Who is Lowassa? Na nani wa kutumbua Jipu hili? JPM tusaidie..

DNR

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
523
337
Wakuu ni miaka mingi sasa jina la lowassa imekuwa kawaida kutamkwa kutoka kwenye vinywa vya watu iwe kwa wema au ubaya na mara nyingi kuandikwa kwenye magazeti kwa dhana hizo hizo wema au ubaya .

Tumeshuhudia kutoka kwa viongozi wakubwa wakimtuhumu kwa UFISADI lakini hakuna hata mmoja alie wahi toa ushahidi juu hizo kashfa, lakini pia tumesikia kauli za viongozi wakubwa wakidai lLowassa FISADI.

Kwa mimi nilifikiri ushahidi uliotolewa kwenye kashfa ya ESCROW ulikuwa mfano mzuri wa ushahidi kuliko huu wa RICHMOND wa maneno watupu na cha ajabu watuhumiwa wa ESCROW ni viongozi na wanatetewa na Wana JF kwa nguvu zote.

Maswali na ombi juu ya huyu:

1. Huyu mzee ni nani mpaka tufichwe fichwe ushahidi wa UFISADI wake?

2. Nani wa kutupa ushahidi ukiachana na ripoti ya Mwakyembe ambayo haitoshelezi?

3. Kama kuna ushahidi kwanini hapelekwi mahakamani?

4. Majibu ya mkato kuhusu RICHMOND anayotoa LOWASSA yanashaka yoyote au ni busara zake anaona atulie.

5. Tunamuomba Rais Magufuli atumbue majipu kama yapo yanayohusiana na huyu mzee ili tuachane na siasa maji taka.

Ni hayo tu.
 
Last edited by a moderator:
Lowassa sio fisadi, ni siasa chafu tu za JK na kundi lake la kina Mwakyembe na Sitta. Hutakuja kusikia Lowassa kashitakiwa kwa ufisadi hata siku moja, sio fisadi na ndio maana ushahidi hakuna. Mpumbavu peke yake ndiye anayeamini Lowassa ni fisadi.
 
Wakuu ni miaka mingi sasa jina la lowassa imekuwa kawaida kutamkwa kutoka kwenye vinywa vya watu iwe kwa wema au ubaya na mara nyingi kuandikwa kwenye magazeti kwa dhana hizo hizo wema au ubaya .

Tumeshuhudia kutoka kwa viongozi wakubwa wakimtuhumu kwa UFISADI lakini hakuna hata mmoja alie wahi toa ushahidi juu hizo kashafa . lakini pia tumesikia kauli za viongozi wakubwa wakidai lowassa FISADI .

Kwa mimi nlifikiri ushahidi uliotolewa kwenye kashfa ya ESCROW ulikuwa mfano mzuri wa ushahidi kuliko huu wa RICHMOND wa maneno watupu na cha ajabu watuhumiwa wa ESCROW ni viongozi na wanatetewa na Wana JF kwa nguvu zote .

Maswali na ombi juu ya huyu :

1. huyu mzee ni nani mpaka tufichwe fichwe ushahidi wa UFISADI wake ?

2. nani wa kutupa ushahidi ukiachana na ripoti ya mwakyembe ambayo haitoshelezi ?

3.kama kuna ushahidi kwanini hapelekwi mahakamani ?

4, majibu ya mkato kuhusu RICHMOND anayo toa LOWASSA yanashaka yoyote au ni busara zake anaona atulie

5. Tunamuomba Mh JPM atumbue majipu kama yapo yanayohusiana na huyu mzee ili tuachane na siasa maji taka .

ni hayo tu .

Lowassa alikwisha KATWA na JK? Huamini?
 
Bora DNR ulivoanzisha uzi kabisa. Huyu jamaa kiukweli kabisa lazima amehusika na ufisadi mwingi sana. Ana mali za ajabuajabu na ana marafiki (rejea anaposema mimi na rafiki zangu) wa siri asiotaka kuwaeka wazi kwa umma. Michango anayotoa ni mingi sana na hakuna biashara inayoonekana wazi kubwa akiifanya.

Huyu ni jipu. Sasa basi kwanini hatumbuliwi miaka nenda rudi?

Kwa sasa alipojiunga Chadema nkajua sasa kwisha. Watamtumbua kabla ya uchaguzi. Hola!

Nikajua utumbuaji wa sasa utamlenga yeye na 'rafiki zake'. Hadi sasa Hola! Labda mhandisi Natty km tetesi zinazosambaa ni kweli.

Ila ni mapema. Acha tuone utumbuaji unavyoendelea.

Tafsiri nyepesi ni kua ktk ufisadi wake, amehusisha wengi sana ndani ya CCMscrow kiasi akiguswa wanaenda wengi. Labda!

Au je, tuamini ni msafi?

Magu asipomtumbua, (JK aliishia 'kumtaja' pale Kirumba) forever mzee aachwe ni msafi hasa. Na haihitaji miaka 2 hadi atumbuliwe ikiwa maneno yanayosemwa ni kweli.

Ye ni nani hadi watafute njia ndefu kumtumbua?
 
Lowassa alikwisha KATWA na JK? Huamini?

Kukatwa ni siasa. Utumbuaji ni sheria. Mahakamani. Ushahidi.

Kwanini hazichukuliwi hatua? Ni maneno maneno tuu km wake wenza kutwa kucha CCMscrow wanamsakama?

Atumbuliwe soon ama MILELE wafumbe midomo kumuhusisha na ufisadi.

#tumbualowassasasa
 
Lowassa sio fisadi, ni siasa chafu tu za JK na kundi lake la kina Mwakyembe na Sitta. Hutakuja kusikia Lowassa kashitakiwa kwa ufisadi hata siku moja, sio fisadi na ndio maana ushahidi hakuna. Mpumbavu peke yake ndiye anayeamini Lowassa ni fisadi.

successor, Magu apewe say miaka miwili awe ashamtumbua. Akishindwa, MILELE CCMscrow waufyate kumhusisha Lowassa na ufisadi.

Muda mzuri ni sasa.
 
Mwenyewe keshaona dalili za kutumbuliwa ndo maana kaanza kulia lia eti wafuasi wake wananyanyaswa. Vijana wanasema ukitupa jiwe gizani ukasikia mtu kalia kwa maumivu jua limempata. Kauli ya lowasa inasadifu tuhuma alizotoa Dr Slaa kuwa biashara nyingi za lowasa hazijaandikwa majina yake. Anachomfanyia Magufuli ni kumkatia mirija.
 
successor, Magu apewe say miaka miwili awe ashamtumbua. Akishindwa, MILELE CCMscrow waufyate kumhusisha Lowassa na ufisadi.

Muda mzuri ni sasa.
Wewe nano kumpangia rais kazi? Sasa kwa taarifa yako lowasa hatashitakiwa ila chamoto atakiona. Majengo ya leopard tour ARUSHA yatataifishwa na kupewa shule iliyoporwa eneo lake, hoteli za kimagumashi zitadondoka halafu tutaanzisha kodi ya mifugo, hawezi kuwa na ng'ombe nchi nzima wanaharibu mazingira bila kulipiwa hata road license.
 
So kodi ya mifugo itaanzishwa kwa sababu lowassa ana ng'ombe nchi nzima? Maajabu hayawezi kuisha
 
Thubutu si lahisi mnavyodhani ila magufuri hizi richimond escownivizuri na vyo vikawekwa sawa
 
We NYUMBU kweli. Yani Magu ni mjinga kiasi hicho? Aanzishe kodi mpya kisa mtu mmoja? Kama kuna ushahidi, amsweke tu. Maana akianzisha kodi, ujue na bei ya nyama itapanda. Ataeumia wala si Lowassa.

Kwanini wanamwogopa Lowassa hadi kuzunguka hivyo?
Kodi ya mifugo ni mpya? We wa lini?
 
In the court is not what you know or your feeling my friend, is what you can proof thats all, ndo maana alishasema kama kuna mwenye ushahidi peleka mahakamani, na kama hauna ushahidi wa uhusika wake kwenye issue ya richmond just shut up you mouth.
 
Lowassa alijitumbua jipu mwenyewe pale Bungeni kwa aibu kubwa. Sasa unataka Magufuli akamue nini tena wakati kazi ilifanywa na jemedari Kikwete?

Magufuli ana deal na majipu yake ya sasa baada ya yeye kuwa rais....ulitaka aende kufukunyua makovu!?
 
mkuu DNR nakubaliananawe 100%...hili ndilo jipu nililozani Magu angeanzanalo!!!!cha ajabu naona wanamzunguka tu kwanini????mbona mahakama ya mafisadi bado kimya,kwanini hawajampeleka mahakamani??????CCM kwanini mnamwogopa lowasa kiasi hki...maneno ndo meeeeengiii mara ohhooo jamaaa ni fisadi kumbe chuki zenu tu binafsi...mmepata mamlaka yakumpeleka mahakamani ili arudishe mali za watanzania alizoiba...msipompeleka mahakamani nakumfunga basi msije mkarudi tena kutuambia huyo mzeeee ni fisadi....
 
Mwenyewe keshaona dalili za kutumbuliwa ndo maana kaanza kulia lia eti wafuasi wake wananyanyaswa. Vijana wanasema ukitupa jiwe gizani ukasikia mtu kalia kwa maumivu jua limempata. Kauli ya lowasa inasadifu tuhuma alizotoa Dr Slaa kuwa biashara nyingi za lowasa hazijaandikwa majina yake. Anachomfanyia Magufuli ni kumkatia mirija.
Sijawahi kuona kilaza kama huyo Lowassa. Jana aliongea kuhusu hilo...nikataka nisikie hayo manyanyaso ni yapi hasa...nikasikia anasema eti mambo ya kodi. Nikasema mtu kuambiwa ulipe kodi ndio manyanyaso! Basi na sisi wananchi watuondolee VAT kwenye bidhaa...maana kama hiyo ndio idea...basi na sisi wananchi tunanyanyaswa.

Lowassa anakera sana....yani ikiwezekana ni bora Israel alipitie tu...maana alichoki kuongea pumba! Jitu la aina gani kila siku pumba tu!
 
Kwa mtu wa kawaida hawezi kuujua ufisadi wake. Taratibu tu utajulikana through majipu yanayoendelea kutumbuliwa. Ngoja wahamie ile sekta yake. DNA zitumike kujua utajiri wake kama ni wa halali au ni wizi.
 
Back
Top Bottom