mchapa shughuli
JF-Expert Member
- May 19, 2011
- 549
- 422
Mangula-nguzo muhimu iliyosaidia ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika miaka ya 80.
Kwangu mimi Mangula ni kiongozi wa mfano daima. Mangula ndiye aliyeijenga CCM na kuiwezesha kumuongezea kura Mkapa mwaka 2000 na pia kumpa kura za kumwaga Kikwete mwaka 2005. Lakini pamoja na jitihada zake nyingi alizozifanya kwa maslahi ya chama chake akaishia kutoswa na Kikwete. Nina uhakika Mangula angekuwa bado yupo CCM CHADEMA wasingefurukuta maana mzee alikuwa ni mtaalamu wa propoganda hasa. Ninakumbuka pale aliyakatalia mataifa ya magharibi kuingilia mgogoro wa Zanzibar. Na akafanikiwa kuingia kwenye mazungumzo ya muafaka na CUF. Hata kama hayakuwa na mafanikio, angalau yalisaidia kuleta hali ya utulivu Zanzibar.
Inasikitisha sana kuona nyota yake inazimwa kirahisi kiasi hiki. Laiti isingekuwa ni hofu ya kukolimbwa naamini Mangula angeweza hata kwenda CHADEMA akakijenge CHADEMA pia. Lakini Mungu amemlipa sana. Naamini huko Africa kusini atakuwa analipwa vema kuliko hata angekuwa bongo.
Kuna jamaa yangu nilikuwa napiga naye story those days Mangula akiwa katibu mkuu wa CCM, aliniambia Mangula ndiyo think tank ya Taifa. Kwamba alikuwa ana uwezo hata wa kumwagiza Mkapa afanye hili au lile. Halafu Mkapa naye akawa anamfurahia sana namna ambavyo mawazo yake yalikuwa yanatekelezeka.Hata kama angelikuwepo. Watanzania si kama zamani. Nyie mnafikiri ni Mabwege tu wa kubebwa kama watoto.
Mtaji mkubwa wa Chadema ni matatizo ya Wananchi yanayotokana na ukilaza wa CCM/mwamko wa Watz. Sasa kama Magamba wako busy kujitajirisha na nchi inauzwa kila siku, unafikiri watu wataacha kutafuta mbinu wajinasue na matatizo?
Kama Kikwete angelikuwa kiongozi mwenye kujali, basi mengi tunayosema leo wala tusingelisema. Ila sasa, watu wazuri wote kwa sasa hawatakiwi CCM. Sasa unategemea Mangula angelibaki? Ilikuwa lazima atoswe. Yamebaki mazee yenye fikra za kuleta watoto wao wawe Marais.
Kila hali inaonyesha kuwa Kikwete aliletwa na Mwinyi na nafikiri lengo ilikuwa ni Kikwete amuachie Mwinyi mtoto awe Rais. Sijajua kama watamfanya awe Rais wa Tanzania au Zanzibar...... Zenji wanamfaa ili huko nako mabomu yalipuke maghalani.
Kuna version nyingine niliosikia ni kwamba Mangula alikuwa ame compile, kwa kushirikiana na UWT, madhambi ya Kikwete na jinsi alivyopata utajiri wa haraka---corruption. Ile ripoti ilikuwa itolewe mbele ya kikao kikuu cha kujadilia wagombea. Lakini ripoti hiyo ilizimwa na Mkapa kwa kusema kuwa hakuna aliye msafi ndani ya CCM. Hilo likawa anguko la Mangula baada ya Kikwete kuteuliwa kuwa mgombea. Pia si kweli kuwa Mkapa alimtaka Salim. Ni yeye aliyesema kuwa hawezi kumwachia nchi Mwarabu.Kuna jamaa yangu nilikuwa napiga naye story those days Mangula akiwa katibu mkuu wa CCM, aliniambia Mangula ndiyo think tank ya Taifa. Kwamba alikuwa ana uwezo hata wa kumwagiza Mkapa afanye hili au lile. Halafu Mkapa naye akawa anamfurahia sana namna ambavyo mawazo yake yalikuwa yanatekelezeka.
Lakini naamini sana kwamba katika kipindi hiki cha Kikwete, kama Mangula angekuwa ndiye katibu mkuu wa CCM ni either angeresign au angefukuzwa, kwa kuwa Kikwete anataka aonekane yeye yupo juu ya kila kitu. Hapendi wachapakazi na anapenda sana kuonekana kwa watu. Kwa hiyo asingependa kabisa aamrishwe na Mangula kutekeleza baadhi ya mambo. Nafikiri wote mnakumbuka vizuri kampeni za CCM za wakati ule wa akina Mangula. Na mnaweza kutofautisha na hizi za mwaka jana.
CCM wamepoteza Kichwa mhimu sana. Kuna haja ya kumwomba ajiunge na CHADEMA. Pengine atatupa tips mhimu za kuimaliza CCM. Ngoja nitakwenda kumuongelesha nione anasemaje.
Duh, kumbe kuna mengi behind the scene. Nilipopigia mstari sikuwa najua kabisa kama kuna habari hiyo. Hii kali kwakweli.Kuna version nyingine niliosikia ni kwamba Mangula alikuwa ame compile, kwa kushirikiana na UWT, madhambi ya Kikwete na jinsi alivyopata utajiri wa haraka---corruption. Ile ripoti ilikuwa itolewe mbele ya kikao kikuu cha kujadilia wagombea. Lakini ripoti hiyo ilizimwa na Mkapa kwa kusema kuwa hakuna aliye msafi ndani ya CCM. Hilo likawa anguko la Mangula baada ya Kikwete kuteuliwa kuwa mgombea. Pia si kweli kuwa Mkapa alimtaka Salim. Ni yeye aliyesema kuwa hawezi kumwachia nchi Mwarabu.
msema hovyo nimerudi baada ya kukaa mafichoni kwa muda mrefu kidogo nikipanga mipango ya maandamano makubwa ya kumng'oa ngeleja na rais wake. Kwa bahati mbaya inteligensia yetu imetutonya kwamba tayari intelijensia ya polisi ilikuwa inatufuatilia kwa karibu na hivyo tungeweza kuishia jela kabla ya maandamano kuanza. Tunajipanga kwa strategy mpya kwa sasa.
Lakini leo nimekuja na hili kubwa ambalo nimelipata kutoka vyanzo vya uhakika ndani ya ccm. Ni kwamba kisa cha mangula kutoswa na kusahaulika kabisa ni kutokana na mangula kugoma kumpa jk form ya kugombea urais. Inasemekana mangula katika uzoefu wake alikuwa anamjua kikwete kama mtu asiye na uwezo wa kuongoza nchi, lakini anayependwa sana na watanzania. Mangula alijua katika hali yoyote, kama kikwete angefanikiwa kupata form lazima angeshinda urais, na namna pekee ya kumuengua ilikuwa ni kumnyima form.
Inasemekana mwinyi (ali hassan) ndiye aliyemkomalia mangula plus mkapa kwamba wampe jk form akakataliwe na wananchi. Katika targeti yao, mkapa na mangula walitaka salim a salim ndiye achukue urais na si kikwete. Lakini kutokana na ubabe wa mwinyi na hofu ya kwamba kama mwinyi angeamua kuside na kikwete kungeleta mpasuko ndani ya chama, basi ikabidi akina mangula waruhusu jk achukue form ya urais. Na matokeo yake ndiyo haya tunayoona sasa. Kikwete anaendesha nchi hovyohovyo.
Shida zote tunazozipata watanzania, chanzo ni mwinyi. Ndiyo maana jk alitumia muda mwingi sana kumshukuru mwinyi katika hotuba yake ya kwanza bungeni. Habari ndiyo hiyo.
Mhe Jasusi, uko sahihi kabisa, Mkapa aliachia uenyekiti wa sisiemu kabla ya muda kamili wa kuachia nafasi hiyo haujafika, akamuachia mwenyekiti wa sasa mhe. Kikwete, ambaye aliitumia nafasi hiyo effectively kuwaondoa wale asiowataka. Hope unakumbuka vizuri jinsi wanamtandao walivyovuruga uchaguzi wa mwaka 2007 katika ngazi zote, na vurugu zile hazijaisha, wanamtandao wanajipanga kwa uchaguzi mkuu wa chama mwakani. Wale wasioiva na JK (kutoka makundi ya Sumaye, Mwandosya na Salim) ndo wanataka kumvua uenyekiti, ili asiwe na nguvu katika chama, picha ndo kwanza inaanza. Kiini hasa cha kuvuana magamba ni juhudi za kutaka ku-deal na hao wanaotaka kumpoka hilo rungu. Anayeua kwa upanga hufa kwa upanga pia.Idimi,
Nimekukubali. Lakini kumbukumbu zangu ni kwamba Mangula aliondolewa ukatibu mkuu mara tu baada ya Kikwete kuukwaa uenyekiti wa CCM.
Mkuu habari hizi nzuri sana hebu endelea kutupa zaidi..mwaka huu tutasikia mengi sana..bado wanavuana magamba, kuna kambi rasmi ya upinzani ndani ya ccm(ccj), bado matatizo kibao na ahadi hewa za ccm...Mhe Jasusi, uko sahihi kabisa, Mkapa aliachia uenyekiti wa sisiemu kabla ya muda kamili wa kuachia nafasi hiyo haujafika, akamuachia mwenyekiti wa sasa mhe. Kikwete, ambaye aliitumia nafasi hiyo effectively kuwaondoa wale asiowataka. Hope unakumbuka vizuri jinsi wanamtandao walivyovuruga uchaguzi wa mwaka 2007 katika ngazi zote, na vurugu zile hazijaisha, wanamtandao wanajipanga kwa uchaguzi mkuu wa chama mwakani. Wale wasioiva na JK (kutoka makundi ya Sumaye, Mwandosya na Salim) ndo wanataka kumvua uenyekiti, ili asiwe na nguvu katika chama, picha ndo kwanza inaanza. Kiini hasa cha kuvuana magamba ni juhudi za kutaka ku-deal na hao wanaotaka kumpoka hilo rungu. Anayeua kwa upanga hufa kwa upanga pia.
Mkuu habari hizi nzuri sana hebu endelea kutupa zaidi..mwaka huu tutasikia mengi sana..bado wanavuana magamba, kuna kambi rasmi ya upinzani ndani ya ccm(ccj), bado matatizo kibao na ahadi hewa za ccm...Mhe Jasusi, uko sahihi kabisa, Mkapa aliachia uenyekiti wa sisiemu kabla ya muda kamili wa kuachia nafasi hiyo haujafika, akamuachia mwenyekiti wa sasa mhe. Kikwete, ambaye aliitumia nafasi hiyo effectively kuwaondoa wale asiowataka. Hope unakumbuka vizuri jinsi wanamtandao walivyovuruga uchaguzi wa mwaka 2007 katika ngazi zote, na vurugu zile hazijaisha, wanamtandao wanajipanga kwa uchaguzi mkuu wa chama mwakani. Wale wasioiva na JK (kutoka makundi ya Sumaye, Mwandosya na Salim) ndo wanataka kumvua uenyekiti, ili asiwe na nguvu katika chama, picha ndo kwanza inaanza. Kiini hasa cha kuvuana magamba ni juhudi za kutaka ku-deal na hao wanaotaka kumpoka hilo rungu. Anayeua kwa upanga hufa kwa upanga pia.