Ripoti ya Uwajibikaji: Changamoto za Usimamizi wa Rasilimali watu katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Katika ukaguzi wa mwaka 2019/20, CAG ameonesha changamoto zifuatazo katika usimamizi wa rasilimali watu katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa;

Idara ya Ujenzi, Sekta ya Elimu na Afya kuathiriwa na Upungufu wa Watumishi 119,753

Katika mapitio ya idadi ya wafanyakazi katika Halmashauri 123, CAG alibaini uhitaji wa watumishi 353,034. Hata hivyo, watumishi waliopo ni 233,281 na kupelekea upungufu wa watumishi 119,753 sawa na asilimia 34.

Upungufu huo umeathiri zaidi idara ya ujenzi pamoja na sekta ya afya ni elimu. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya vituo vya afya katika Vijiji/Kata na ongezeko la uandikishwaji wa wanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari lililosababishwa na utekelezaji wa sera ya elimu msingi bila malipo tangu mwaka 2016/17.

Kwa kipindi cha miaka minne, kumekuwa na upungufu wa watumishi kati ya asilimia 32 hadi 34 katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Kwa mwaka wa fedha 2016/17 upungufu wa watumishi ulikuwa ni asilimia 32 katika Halmashauri 161, kwa mwaka 2017/18 ni asilimia 33 katika Halmashauri 158, kwa mwaka 2018/19 ni asilimia 33 katika Halmashauri 169 na kwa mwaka 2019/20 ni asilimia 34 katika Halmashauri 123.

WAJIBU INSTITUTE
 
Back
Top Bottom