Uchaguzi Tanzania haukuwa na "dosari"
Wachunguzi wa uchaguzi nchini Tanzania wamesema hakuna taarifa yoyote kuu ya dosari iliyojitokeza inayoweza kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili.
i
Kiongozi wa jopo la wachunguzi kutoka Jumuiya ya Madola Bw Paul East, amesema uchaguzi huo uliendeshwa vyema ikilinganishwa na ya miaka mitano iliyopita.
Hata hivyo East amesema kuchapishwa kwa matokeo ya uchaguzi huo kumecheleweshwa sana.
Amesema kutokana na kuwepo teknolojia ya kisasa, haipaswi matokeo hayo ya uchaguzi kuchukua siku nne hata tano kuweza kujulikana.
Wakati huo huo Mawaziri kadhaa tayari wamepoteza viti vyao vya ubunge katika uchaguzi huo

Kuna akili nyingine inaniambia kwamba waangalizi hawa wa kimataifa hawana tija kwenye hizi chaguzi zetu maana tangu waanze kuja hakuna kinachobadilika wala kuongezeka zaidi ya kushabikia dhuluma dhidi ya wengi.
hii jumuiya ya kimataifa ndiyo inayofaidika na mikataba mibovu wanayoingia viongozi wetu kwa kununuliwa kwa vipande vya pesa. Mimi nasema kwamba ripoti yao ni another evidence ya jumuiya ya kimataifa kufukarisha maendeleo ya nchi maskini za afrika.
next time tuwakatae tuweke waangalizi wetu wenyewe.
hii itawezekana endapo tutaibadili serikali DHALIMU hii iliyopo.