Zungu Pule
JF-Expert Member
- Mar 7, 2008
- 2,218
- 1,218
Mimi pia napata wasiwasi kuwa ripoti hii ni nyeupe. Haina makali tunayotarajia. Ukisoma kurasa zilizowekwa hapa na Invisible na zinazodaiwa kunyofolewa, hazina Makali. Zitto pia aliwatahadharisha wabunge wajiandae kujadili facts na sio watu, akimaanisha kujadili taasisi/regulators waliofanya uzembe fulani, kwa mfano, serikali ikashindwa kukusanya kodi kutokana na muamala wa akaunti ya Tegeta escrow. Hapa Zitto anatoa signal kwamba ripoti ya CAG haijamtuhumu mtu bali imeonesha mapungufu ya kimfumo. Hata hivyo, hatujajua ripoti ya TAKUKURU ina nini.