Ripoti zote za CAG, siuoni ufisadi wa Lowassa

Ripoti zote za CAG, siuoni ufisadi wa Lowassa

Ile ilikuwa siasa ya majukwaani sasa tuko kwenye sheria. Makosa ya jinai hayakuulizi itikadi yako ni nini na zamani ulikuwa unaamini au kusema nini, bali kama mwizi ni mwizi tuu kulingana na ushahidi.
Mtu hata mkimzomea mtaani kuwa ni kibaka sio sababu ya kumpeleka mahakamani bila ushahidi, lakini mtu mwaweza kumuita sheikh au Padre lakini kama kuna ushahidi anapelekwa mahakamani. Kama tuko serious na utumbuaji majipu tuchukue hatua za kisheria sio hizo blabla za eti sijui nani alisema vile au nani kasema nini bali ushahidi tuu na mahakama ichukue mkondo. Lowassa kesha toa ruksa kushtakiwa kama kuna ushahidi ili akajitetee mahakamani kwa nini wanamuogopa miaka tisa toka aachie ofisi? Ndio maana tunasema aje Ben nae aseme ondoa kinga yangu na kama Kiwira nimevunja sheria nishtakiwe nikajitetee mahakamani au JK na yake aseme hivyo hivyo kisha tuone!
Tumechoka mtu kuitwa mwizi lakini hatumchukulii hatua. Binafsi Lowassa akiwa na kesi mahakamani sitamuunga mkono mpaka kesi itakapoamuliwa kwa haki na kujua yuko upande gani.
Kweli pesa tamu.. duh!
 
Ukiibuliwa ufisadi wa EL naamini theluthi mbili ya CCM itakuwa kwenye kashfa hiyo.
 
Mpaka sasa sijafanikiwa....bado naendelea. Nachotaka ni kumpata Lowasa ili nimlipue atumbuliwe na Magufuli. Nalazimika kutumia ripoti hii maana Richmond inayosemwa hawamchukulii hatua yeyote nguli huyu, ni maneno maneno ya kanga tu toka Lumumba na vibaraka wao. Ina maana huyu "fisadi" kaweka mamlaka zote mfukoni? Mpaka Ikulu? Majipu yanatumbuliwa, mengine yanatajwa lakini yanashindikana, lakini Lowasa jiiiii
Ata ufisadi wa dr. DAU na Zitto siuoni
 
MTU anayejua jambo kwa kukariri ni tatizo, kwanza nivigumu sana kumwelewesha tofauti na alivyoambiwa mpaka arudi kumwelewesha aliye mwambia ambaye wakati huo huenda amebadilisha msimamo kutokana na kuelewa. Inawezekana hawa wenzetu wajua mambo kwa kuelewa sio kukaririshwa ndio maana wanabadirika wanapoeleweshwa kwa hoja.
 
Hivi Lowassa anamiliki halmashauri au taasisi ya serikali?

Kama Kuna wizi ulifanywa na kampuni yake au ile ambayo yeye ni mmoja wa wanahisa atafikiwa tu, lakini Kama hakuna itadhihirika pia.
 
Tunawangoja viongozi wetu wa CHADEMA watuambie kuwa ule uzushi wa kusema Lowasa fisadi waliutoa wapi......

Na ule ushahidi waliosema kuwa wanao juu ya ufisadi wa Lowasa umeyeyukia wapi.....??

Au waitishe mkutano wa waandishi wa habari wakiri kuwa walimsingizia mzee wa watu....na wamuombe msamaha kwa kumchafulia jina lake.......
Hivi Samwel Sitta,Harrison Mwakyembe,Kikwete,Bernard Membe,Joseph Butiku na yale madomokaya Nape Nauye,Humphrey Polepole na liMakonda ni viongozi wa CHADEMA???
 
Tatizo letu waafrika hatujui kua adui yetu ni sisi wenyewe. Tunadanganyika na maneno ya wanasiasa ambao lengo Lao ni kujifaidisha kwa mgongo wa kujifanya wanatumikia wananchi na sie bila kufikiri mara mbili tunawaamini. Mimi nilikua shabiki mkubwa wa boys 2 men(jk na lowasa) lakini toka lowasa ajiuzuru uwaziri mkuu nilianza kua na wasiwasi juu ya ushabiki wangu kwa watu hawa wawili katika kuiendeleza Tanzania. Mwanzoni nilifikiri lowasa kaonewa lakini kadri siku zilivyoyoma nikatambua kua hakuna jambo gumu kwa mtanzania kama kulielewa sakata la Richmond kuanzia mwanzo mpaka mwisho wake labda huyo mtu awe muhusika au kasimuliwa na muhusika. Baada ya lowasa kuhamia chadema nikadhani kwamba sasa wakati wa ukweli wa Richmond kujulikana umefika kumbe nilikua nimejidanganya kwa sababu alitoa sababu ambazo mpaka leo haziniingii akilini hata kidogo kwani alitoa jibu jepesi sana eti ye aliagizwa tu, na watu wakampigia makofi eti mwenye ushahidi aende mahakamani. Nani mwenye ushahidi zaidi ya wahusika wa hiyo saga?, nani atashtaki kwa kesi ambayo yeye mwenyewe ni mhanga?. Nadhani wakati wa kuacha kushabikia siasa za vyama umefika la sivyo maendeleo tutayaona na kusikia kwa wenzetu tu na sisi tukifa na chadema na ccm zetu
 
Ile ilikuwa siasa ya majukwaani sasa tuko kwenye sheria. Makosa ya jinai hayakuulizi itikadi yako ni nini na zamani ulikuwa unaamini au kusema nini, bali kama mwizi ni mwizi tuu kulingana na ushahidi.
Mtu hata mkimzomea mtaani kuwa ni kibaka sio sababu ya kumpeleka mahakamani bila ushahidi, lakini mtu mwaweza kumuita sheikh au Padre lakini kama kuna ushahidi anapelekwa mahakamani. Kama tuko serious na utumbuaji majipu tuchukue hatua za kisheria sio hizo blabla za eti sijui nani alisema vile au nani kasema nini bali ushahidi tuu na mahakama ichukue mkondo. Lowassa kesha toa ruksa kushtakiwa kama kuna ushahidi ili akajitetee mahakamani kwa nini wanamuogopa miaka tisa toka aachie ofisi? Ndio maana tunasema aje Ben nae aseme ondoa kinga yangu na kama Kiwira nimevunja sheria nishtakiwe nikajitetee mahakamani au JK na yake aseme hivyo hivyo kisha tuone!
Tumechoka mtu kuitwa mwizi lakini hatumchukulii hatua. Binafsi Lowassa akiwa na kesi mahakamani sitamuunga mkono mpaka kesi itakapoamuliwa kwa haki na kujua yuko upande gani.

Screenshot-1.png
 
Kwani Lowasa ni shirika la umma au Halmashauri za Wilaya
 
Achana na siasa mkuu, zina wenyewe hizi, tumuunge mkono Magu twende tukalime, km ni viyoyozi hata shamba tutavifunga
Nalima ndizi na kufuga mbuzi mkuu, hua nakuja mjini mara moja moja kuleta mazao yangu, hata huku shamba pia JF inapatikana
 
Ushahidi wa akina mnyika una elements za kisiasa zaidi. Dhidi ya serikali nzima ya CcM na mfumo wake. Kumbuka kile ni chama cha siasa(stuka).
Tundu lisu alisema fisadi wa richmond ni JK. Jk hakujibu neno hata tone(stuka).
Na jk siku anamaliza kampeni kule mwanza angali akijua ni siku ya mwisho na hakutakua na kampeni nyingine za kufanya wapinzani wajibu hoja akasema EL anahusika na richmond (stuka).

So DETAILS ZOTE WATAKUA NAZO HAO CCM ESPECIALLY MwaKYEMBE, PLUS DR. SLAA. Walioongea bungeni akamtuhumu el waziwazi.mpaka akajiuzulu.
Kisha akarudi tena bungeni kumsafisha el. aliposema kua EL hana kosa bali ameangushwa na makatibu wake. Akaufunga mjadala.

Tena akarudi wakati wa kampeni akasema anazo documents zote. Akishirikiana na dk.slaa.



Na vilevile mazingira yanaonyesha kua:- HAWA CCM WAMEKUA WAKISHIKWA NA UFISADI NA MAMBO WAKAYAZIMA KIMYAKIMYA. KAMA ESCROW, EPA, RADAR M, NDEGE YA GHULF STREAM, NK. Kwakua yanagusa wale untouchoubles.

Sana sana ubuyu ulikua unaonyesha kuna mahusiano mabovu kati yake na jk aliyekua mkuu wa nchi. Ndio chanzo cha yeye kukatwa. Na asilimia 75%ya ubuyu kwenyw.organization.yoyote.kina ukweli.

EL ALIhoji ikiwa yeye ndiye fisadi je hizo hela MILIONI 150(Round figure) zinazoendelea kulipwa. Ni nani anazichukua?

CCM hawajajibu. Wamefanya kupotezea. Kama wafanyavyo kule kwingine. Thats why i hate politics.
Unafiki juu ya unafiki.

Nashangaa waliomtuhumu EL wakati wa kampeni na sasa wameshika mamlaka na wamekaa kimya kama hakuna walichokisema Plus dk Slaa. Mmetumiwa kama kondom.... mmeshatupwa.
Na sasa mnazimiwa bunge maninerrr.. msisikie tena.
Na bado mnahangaika na wasio na Dola kama Lowasa.
Aibu yenu.

My take:-.kumtusi EL kwa kumwita fisadi haina tija na ni dhambi, Njia sahii ni kuwa simamia wale wenye mamlaka wamshtaki EL kwa ushahidi waliomtuhumu mkawaamini na kuwapa dhamana. So far mpaka leo majipu yanatumbuliwa sijasikia el akitumbuliwa popote.

Na kama waliomtuhumu hawamshtaki tena basi mmetapeliwa. Mmefanywa malofa kwelikweli. Mmelamba garassa.

Mwajifanya mwajua kumbe mnaungua jua.Nuff said.

Nahop nimejifafanua vya kutosha.
Wabongo waliandamana eti hawali mapanki ili kumfurahisha jk
Wakati wanakula. Leo mnaimba nyimbo za kujikomba kwa dola lakini nyie ndio imekula kwenu.

Kula like mara tano ingawa Lumumba wanaona mkwamo wa kuleta maendeleo nchi hii ni Lowassa
Kwa ujumla wanakikimbia kivuli chao
 
Nalima ndizi na kufuga mbuzi mkuu, hua nakuja mjini mara moja moja kuleta mazao yangu, hata huku shamba pia JF inapatikana
Hivyo ndivyo mwanaume anavyotakiwa kuwa, hongera sana, kumbe ni mahaba ya ukada tu hapa JF, kilimo ndio uti Wa mgongo, japo sijajua slogan ya Magu ktk kilimo
 
Tatizo unafiki tu.

Fine! Tuseme Lowassa siyo fisadi,sasa huoni kwamba wewe ni mpumbavu kwa kuendelea kuwaamini hao waliokukaririsha Lowassa Ni fisadi kwa miaka 8? Huoni kwamba unatutangazia kwamba hujitambui?

Kipindi bwana zenu wanatangaza list of shame mbona mlikuwa hamuwapingi badala yake mlikuwa mnakenua tu.

Kama mmeamua kushikiwa akili basi tafuteni watu wenye akili timamu ndiyo muwape otherwise kila siku mtakuwa mnaonekana wapumbavu tu.

Msiojielewa ndiyo mtaji kwa wanasiasa maanake mnakaririshwa tu kama kasuku wala hamhoji halafu mnakimbilia huku kututangazia viwango vyenu vya umbumbumbu.

Elimu, Elimu, Elimu....
Wewe umeulizwa mbona ufisadi wa Lowassa hauonekani kwenye ripoti za CAG? unajibu pumba
Lowassa alishawaambia kama mna ushahidi mpelekeni mahakamani otherwise mpige kimya badala ya kuendelea kuandika upumbavu humu.
Mamlaka mnayo,kila kitu mnacho mnashindwaje kumfunga mwizi?
Naona ni wakati sasa wa kuacha kuongea maneno yasiyo na proof
 
Mpaka sasa sijafanikiwa....bado naendelea. Nachotaka ni kumpata Lowasa ili nimlipue atumbuliwe na Magufuli. Nalazimika kutumia ripoti hii maana Richmond inayosemwa hawamchukulii hatua yeyote nguli huyu, ni maneno maneno ya kanga tu toka Lumumba na vibaraka wao. Ina maana huyu "fisadi" kaweka mamlaka zote mfukoni? Mpaka Ikulu? Majipu yanatumbuliwa, mengine yanatajwa lakini yanashindikana, lakini Lowasa jiiiii

Kweli aisee, tuwaulize waliokuwa viongozi waandamizi wa Chadema; Dr. Silaa na Tundu Lissu kwa kumsingizia huyu jamaa na kumweka kwenye orodha ya mafisadi.
Inabidi tumuulize pia Kamanda Lema kwa kutuaminisha kuwa ni heshima kubwa kwa Mungu kumzomea fisadi Lowassa.
Walahi, makamanda hawa wa Chadema wanapaswa watueleze vizuri na wanyooshe Kiswahili hapa..
 
Back
Top Bottom