Ripoti ya tume ya maadili ya Philip Mangula iko wapi?

Ripoti ya tume ya maadili ya Philip Mangula iko wapi?

Alikuwapo Philipo Mangula katika siasa ya Tanzania Chama cha Mapinduzi
Mtu huyu yuko wapi na anafanya nini sasa Kutoka Ukatibu Mkuu wa CCM mpaka jina kufifia namna hii
Yuko nyumbani kwake akiangalia wenzake akina Makamba "wanavyojua kuendesha nchi"
 
yupo kule anakoelekea makamba.huko ndo utampata...kwenye ulimwengu wa kufilisika kabisa kisiasa na kusahaulika kama alishawahi kuexist.
 
Alikuwa mkuu wa wilaya nikiwa shule ya msingi. Nilimwa-admire sana kwa jinsi alivotumikia kazi yake kwa makini na kujitolea. Alikuwa mjamaa sana. Huwezi kumlinganisha makamba na Mangula. Mangula ni mtu mwenye hekima na mfikirivu. Makamba IQ yake ndogo sana halafu ni mtu anayesema kwanza kabla ya kufikiri. Intelligency ya MaKamba ni degenerative. Kwa kweli hafai kushika madaraka ya juu kwenye taasisi.
 
Alikuwapo Philipo Mangula katika siasa ya Tanzania Chama cha Mapinduzi
Mtu huyu yuko wapi na anafanya nini sasa Kutoka Ukatibu Mkuu wa CCM mpaka jina kufifia namna hii

Jina lake la Philip limemponza.
 
Mimi hawa wazee siwafagilii kabisa wamekaa kwenye system years and years na hawakutufanyia lolote la maana kama taifa..zaidi ya kutuaminisha kwamba walikuwa ni waumini wa Nyerere......let them get lost kwenye siasa....wengine wajaribu.....
 
Kwa taarifa tu hakuwa anategemea utabiri wa sheikh. Alikwa hatari kwa mustakabali wa mtandao. Kunguru mwoga,,,,,,,,,,, huficha......... Ila kiukweli hawa jamaa wanatisha wakiamua kukupoteza. Hivi huwa roho haziwaumi? Yaani ukikumbuka ya Kolimba miguu inajaa maji.
 
CCM wakaiamua kukupotezea tuuu.............................
 
Alikuwapo Philipo Mangula katika siasa ya Tanzania Chama cha Mapinduzi
Mtu huyu yuko wapi na anafanya nini sasa Kutoka Ukatibu Mkuu wa CCM mpaka jina kufifia namna hii
Mara ya mwisho nilimsikia alipochakachuliwa katika kura za kugombea uenyekiti wa Mkoa wa Iringa ambapo ilisemekana walimpa alama za kutofaa hata kuongoza Kata! Hiyo ndiyo CCM; chama kilichopoteza kabisa uelekeo na kukumbatia mabaya yote Mwasisi wao Mwl. Nyerere aliyowaasa kuyaacha. Sasa CCM wanajitanabahisha na Ukabila (Unakumbuka yaliyompata Dr. Salim?), Udini, na ubaguzi wa kipato kwani kwa CCM ya leo kila nafasi ya uongozi ina bei yake na kamwe usitazamie kupata nafasi ya kugombea hata udiwani wa kata kama huna fedha. Tatizo la baadhi ya wana CCM ni uoga wa kujiunga na wanaharakati wa upinzani kwa hofu ya kuitwa wasaliti. Mimi naamini Mzee huyu bado ana nguvu za kutosha na mchango wake unahitajika sana katika Tanzania hii iliyokwenda arijojo. Namshauri ajiunge na Upinzani kuharakisha mabadiliko yatayolinusuru taifa letu na kuangamizwa na 'vibakauchumi' waliosheheni CCM na ambao wanalikana jina wanalostahili la mafisadi.
 
Kwenye hili mzee wa watu alikuwa very objective kiukweli wala haikuwa personal kihivyo. I have come to learn kwamba huyu mzee anamjua huyo mnayemwita muungwana (kwangu mimi c muungwana otherwise asingpiga risasi na kuua wapiga kura wake juzi arusha) kuliko wengi wetu. Watanzania wengi ni mashahidi namna kazi inavyomlemea mkwere, yaani ni kama vile kibajaji kukibebesha mzigo wa tani 30. Kibaya kuliko vyote ni kwamba by then Mzee MAngula hakueleweka na wengi, tulimwona mtu mbaya anayetaka kutupotezea handsome boy wetu, mtu wa watu kipenzi cha watu, you name it. Anyway ndio hivyo tena imekula kwetu hiyo.

Tusimtetee Mangula kirahisirahisi.Tujiulize,kama alimuona Kikwete hafai kuwa Rais,ni nani lilikuwa chaguo lake?Je lilikuwa ni chaguo kwa maslahi yake au maslahi ya taifa?Je huyo mtu wake,angetufaa?
 
labda mzee alijua mapema hasara ya kumweka huhu nanga tuliyenaye sasa! Si alisema mkwere akishinda ataenda kulima...hahaha
Nashangaa alishindwa kum-kolimba mkwere! angetu-save sana!
 
Mwaka jana Disemba niliuliza swali hilihili na baadhi ya jawabu zilizopatikana kuongezea zilizopo zilikuwa hizi:

Kuna kipindi fulani mwaka huu alikuwa nafanya special assignments za chama cha ANC. Jamaa bado anaonekana kuwa resourcefull kwa wenzetu. Sijafahamu details za hiyo assgnments. Kama mara mbili alikuwa ndge moja na ndugu yangu wa karibu kuelekea SA (kutoka kwa Whisper)

Ni mshauri wa mambo ya Siasa wa Jokob Zuma. Mara nyingi huwa huyupo bongo, yupo South Africa kwa muda mrefu. Nafikiri hiyo assignment unayoisema Whisper ni kubwa, probably yupo kwenye nafasi kama ya akina Kingunge kwa huku bongo (kutoka kwa Lulongo).
 
labda mzee alijua mapema hasara ya kumweka huhu nanga tuliyenaye sasa! Si alisema mkwere akishinda ataenda kulima...hahaha
Nashangaa alishindwa kum-kolimba mkwere! angetu-save sana!

Kwani Philip Mangula alishawahi kum-kolimba nani?naona anahusishwa sana na hili neno ku-kolimba
 
Msema hovyo nimerudi baada ya kukaa mafichoni kwa muda mrefu kidogo nikipanga mipango ya maandamano makubwa ya kumng'oa Ngeleja na Rais wake. Kwa bahati mbaya inteligensia yetu imetutonya kwamba tayari intelijensia ya polisi ilikuwa inatufuatilia kwa karibu na hivyo tungeweza kuishia jela kabla ya maandamano kuanza. Tunajipanga kwa strategy mpya kwa sasa.

Lakini leo nimekuja na hili kubwa ambalo nimelipata kutoka vyanzo vya uhakika ndani ya CCM. Ni kwamba kisa cha Mangula kutoswa na kusahaulika kabisa ni kutokana na Mangula kugoma kumpa JK form ya kugombea urais. Inasemekana Mangula katika uzoefu wake alikuwa anamjua Kikwete kama mtu asiye na uwezo wa kuongoza nchi, lakini anayependwa sana na watanzania. Mangula alijua katika hali yoyote, kama Kikwete angefanikiwa kupata form lazima angeshinda urais, na namna pekee ya kumuengua ilikuwa ni kumnyima form.

Inasemekana Mwinyi (Ali Hassan) ndiye aliyemkomalia Mangula plus Mkapa kwamba wampe JK form akakataliwe na wananchi. Katika targeti yao, Mkapa na Mangula walitaka Salim A Salim ndiye achukue Urais na si Kikwete. Lakini kutokana na ubabe wa Mwinyi na hofu ya kwamba kama Mwinyi angeamua kuside na Kikwete kungeleta mpasuko ndani ya chama, basi ikabidi akina Mangula waruhusu JK achukue form ya Urais. Na matokeo yake ndiyo haya tunayoona sasa. Kikwete anaendesha nchi hovyohovyo.

Shida zote tunazozipata watanzania, chanzo ni Mwinyi. Ndiyo maana JK alitumia muda mwingi sana kumshukuru Mwinyi katika hotuba yake ya kwanza bungeni. Habari ndiyo hiyo.
 
Haya yatakuwa ni maneno ya mtaani,kwani mangula halikuwa hana ubavu wa kumnyima fomu mgombea yoyote wa CCM kwa kuwa sheria na taratibu za uchaguzi ndani ya CCM haikumpa uwezo huo!ingawa nakubaliana na wewe kuwa JK anauwezo mdogo wa kuongoza nchi hii!!
 
kweli!? ...kumbe alishauona mwanga mapema na alitaka kuinusuru nchi. Kweli sikio la kufa... lakini kama unaamini uwezo uliomo ndani ya hawa WaTZ 45million, najua si muda mrefu atatokea MTZ mwenye uwezo na historia itaweza kuwasoma vizuri hawa wote walio/wanaotucheleweshea maendeleo na heshima ya nchi.
 
Haya yatakuwa ni maneno ya mtaani,kwani mangula halikuwa hana ubavu wa kumnyima fomu mgombea yoyote wa CCM kwa kuwa sheria na taratibu za uchaguzi ndani ya CCM haikumpa uwezo huo!ingawa nakubaliana na wewe kuwa JK anauwezo mdogo wa kuongoza nchi hii!!
Ni kweli kwamba kuna sheria za utoaji wa form lakini kama chama wanayo nafasi ya kusema huyu no or yes. Kwa hiyo Mangula katika nafasi yake alikuwa na nafasi ya kusema wewe no. Ni kama ambavyo Msekwa alimuita Lowassa na kumwambia achana na mbio za urais, ndivyo ambavyo Mangula alitumia lungu la nafasi yake kumuzuia Kikwete asichukue form ya kugombea urais. Kama huamini, basi tafuta source nyingine ndani ya CCM utapata ukweli wa hili.
 
Mkuu, lisemwalo lipo yasemekana alimwambia no way!!! ndo maana nguvu kubwa ya mtandao ilitumika kumwangusha ktk kinyang"anyiro kule iringa. Lkn je wajua sasa yuwapi??? nyungo za intelijensia zimenasa kwamba yupo kwa Madiba akiwa na cheo cha Mshauri wa Mambo ya Siasa kwa Mzee XUMA from the North!!!!

TAKE NOTE!!!!!!!
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Yaani hapo ndipo ninapochoka na hizi siasa za bongo (gutter politics). Unaamua kumtosa mtu kwa sababu tu ya bifu zenu unaacha kuangalia uwezo wake katika utendaji. Sasa Mangula anayemshauri Jacob Zuma si angefaa sana kumshauri Kikwete akiwa kama katibu mkuu wa chama? Although ninaamini kabisa kwamba Mangula angeendelea kuwa katibu mkuu wa CCM, Kikwete angeendesha nchi kwa shida sana. maana jamaa alikuwa very serious katika mambo yake.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mangula baba, kama umo humu Jf tupe ukweli! kama ni kweli, vizazi vijavyo vikukumbuke! na historia iandikwe! Kwa nini mnakuwa waoga?
 
MANGULA should be our hero maana he was that visionary! Mwinyazi Mungu amjalie...
 
Back
Top Bottom