa na sheria yakinga kwa vile wanatajwa kwa makosa ya jinai wajitokeze nao watake kuwa kama kuna ushahidi kinga zao ziondolewe na washtakiwe ili kusafisha majina yao. Maana kama hakuna wa kukushtaki basi wewe ni safi na hayo maneno ni majungu na fitina tuu kama ilivyojidhihirisha kwa Lowassa kuwa ni maneno tuu ya kisiasa kwani DP,PCCB, Time ya maadili hata CAG hawajawahi kumgusa.
Tuwaombe JK, Ben, hata aliyepo wajitokeze kwa nia njema waombe kinga ziwekwe kando kama ilivyo nchi nyingi tuondoe haya maneno maneno
Hahahahahhaa......ukimuondolea Ben na JK kinga watafungwa maisha....
 
Ni chadema pale mwembeyanga......Mwakyembe alithibitisha tu.
Ripoti ya Kamati teule ya bunge chini Dk. wakichina (Mwakyembe) ndio iliyomchafua kwa maslahi ya watu wachache .. na leo kila kitu kipo wazi Lowassa hakuhusika na kashfa ya richmond.
 
Ripoti ya Kamati teule ya bunge chini Dk. wakichina (Mwakyembe) ndio iliyomchafua kwa maslahi ya watu wachache .. na leo kila kitu kipo wazi Lowassa hakuhusika na kashfa ya richmond.
Lete ushahidi ni kwa vipi hajahusika.
 
Kiuhalali Lowassa ndiye rais;
Hata hivyo JPM ameweza kuvaa viatu vyake;
 
Katika ripoti ya BUNGE na mwenyekiti wa kamati ya bunge akiwa Dr H. Mwakyembe
Bunge ni mhimili wa dola, na kuna wakati unawajibisha.....waliwajibishwa kina Lowassa, Kagasheki, Msabaha, Karamagi, nakadhalika.
 
Aisee, ukawa si wanasema kua kila ccm ni fisadi isipokua lowasa? ukizingatia kwamba lowasa alipokua ccm, mlimuiuta fisadi lakini kwa sasa sio fisadi maana yupo chadema?
Aliye muita Lowasa fisadi siyo CHADEMA, bali ni fisadi mwenzenu Dr. Mihogo a.k.a mchumba wa Josephine.
 
Ripoti ya Kamati teule ya bunge chini Dk. wakichina (Mwakyembe) ndio iliyomchafua kwa maslahi ya watu wachache .. na leo kila kitu kipo wazi Lowassa hakuhusika na kashfa ya richmond.
sema hivi kwamba mwakyembe na chadema walishiriki kumchafua lowassa kwa maslahi ya watu wachache......hili swala la kusema ripoti ya mwakyembe pekee ndio iliyomchafua napata shida na ufuatiliaji wako,wakati mnyika alisimama na kusema anao ushahidi tosha juu ya ufisadi wa lowassa,na huyu mnyika unataka kusema alikuwa anatetea maslahi ya watu gani??
 
Mkuu kuwaelewesha CDM-Lowassa kwataka moyo.....

Yy mwenyewe Lowassa akiulizwa kuhusu Richmond anajikanyaga kanyaga tu.
 
Back
Top Bottom