Ripoti ya tume ya maadili ya Philip Mangula iko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti ya tume ya maadili ya Philip Mangula iko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Nov 1, 2008.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Nov 1, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  wana JF...


  ..ripoti ya tume ya Philip Mangula aliyefanya uchunguzi kuhusu kukiukwa kwa maadili ya chama wakati wa CCM presidential primaries imepotelea wapi?

  ..nadhani wakati umefika ripoti hiyo ipatikane kwani inaweza sana kutusaidia kuelewa yanayoendelea sasa hivi Tanzania.

  ..mwenye uelewa wa kilichomo kwenye ripoti hiyo naomba atuhabirishe.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Joka, unataka kufufua skeleton? Akikusikia Mkapa mtaelewana vibaya kwa sababu alishasema kuwa yale ni majungu
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  jokaKuu,
  Umeuliza swali la msingi. Nina hakika Mangula alijiwekea makala. Hata kama Mkapa atavimba kama anavyosema Mpita Njia, ripoti hiyo lazima ione the light of the day. Kama madhambi ya Mkapa yaliweza kufahamika, itakuwa vigumu kwa ya mwenzetu kufichika.
   
 4. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mnataka ripoti hiyo ya nini ama mtafanya nini? (mna uwezo gani?).
  Suala la EPA lina ushaidi tosha wa kuwakamata wahusika lakini serikali imelikalia na kupiga danadana, je wananchi mmefanya nini katika kutaka ukweli huo?. Na sasa mnataka ripoti ya Philip Mangula ili iweje?.

  Tanzania chini ya CCM hakuna demokrasia ya kweli na watanzania ni waoga katika kudai haki zao. Suala la EPA, RICHMOND. RADA, KIWIRA na shija kuwa $1,000,000 ni masuala tosha kabisa kuonesha kwamba Tanzania inaongozwa kisanii, watu waoga na machafuko yako njiani.
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele bro, nijuavyo ni kwamba Mangula mwenyewe alitaka kugombea urais, lakini kabla hajachukua fomu, mstaafu wa idara aliyekwua ametumw ana mkapa akamkataza hayo mawazo, lakini mangula hakuridhika na alikuwa akimuaminia sana makpa kua ni msafi na ataweka rais msafi baada yake, aliamini kwamba yeye mangula ni msafi kuliko wengi ndani ya CCM.

  Akaamua kwamba atacheza mchezo wa manipulation, kwa kuyachafua mafaili ya wagombea kwa makusudi, ili CCM ifike mahali iamue kwamba wagombea wote hawafai na hivyo yeye kupewa hiyo nafasi ya kugombea, lakini aliyemuuza ni Sozigwa aliyetoa siri hiyo mapema kwa Mtandao, ambao walipomkaba koo mkapa sharti lao la kwanza lilikuwa ni kwamba lazima azuie mafaili kujadiliwa na kuyakabidhi kwa Mtandao, mkapa did.

  That was pretty much the end of the story na hayo mafaili, niliwahi kubahatika kuyaona mawili, lakini kwa masharti magumu sana nikashindwa hata ku-kopy kwa simu maana sikuruhusiwa kuingia nayo humo ndani yalipokuwepo, kutokan na nilichokiona kwa kweli nilichokiona ulikuwa ni uongo na uzushi wa hali ya juu sana na binafsi ninasema thanks to God hayakutumika maana yangeweza kuamsha hata vita vya sisi wenyewe kwa wenyewe, kwa sababu hao wagombea wawili wahusika na hayo mafaili nilikuwa karibu nao sana hata kujua nyendo zao nyingi kwa karibu, yaliyokuwemo kwenye mafaili yale hayakuwa karibu kabisa na ukweli wa waliyoyafanya wakati wa kampeni, na jina langu lilikuwemo kwenye hayo mafaili nikituhumiwa kuhusika na kukusanya hela nyingi sana za kampeni toka kwa wazungu, hapo ndipo nilipokata tamaa kwani wananchi wa Tanzania wana-desrve better than what mangula did na yale mafaili,

  I mean haya ni machache ninayoyajua kuhusiana na yale "famous mafaili".
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  The other side of the coin. Mimi nilivyosikia kulikuwa na file kuhusu Mwungwana ambalo limetayarishwa na UWT. File hili lilikuwa linaorodhesha mali za mwungwana alizopata through corrupt means. I do not know or claim to know the contents of the file lakini ilipofika wakati wa kulitoa kwenye kikao, kazi ambayo alikuwa amepewa Mangula, Mkapa alimkatisha akisema kuwa hakuna aliye safi kati yetu. Ndiyo maana nimesema kuwa kuna siku yaliyokuwemo kwenye faili hilo yatafahamika. Siri huwa ya mtu mmoja. Faili likishaonwa na zaidi ya mtu mmoja si siri tena. FMES may be right but this is the version that I heard.
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Mkuu Jasusi,

  Heshima mbele, nijuavyo ni kwamba unalosema lilikuwa ni changa la macho, kwa sababu mstaafu wa idara alikuwa Mtandao, lakini kwa siri sana ni mpaka mtoto wake alipopewa ubunge wa bure na Mtandao ndi ikafahamika,

  hivi kweli unaamini kwamba angeweza kuandika hilo file la Muungwana, na kuruhusu lifike kule Maadili?
   
 8. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  SAM wa BCS forum yuko wapi? Kwa data zake za wakati ule wa uchaguzi 2005 lazima atakua anajua kilichoandikwa. Au ndie huyu huyu FMES

  PM
   
 9. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  I think this is an imaginary story.
   
 10. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Lets hope and pray for a better Tanzania. My only worry ni sisi kufikia stage ya DRC na nchi nyingine zenye vita. Maana kwa mtazamo wangu ndio tunaelekea huko. Hii migomo kila mahali na raisi kuzomewa huko Tabora ni dalili mbaya.
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Kwa mara ya kwanza niliztoa hizi habari rasmi mwaka 2005, haya ni marudio tu na infact siku nilipokwenda kuyasoma mafaili ndio siku niliyojionea barua kali ya Butiku, kwa Mkapa na nikyasema yote kule BCS, labda utafute mafaili ya BCS, otherwise pole sana na kazi uliyonayo maana kweli una nguvu na a lot of free time mkuu, hilo ninakupa!
   
 12. C

  Chief JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2008
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Ndiyo Yeye.

  Ninachokumbuka kuhusuu hii issue enzi za BCS (sikumbuki kama ni Sam ndiye alikuwa author but I'm inclined to believe) ni kwamba ni kweli Mangula aliwasilisha dossier ya kumchafua JK mbele ya BWM na kwa wakati ule haikuwa alleged kuwa dossier ile ilikuwa cooked. Lakini kabla ya hapo Mtandao ulishatayarisha dossier ya BWM na RA alienda Ikulu na hii dossier na kum-blackmail kuwa kama JK hatapitishwa kuwa mgombea, basi yote yaliyomo humo ndani yatawekwa public na mtandao utajitoa CCM. Mrengo wa BWM wakati ule ulikuwa ni kumpendekeza Kigoda. Kama sikosei, ndio sababu inayosemekana ya CHADEMA kuchelewa kumtaja mgombea wake wakitegemea kuwa huenda JK angehamia kule.

  Hivyo Magula alikuwa shocked kuona kuwa file alilolitayarisha la JK likitupwa pembeni.

  JUst a small recap from the once mighty BCS
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0

  Sawa sawa 100%, exactly habari ndio hiyo.
   
 14. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2008
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka si kweli kuwa Mwang'onda alikuwa mtandao. Yeye alifanya kila njia ya kupambana na mtandao hadi mwisho alipoona upepo mkali mno ndipo alipojipeleka ktk mtandao na kufanya makubaliano maalum nao halafu ndipo alipobebeshwa dozi iliyomfanya Mzee Ben kuingia line na kukubali yaishe. TOM alikuwa karibu "kiasi" na mtandao lakini sababu ya kupewa ubunge ni kuhakikisha kuwa Mzee Mwang'aonda anaendelea kuwa loyal kwa JK na kumfanya ajione ni mdau huko hata kama sio kweli.

  Kazi ya Mangula haikufanywa na UWT kama asasi bali ilifanywa na sekretariat ya CCM maadili ambayo inahusishwa watu wa UWT. Na ukweli ni kuwa ripoti hiyo ipo imejaa kibao na wala sio tunu kama inavyodhaniwa hapa. Ripoti imejaa ukweli, uongo na habari za kusadikika. Hata hivyo kutoka hadharani kwa kweli ni hatari kwa chama na hata serikali iliyopo madarakani kama ilivyo kwa ripoti nyingine nyingi za aina yake.

  Tanzanianjema
   
 15. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2008
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  RA hakuwa na ubavu huo. Kwanza ilifika wakati alikuwa anahaha kuhakikisha kuwa anabaki salama hata kama JK anashindwa. Dozi ya Mzee BEN alibebeshwa Mwang'onda....

  Tanzanianjema
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Ahsante kaka, ninachojua ni mstaafu alipoenda Kenya ku-monitor uchaguzi kule kwa miezi mitatu aliogopeshwa sana na kushindwa kwa Uhuru kilichomfanya amkatae Kigoda chaguo la mkapa, aliporudi ndipo alipojiunga rasmi na mtandao kupitia kwa Rostam na Lowassa, lakini kwa siri kubwa sana kwa sababu at the same token yeye pia ndiye aliyekua mmoja wa wafadhili wakubwa financially wa JM, sipendi kuyarudia tena na tena maana nilishayasema sana awali, mtandao walitaka kumlipa kwa kumpa uwazri mdogo tom, mstaafu aliposikia akakimbia kwa mkulu mmoja na kumuuliza kama ni sawa, ni huyu mkulu ndiye aliyemuambia kwamba hapana kubali apewe ubunge tu, lakini omba rafiki yako na patner wako wa biashara mwakipesile apewe u-RC.

  Mstaafu alifanya mambo mengi sana tena kwa siri kubwa sana, kama sio mtoto wake kupewa ubunge hakuna ambaye angejua mimi nilipewa ujumbe mapema na waziri mmoja wa sasa, lakini hata mimi nilikuwa ninamuaminia sana mstaafu sikukubali kabisa nikasema ni uongo na majungu, haiwezekani mtu atoe mahela yote yale kwa JM lakini yuko kwa mtandao, baada ya kugundulika kuwa ni kweli mstaafu alikua nao, siku hizi hata jm haongei naye tena siku hizi, na huyu ndiye aliyekuwa kipenzi chake.

  Mkuu OmaryIlyasi ni habari ndefu sana siwezi kuzirudia zote, kuna siku moja mtoto mmoja wa jm aliwakamata lowassa, rostam na mstaafu kwa bahati mbaya usiku sana mahali Dodoma, alipofikisha ujumbe kwa kambi ya jm wakamkatalia kua sio kweli labda amefananisha tu, mimi nilipowapelkea ujumbe toka huyu waziri mmoja wa sasa walikataa kabisa sio kweli, baadaye tena niliambwia na mama ntimizi ambaye by then alikuwa karibu sana na sumaye, the same story lakini wakagoma kuwa sio kweli, only now ndio wamekubali.

  Siku tu alipoapishwa kuwa rais, muungwana the first thing alitaka kumtoa mangula kazi na makatibu wote wa mikao na wilaya, akidai ndio waliohusika na kuandika yale mafaili, lakini akatulizwa na mkulu mmoja wkamba ukiwafukuza huko mikoani watajiunga na upinzani na wataitwanga CCM kwenye uchaguzi, na besides akaambwia yeye bado hajawa mwenyekiti wa CCM, ni rais tu, ndio mtandao wakaanza kampeni chafu ya kumlazimisha mkapa atoke mapema kwenye uenyekiti, alipotoka tu kitu cha kwanza muungwana alimtoa mangula na sekretariati yake yote kulipa kisasi cha yale maafaili na mengine mengi lakini hii ni kwa ufupi ninachojua, huenda pia kuna tofauti zingine, lakini this is what I know!
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Hiyo dozi nijuavyo aliyepewa ni the only best friend wa mkapa, ruhinda, ambaye by then alikuwa ameajiriwa Vodacom na rostam three years inadvance kwa no show job ya mshahara wa sillingi millioni tatu kwa mwezi, kwa makusudi haya ya plan B iwapo A ya mtandao ingeshindwa. Mstaafu ndiye aliyehusika kwa 100% kutayarisha hiyo dozi, maana mtandao na rostam hawakuwa na resources za kutengenza hiyo dozi, na hasa biashara chafu za mama, ambazo ndio zilizotawala ile dozi kwa 70%.

  Na jinsi Joemaro alivyoileta netgroup, baada ya kuugua na kulazwa SA, ambako siku moja mkapa alikwenda kikazi akiwa rais na kuamua kupitia hospitali alipolazwa yaani kumuona joemaro, mkapa alipoondoka tu pale hospitali kuna mtu mmoja wa netgroup aliyemuona na kuamua kumrudia joe pale kitandani, the next thing netgroup ikaja.
   
 18. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Usinielewe vibaya ninacho tilia mashaka ni pale ulipoeleza kuwa yeye alikuwa na wazo la kugombea urais hapo ninakataa kwa masuala mengine sikupingi
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Nimesema hivi mangula alikuwa na nia ya kugombea urais, mkapa akamuwahi mapema kwa kumtuma mstaafu amwambie aache kuchukua fomu, atamuabisha bure, unasema hii habari sio ya kweli labda sijakupata vizuri?

  Halafu hii topic ilivyoanza nilidhani ni a serious one kumbe ni yale yale, okay I am out!
   
 20. M

  Masatu JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hii ripoti ya Mangula niliwahi kuisikia na inasemekana Mkapa alikataa kata kata isijadiliwe kwa kuwa ni uzushi
   
Loading...