David Kafulila apangua hoja zote za Zitto Kabwe kuhusu ripoti ya CAG

KADA08

Member
Dec 2, 2017
44
152
1. Baada ya Chama Cha ACT kutoa tamko lao kwa kina Jana kuhusu Ripoti ya CAG kwa hesabu za 2016/17, nimeulizwa na wadau wengi kuhusu maoni yangu kufuatia tamko hilo wakihusianisha na msimamo wangu kwamba serikali ya awamu ya tano ni tofauti sana na hivyo kutaka kunisikia maoni yangu kufuatia kilichoitwa madudu yaliyobainishwa katika uchambuzi wa chama cha ACT kuhusu serikali hii kwa mujibu wa ripoti hiyo.

2. Kwanza niwapongeze ACT kwa kuunguza bongo hata kutoka na tamko lililosababisha mjadala wa masuala muhimu kwa Taifa. Binafsi naamini kwamba Ripoti za CAG ni kioo kwa Serikali na Mamlaka zake,nakwasasa ni kioo kwa vyama vya siasa pia, ndio sababu serikali huzipa uzito wa kipekee kwa kuchukua hatua haraka na hivyo kutoa somo kwa vyama vya siasa kufanya hivyo pia.Hivyo nawapongeza ACT kuipa joto hoja ya CAG ili tujadili na kubadilishana mawazo kwa maslahi ya Taifa.

3. Katika hoja ya 7, ACT wanasema " Kwa ujumla Serikali imepata hati Chafu.Taarifa ya CAG ya ukaguzi wa kwanza wa makusanyo na matumizi ya kibajeti ya Serikali ya awamu ya tano, imeonesha kuwa , kwa ujumla , Serikali ya Jamhuri ya Muungano imepata hati Chafu , kwakuwa Hesabu Jumuifu za Taifa ( Consolidated Accounts ) zimepata Hati ISIYORIDHISHA ( Chafu)."

UKWELI nikwamba Nimesoma Ripoti hiyo yenye kurasa 434, sikukuta mahala CAG ameandika kwa kigezo chochote kwamba Serikali kwa ujumla imepata hati Chafu.Nikajaribu kusoma mijadala kutafuta nani ameweza kutoa Rejea ya ni wapi CAG kasema hilo, nikakuta kwenye mjadala wa Jamiiforum, Kiongozi Mkuu wa ACT amemjibu mmoja wa waliotaka kujua ni wapi CAG kasema kwa ujumla Serikali imepata hati Chafu, katibu majibu yake, Kiongozi huyo katika majibu yake kwenye mjadala huo muda(8:09PM) ameandika kwamba CAG amesema hilo kwenye ukurasa wa 298. NIMERUDIA KUSOMA UKURASA HUO NENO KWA NENO HAKUNA KITU HICHO. Ukurasa huo umeleza mapungufu ya hesabu, lakini hakuna maneno ambayo ACT inataka kuaminisha Umma kuwa yametajwa na CAG.

Inawezekana ACT baada ya kusoma maelezo hayo wakahitimisha kwamba Serikali kwa ujumla imepata hati Chafu.Hata hivyo, Mwenye Mamlaka ya kuamua madaraja ya Hati si Mwingine bali CAG kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya Ukaguzi wa Taasisi za Umma( ISSAIs) na Bodi ya Kimataifa ya Maadili kwa kanuni za Maadili ya wahasibu ( Kanuni ya IESBA). Hivyo sio mtu yeyote au chama au taasisi inamamlaka ya kusoma hesabu na kuzipangia daraja la Hati kama ACT wanavyotaka kufanya. Ni kwa msingi huo maneno kwamba Serikali imepata hati Chafu yanabaki kuwa kwa mujibu wa chama cha ACT na sio CAG .

2. Kwenye hoja 1, ACT wanasema Mawaziri wanafanya makosa kujibu hoja za CAG kwa waandishi wa habari na kwamba sheria ya Ukaguzi wa Umma kifungu38(1)&(2) kinaeleza Maafisa Masuuli/ Makatibu Wakuu ndio wanapaswa kujibu hoja zilizoibuliwa na CAG tena mbele ya Kamati ya PAC&LAAC.

UKWELI Nikwamba Mawaziri wangejibu hoja za CAG mbele ya Kamati za PAC& LAAC wangekuwa wamevunja Sheria hiyo, lakini Mawaziri kueleza Waandishi wa Habari maoni yao au hatua wamezokwisha kuchukua kuhusu Ripoti ya CAG haijakatazwa popote kwenye sheria hiyo kwani wanahabari sio kamati ya PAC wala LAAC kama ilivyotajwa katika sheria hiyo.Ndio sababu tamko hilo hilo la ACT, pamoja na kujua kwamba Ripoti hiyo haijaanza kufanyiwa kazi na Kamati za PAC& LAAC , ACT wamepongeza Serikali kuanza kuchukua hatua hadharani kufuatia Ripoti hiyo. Hivyo walichokipongeza ndicho wanachokihoji tena kwenye tamko hilo hilo.

3.Kuhusu kinachoitwa upotevu wa 1.5trilioni. Kwa mujibu wa ACT nikwamba kwakuwa kwenye ukaguzi wa matumizi imeonekana kiasi kilichotolewa ni trilioni 23.8..wakati kwenye makusanyo kilichopatikana ni trilioni 25.3 .hivyo kuna upotevu wa 1.5trilioni.

UKWELI ni kwamba kwamba ACT ilipaswa kuweka hoja hii katika mfumo wa swali badala ya kuhitimisha kwani hata CAG hakuna mahala amehitimisha kuwa kuna upotevu wa trilioni1.5. Nasema walipaswa kuuliza kwasababu Mimi baada ya kusoma Hotuba ya Bajeti 2017/18, kwenye eneo la Mapitio ya Bajeti ya 2016/17 ambayo ndio hesabu zake zimekaguliwa, Waziri wa Fedha kwenye Hotuba yake alibainisha wazi kwenye Paragrafu ya 2 kipengele cha mapitio ya matumizi kwamba Kati ya Pesa za miradi ya maendeleo kutoka nje( trilioni trilioni 3.047).Kuna kiasi cha Pesa hizo Matumizi yake hayakupitia mfumo wa malipo wa Serikali baada ya baadhi ya washirika wa maendeleo kuzipeleka moja kwa moja kwenye miradi.Nanukuuu " Hata hivyo ,baadhi ya fedha za nje za kugharimia miradi ya Maendeleo hazikujumuishwa kwenye matumizi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kuchelewa kupata thamani halisi ya vifaa vilivyopelekwa moja kwa moja kwenye miradi kutokana na baadhi ya washirika wa Maendeleo kuendelea kupeleka fedha moja kwa moja bila kupitia mfumo wa malipo wa Serikali" Katika msingi huo ni wazi fedha ambazo hazikutolewa kupitia mfumo wa malipo wa Serikali CAG asingeweza kuziona na hivyo kujitokeza kwa tofauti ya makusanyo na fedha iliyolipwa sio jambo la kushangaza katika mazingira hayo.Najua Serikali inaweza kueleza hili kwa takwimu zaidi.

4. Hoja kwamba Serikali imetekeleza Bajeti kwa asilimia 68% huku Bajeti ya Serikali za mitaa ikitekelezwa kwa asilimia 51ni utekelezaji hafifu nadhani ingekuwa vema kama ACT wangefanya ulinganisho.waseme kiasi hicho ni kidogo kulinganisha na miaka gani. Kwani navyojua miaka michache iliyopita Bajeti ya Serikali za mitaa ilitekelezwa mpaka kwa asilimia35%. Hivyo utekelezaji huu wa asilimia 51 % ni hatua kubwa hata kama haitoshi kwakuwa haijafika asilimia100%

5. Kwamba ACT wanasema Madeni ya nyuma yaliyolipwa bila idhini ya bunge ni madeni hewa, Nadhani ACT wangetafuta msamiati tofauti kwani madeni hewa ni Yale yasiyokuwepo, lakini kama yamehakikiwa kuwa ni madeni halali hayawezi kuitwa madeni hewa.

6. Kwamba CAG hakukagua ATCL hivyo nikasoro kwa CAG, nadhani ibaki kama walivyoshauri kwamba ukaguzi ujao CAG aone haja ya kukagua lakini huwezi kumlaumu kutokagua kwa hoja tu manunuzi ya ndege yalifanyika katika mwaka huo wa fedha uliokaguliwa 2016/17 kwani hakuna mwaka CAG alikagua mashirika yote. laiti ingekuwa yamekaguliwa mashirika yote likaachwa ATCL kulikuwa na uhalali wa kuhoji kulikoni.

7. Hoja kwamba Matumizi ya Serikali yanapangwa na Ikulu siku hizi badala ya Serikali ni tuhuma nzito, ingawa kwakuwa wameitoa bila uthibitisho wowote ni ngumu kwa mtu makini kuipa uzito sawia na hivyo inakosa uzito na kuonekana kama vijembe vya kisiasa tu

8. Hoja kwamba namna serikali inavyokopa ndani kupitia minada ya dhamana za Serikali inasababisha Benki za biashara kuvutiwa zaidi kuikopesha serikali badala ya sekta binafsi na hivyo kufanya biashara isichangamke ni hoja inayohitaji mjadala mpana.Nasema hivyo kwasababu kwenye awamu ya nne tulilalamika kwamba Serikali ilikuwa inakopa ndani kwa mfumo huo lakini kwa riba juu sana mpaka zaidi ya asilimia17% mwaka 2015 kwa TBs za Sik182&365 na hivyo hoja ikawa ni kwamba Benki zinapoteza hamu ya kukopesha sekta binafsi na hata kuongeza riba zaidi kwa kulinganisha na riba ambayo Benki huvuna inapoikopesha serikali( kwasababu Benki zinajua Serikali ni Risk free). Ni kwasababu hiyo tukawa tunajenga hoja bungeni serikali isikope kwa riba ya juu katika masoko ya dhamana ili Benki za biashara ziwe na hamu ya kukopesha sekta binafsi na kwa riba nafuu. Kitu ambacho Serikali hii imetekeleza, kwamba kwasasa Serikali inakopa kwenye mfumo huo wa TBs kwa riba ya asilimia 5% kwa TBs za siku365 na riba ya kwa TBs za siku182.Hii inathibitisha wazi dhamira ya serikali kutozivutia Benki za biashara ziikopeshe n badala yake zijielekeze kwenye sekta binafsi kwani riba zinayopata sasa kwa kuikopesha Serikali ni pungufu kwa zaidi ya asilimia 300% kulinganisha na mwaka 2015.

9. Mwisho nihitimishe kwa kuipongeza Serikali kwa namna imevyofanikiwa kutekeleza kilichokuwa kilio cha Bunge la 9&10 kuhusu misamaha ya kodi ambapo kwa miaka10 mabunge hayo yalipigania misamaha ishuke mpaka asilimia1% ya pato la Taifa ikitolewa mifano ya nchi wanachama Afrika Mashariki kama kigezo( misamaha yake ilikuwa asilimia1% ya Pato la Taifa). Miaka miwili yote ya Serikali hii, misamaha ya kodi ni asilimia1% kutoka asilimia2 % mpaka asilimia3% ya pato la Taifa kabla ya awamu hii( Kwa mujibu wa Ripoti hii ya CAG).Aidha ufanisi wa TRA katika kukusanya kodi tangu mwaka 2016 upo juu kuliko miaka mingi kama inavyojieleza kwenye Ripoti ya CAG ukurasa wa 31&32. Ambapo imebainishwa kwamfano, mwaka 2013/14 makadirio ya makusanyo ya kodi yalikuwa billion10,320 lakini ikakusanywa bilioni 9289 , sawa na pungufu ya bilioni 1031, Mwaka 2014/15 Makisio ilikuwa kukusanya billion11262 lakini ikakusanywa billion9919 sawa na pungufu ya billioni1343. Lakini Mwaka wa Kwanza wa awamu ya tano, hesabu za 2015/16 , Makadirio yalikuwa billioni12363 lakini makusanyo yakafika billion12464 sawa na ziada ya billion101 na hata mwaka 2016/17 ambapo makisio yalikuwa juu kuliko mwenendo wa awali kwa kuwekwa billioni 15105 lakini bado makusanyo yalifika billioni14271 sawa na pungufu ya billioni834,pungufu ambayo bado ni kidogo kulinganisha na miaka iliyotangulia.( Rejea Ripoti ya CAG ukurasa31&32).

Niwashukuru watanzania wote mliohitaji kusikia maoni yangu.

Soma: Serikali imepoteza TZS 1.5 trilioni mwaka 2016/17. Imetumia Mabilioni kinyume na Utaratibu, Imelipa Madeni Hewa...

=====

Baadhi ya maoni ya Wachangiaji...

Queen V, said:

Kafulila amesoma kweli page 400+ au anatutania?

Utaratibu haupo hivyo. Sababu hata bungeni hii imepingwa ndio maana Mawaziri wamesitisha kutoa majibu. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka amekosoa utaratibu unaoendelea wa mawaziri walioguswa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2016 kuwa si sahihi kujibu hoja zake nje ya Bunge.

Akizungumza baada ya semina iliyotolewa na Taasisi ya Uwajibikaji ya Wajibu kwa kamati tatu za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na ile ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Kaboyoka alisema utaratibu huo wa Serikali kujibu ripoti ya CAG si sahihi na watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho kuelezea kwa nini hawakubaliani nao.

“Nafikiri hili tulizungumzie Jumatatu, tutalitolea maelezo maana sio sahihi kabisa. Maana nani ame-verify (amethibitisha) ndio useme hivyo. Ile ripoti ni ya kibunge na ina taratibu zake za kupokewa na kufanyiwa kazi, kwa hiyo haiwezi kujibiwa tu hivihivi,” alisema.

Hii hoja yako nmekuwekea Picha ili usome kwa makini zaidi, na hizi ni sababu zilizosababisha kupata hati chafu.

whatsapp-image-2018-04-16-at-14-53-46-jpeg.746427

4. Hesabu Jumuifu za taifa

a) Taasisi 13 zilizojumuishwa na zenye uwekezaji wa mitaji kibiashara wenye thamani ya shilingi 549,199,224,690; ulibainisha kuwa, uwekezaji huo ulithaminishwa kwa bei za awali kinyume na matakwa ya aya ya 48 ya IPSAS 29 ambayo inahitaji mali za kibiashara (financial assets) baada ya kutambua thamani ya uwekezaji kwa mara ya kwanza; kuthaminishwa kwa bei ya soko la wakati husika bila kuondoa gharama za miamala inayoweza kuhusika wakati wakuuza mali hiyo. Kwa hiyo, msingi wa thamani wa uwekezaji uliotaarifiwa haukuweza kuthibitishwa.

b) Maelezo ya ziada (Note) 77 yanayohusiana na uwekezaji katika Mashirika (associate) na Mipango ya pamoja (joint ventures) imebainishwa uwekezaji hasi katika Mashirika na Mipango ya pamoja (Joint Ventures) wa shilingi 405,349,237,000 kwa mwaka 2016/2017 na shilingi 362,241,134,000 kwa mwaka 2015/2016. Hii ni kinyume na Aya ya 41 &42 ya IPSAS 36 inayohitaji mwekezaji kuacha kutambua sehemu yake ya upungufu/hasi alikowekeza mara tu uwekezaji huo unapokuwwa umepungua hadi kufikia sifuri. Baada ya hapo, kunahitajika kutaja/kuonesha (Disclose) upungufu wa thamani (impairment) wa mali husika. Sababu zaidi soma kwenye kiambatanisho hapa chini kuanzia ukurasa wa 296.

Fedha kutokupita kwenye mfumo wa Malipo ya Serikali nso mwanya Ulitumika kupiga hiyo Trilioni 1.5. Je ulitaka nani alaumiwe kwenye hili? Tutaaminije kama kweli zilienda kwenye Miradi ya Serikali? leta ushahidi kama hazijapigwa. Kafulila anachokifanya ni kututoa kwenye reli ya kuiwajibisha Serikali. CAG kaivua nguo Serikali na kila mtu kaona. Kinachotakiwa Serikali ijitafakari na kurudisha hela iliyopotea au kuitolea ufafanuzi.

whatsapp-image-2018-04-16-at-14-53-47-1-jpeg.746428

Naomba urudie kuisoma ripoti kuu ya Serikali ya CAG hapa=>Ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka ulioishia 30 juni, 2017, imejaa madudu

=========

barafu said;

Sisi watu weusi na wa hovyo sana!!Huu mjadala nimeukuta kule "mybroadband"(Jf ya south Africa).Hawa viongozi wa Afrika ni wanafiki sana,baada ya hotuba ile ya Malema pale Orlando Stadium,na documentrary ya jana iliyotolewa hadharani kwa mara ya kwanza na e-tv ikimuonyesha Mama Winnie anavyoeleza "option" alizopewa Mandela ili atoke gerezani,huwezi tena kuwaamini wanasiasa wa Afrika

Ndio maana juzi niliwaambia watoto wangu,kama mimi nikiwa hai au hata nimekufa,ningependa sana wao kama wanangu,wasijiingize ktk siasa.Na jambo hili nalisema nikiwa hai,na walikumbuke nikiwa kaburini.

Maana ktk kua yangu,hakuna tabaka la wanafiki nililokutana nalo kama tabaka la "Wanasiasa".Hakuna tabaka lisiloeleweka kama hili...Iwe upinzani au tawala,wanawaza matumbo yao tu.

Huyu Kafulila,sijui ni tatizo la lugha ya "Kimahesabu"?Unaposema deni "hewa",maana yake ni deni ambalo halijathibitishwa na bunge,wala hakuna mahali ambapo bunge limeazimia pesa itoke ili ikalililpe hilo deni,hata kama deni hilo lipo,mpangaji wa kulilipa na kuidhinisha kulipa ni bunge kwa mujibu wa sheria,sasa kama serikali imeamua kulipa tu bila kupitishwa na bunge,hilo ni deni "hewa"...Au tuite "Ghost Debt".

Yaani kwa mfano,baba akupe shilingi 50 ukalipe deni kwa Mzee Sakawe,lakini njiani ukakutana na Mzee Ambwene,ukampe hiyo hela na hata kama kweli alikuwa anamdai baba yako,hilo ni "deni hewa",sababu baba yako alikupa umpe Mzee Sakawe na wewe umempa Mzee Ambwene.Katika mambo ya utawala bora,huo ni utovu wa nidhamu kwa bunge kama ilivyo utovu wa nidhamu kwa baba yako maana umelipa deni kwa mtu ambaye hukutumwa.Eboo Kafulila,umepatwa na nini?

Anasema kuvunja sheria ni kama Mawaziri wangeenda kuwajibu PAC na LAAC,eti sababu Waandishi sio LAAC wala PAC basi hakuna shida.Eboo!!Sheria inawataka CAG akishasoma hayo mapungufu,basi serikali iyafanyie kazi na si kuyajibu wala kuyatolea ufafanuzi,maana kama wataendelea kutolea ufafanuzi jambo ambalo CAG kalitazama kitaalamu,itakuwa ni kutaka kuficha mapungufu ambayo ni kinyume na utawala bora,CAG yupo kisheria,yale anayosema ni MAPUNGUFU hayaitaji ufafanuzi zaidi ya kuyafanyia kazi.Na sheria iliweka PAC na LAAC,maana haikujua huko mbele atakuja mtu anayejiona "Malaika" hakosei,kwa hiyo kama anaona hapati nafasi kujibu bungeni(kisheria) anaamua kununua muda kwenye vyombo vya habari ili kujisafisha.Kitendo walichofanya mawaziri ni sawa na kusema CAG na report yake wamesema UWONGO hivyo tusiiamini ofisi yake.Hili nalo Kafulila halioni kisa kahamia CCM??

Halafu anasema eti hiyo 1.5 trilion hakuna mahali ilipoandikwa.Lakini anakubali kuwa kulikuwa na 25.3 dhidi ya 23.3,na serikali haijasema hiyo 1.5 imeenda wapi na imeitumia kufanya nini...Kweli kwenye dhana ya utawala bora na uwajibikaji unashindwa kuuliza??Yaani wewe muuza duka wako mahesabu yanaonyesha amekusanya shilingi 10,halafu matumizi ya kuongeza mzigo wa dukani ametumia shilingi 9...ukimuuliza hiyo shilingi moja iko wapi basi unakosea?Utawala bora ambao CAG ni nguzo,unatutaka kuiuliza hiyo shilingi 1,maana inaweza kuwa ndio imeenda kulipa deni la bombadia bila kupitishwa na bunge.Hata hili Kafulila unapinga??Loooh...Umepatwa nini mwanangu???

Kuhoji ATCL ni LAZIMA kwa sasa,sababu ndio moja ya mashirika ambayo yanatumia pesa nyingi za walipa kodi kwa sasa,kununua ndege "cash" sio jambo dogo,tena mpaka ndege aina ya B787-800series,CS300 na bombadia mpyaa!!Bado hutaki liwe kipaumbele katika kukaguliwaa.Hili ni shirika ambalo hata AITA imeliondoa kwenye uanachama sbb ya madeni yake,hili ndio shirika ambalo JPM kwa kujua,ameamua ndege alizonunua azisajili kama ni mali ya TGFA(Tanzania Gvt Flight Agency) na si ATCL,sababu wanajua zikiwa zao tu,wanapokwa kwa madeni,sasa tujiulize bila CAG kuchunguza humu ATCL,huu uwekezaji wa kununua ndege in cash,tutakuwa na TIJA huko mbeleni?Na hapa mwanangu KAFULILA huoni hoja ya ZITTO kweli?

Ni kweli IKULU kwa sasa ndio mpangaji wa matumizi ya serikali ya kila siku,Ikulu imepoka madaraka yote ya kifedha.Kibubu cha nchi sasa kinamilikiwa na mtu mmoja.Ndio maana kwa sasa,mashirika na kampuni zilizo chini ya serikali "Account" zake zipo BOT,kila wanachokusanya wanapeleka BOT,kule Mzee ndio anaminya batton ya wapi achukue na wapi atumie.Si ajabu anasimama anasema IGP ntakupa bilioni 10 ujenge nyumba,anasimama anasema Uhamiaji ntakupa bilioni 10 ujenge HQ Dodoma,sasa hizo 10 billion,ni bunge gani limepitisha?Hata hili hujui kuwa kwa sasa Rais ndio Hazina?Mwanangu Kafulila...

TRA inakusanya pesa kama "Wakala",yaani sio sehemu ya makusanyo kama kodi,ni pesa ambazo hapo mwanzoni huwezi kuziona kama "kodi" sbabu mashirika kama TBS,TPA,TCRA,TCAA,TFDA,TAA nk yalikuwa yanakusanya yenyewe kwa mujibu wa sheria ya Gvt Agency ya mwaka 1999(?),sasa TRA inaturundikia kana kwamba ni makusanyo ya kodi na kuimba kuwa kodi ukusanyaji umepanda!!!Hili nalo hulioniiiiii!!!Siasa na njaaa ni balaa...A man with an empty stomach can not be a good political adviser.

Cc chige Mag3 Salary Slip Quinine
 
Mkuu barafu hapo ungeendelea kidogo kufafanua hata sisi tuliofunikwa kwenye blanket tungeelewa sana mkuu. Nikupe hongera kwa hilo
 
Kafulila umejitahidi, tunataka uchambuzi ambao hauko political sana , utekelezaji wa budget by 51% ni hatua nzuri ukilinganisha na 35% , hatua nzuri ingawaje hatua zaidi zinatakiwa zichukuliwe angalau tufikie 70%, na kufikia 70% maana yake serikali lazima ianzishe miradi/vyanzo vipya vya mapato ,tutoke katika ukusanyaji wa tril 1.2, 1.3, to 1.5+ kwa mwezi, serikali ipate pesa nyingi kusimamia miradi ya maendeleo.
 
Back
Top Bottom