Ripoti zote za CAG, siuoni ufisadi wa Lowassa

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,053
114,519
Mpaka sasa sijafanikiwa....bado naendelea. Nachotaka ni kumpata Lowasa ili nimlipue atumbuliwe na Magufuli. Nalazimika kutumia ripoti hii maana Richmond inayosemwa hawamchukulii hatua yeyote nguli huyu, ni maneno maneno ya kanga tu toka Lumumba na vibaraka wao. Ina maana huyu "fisadi" kaweka mamlaka zote mfukoni? Mpaka Ikulu? Majipu yanatumbuliwa, mengine yanatajwa lakini yanashindikana, lakini Lowasa jiiiii
 
Lowasa ameifisadi sana hii nchi Richmond kwa siku analipwa tsh milioni 152 na TANESCO pesa zake ameinunua CHADEMA hatimiliki ya CHADEMA ipo nyumbani kwake Monduli
 
Tunawangoja viongozi wetu wa CHADEMA watuambie kuwa ule uzushi wa kusema Lowasa fisadi waliutoa wapi......

Na ule ushahidi waliosema kuwa wanao juu ya ufisadi wa Lowasa umeyeyukia wapi.....??

Au waitishe mkutano wa waandishi wa habari wakiri kuwa walimsingizia mzee wa watu....na wamuombe msamaha kwa kumchafulia jina lake.......
 
siku lowasa akitumbuliwa na kupelekwa gerezani ufisadi ndio utafikia tamati..Watanzania tunasubiri kwa hamu sana kumuona lowasa magereza kwa kuhujumu uchumi
 
Lowasa anawakeshesha watu mitandaoni kama popo du poleni sana vijana wa Lumumba kwa kuhangaika bila mafanikio
 
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malumbano ya kisiasa huku jina la Lowassa likitumika kama mtu fisadi na aliyehujumu sana uchumi wa nchi hii.
Kauli hizi zimetumika sana sio kwa wapiga debe na mavuvuzela tuu bali hata viongozi wa vyama na serikali. Lakini wakati Lowassa akiomba kujiunga na CHADEMA alijieleza kuhusu kashfa zake anazopewa ikiwemo ya Richmond na mwisho alijitoa muhanga kwa kusema yuko radhi kwa yeyote au taasisi yeyote yenye ushahidi impeleke mahakamani. Huo ni ushujaa.

Sasa tuwaombe na wengine ambao kwa bahati mbaya wanalindwa na sheria yakinga kwa vile wanatajwa kwa makosa ya jinai wajitokeze nao watake kuwa kama kuna ushahidi kinga zao ziondolewe na washtakiwe ili kusafisha majina yao. Maana kama hakuna wa kukushtaki basi wewe ni safi na hayo maneno ni majungu na fitina tuu kama ilivyojidhihirisha kwa Lowassa kuwa ni maneno tuu ya kisiasa kwani DP, PCCB, Time ya maadili hata CAG hawajawahi kumgusa.
Tuwaombe JK, Ben, hata aliyepo wajitokeze kwa nia njema waombe kinga ziwekwe kando kama ilivyo nchi nyingi tuondoe haya maneno maneno
 
Tunawangoja viongozi wetu wa CHADEMA watuambie kuwa ule uzushi wa kusema Lowasa fisadi waliutoa wapi......

Na ule ushahidi waliosema kuwa wanao juu ya ufisadi wa Lowasa umeyeyukia wapi.....??

Au waitishe mkutano wa waandishi wa habari wakiri kuwa walimsingizia mzee wa watu....na wamuombe msamaha kwa kumchafulia jina lake.......
Mwakyembe ndiye aliyetengeneza uongo wa kumchafua..
 
Aisee na hii nayo ni hoja? we have a very ,long way to go, ni sawa na kutaka kuuliza ufisadi wa mwinyi au mkapa kwenye ripoti za mwaka jana awamu ya 4,
Mungu hamfichi mnafiki, ziwekwe ripoti za ufisadi wa Lowasa hadharani sio kuja na mipasho hapa, mpaka sasa anaestahili kuwa fisadi mkuu ni rais mstaafu wa awamu ya 4 maana haya yote yamefanyika kwa baraka zake, Lowasa nyota yake ndio tatizo inang'aa mpaka watu wanajiogopa.
 
Back
Top Bottom