Ripoti ya PAC yaibwa Bungeni mpaka ya CAG iliyoko Dar!

Ripoti ya PAC yaibwa Bungeni mpaka ya CAG iliyoko Dar!

Eti ukawa wacharuka ripoti kusambazwa mitaani, mbona wao wanatuhumu watu na taasisi mbalimbali bila kusubiri ripoti ya uchunguzi. Na kama pesa ni za wananchi kuna ubaya gani wananchi wakiona hiyo ripoti.
 
Eti Nimrod Mkono yu hoi hospital London!!! Ni shahidi muhimu sana katika sakata la ESCROW kama Balal katika EPA!!! Sijui atapona na kurudi mzima???!!!!
 
Kwa hatua waliyofikia hao mafisadi kwa sasa, uamuzi muafaka pekee uliobaki ni kuwa, kama wabunge wetu wote wa bunge letu watakuwa wazalendo na kuweka maslahi ya nchi mbele, bila kujali itikadi zao za vyama.

Itakapofika siku ya Jumatatu wakati wa kuanza kikao cha bunge asubuhi, waombe mwongozo wa kuomba bunge lisitishe shughuli nyingine na lilazimike kujadili suala la Escrow kama, suala la dharula sana.

Kwa hali inayoonekana jinsi mafisadi wanavyofanya kila njia ili ripoti hiyo isisomwe bungeni, kungojea ripoti hiyo isomwe siku ya Jumatano, tarehe 26, upo uwezekano wakatumia mbinu zozote, kwa kutumia vyombo vyao vyote vya dola, kama vile policcm, usalama wa watawala wa magamba, pamoja na mahakama kuhakikisha, ifikapo Jumatano asubuhi, kuwe tayari kuna zuio la mjadala huo usijadiliwe bungeni.

Kwa hali ilivyo sasa, naamini nchi yetu itakuwa inapitia katika kipindi kigumu ambacho, hakijawahi kupitia tokea nchi yetu ipate uhuru wake mwaka 1961 toka kwa mkoloni.

Kutajwa kwa majina waziwazi ya vigogo waliopata mgawo wa IPTL, kwenye ripoti ya CAG, ni jambo kubwa na la kutisha sana, kuliko watanzania wengi tunavyoweza kufikiri.
 
Eti ukawa wacharuka ripoti kusambazwa mitaani, mbona wao wanatuhumu watu na taasisi mbalimbali bila kusubiri ripoti ya uchunguzi. Na kama pesa ni za wananchi kuna ubaya gani wananchi wakiona hiyo ripoti.
Shangaa.
 
#Habari Mtu wa karibu na waziri wa nishati na madini Prof.Sos
peter Muhongo ni miongoni mwa wanaoshikiliwa na polisi kwa tuhuma za Escrow.
 
Kila mtu utaskia Watanzania tuko hivi mwengine tuko vile, wengine sijui hatujiamini, kila mtu analaumu Watanzania kwa kutokuchukua hatua.
Mtanzania ni mimi na wewe hebu tuanze then tuone na sio kusema juu juu tu. Swali ni "tunalianzisha vipi"
 
Taarifa ya (CAG) yakutwa ikisambazwa mitaani ikiwa imenyofolewa kurasa.

Taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali kuhusiana na kashfa ya wizi wa bilioni 321 kwenye akaunti ya tegeta Escrow iliyokabidhiwa kwa katibu wa bunge imekutwa inasambazwa mitaani huku ikiwa imenyofolewa kurasa tatu za mwisho zenye majina ya waliohusika na mgawo wa fedha hizo kwa lengo la kutengeneza propaganda ili kuwadanganya wananchi kuwa taarifa hizo hazijawataja wahusika.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti mwenza wa ukawa Mh. James Mbatia amesema zipo taarifa za baadhi ya waliokuwa wanasambaza taarifa hizo kuwa wamekamatwa na jeshi la polisi na kuwataka wananchi kutoa taarifa kituo cha polisi ili waweze kuchukuliwa hatua haraka ambapo amesesistiza kwamba (UKAWA) wanataka taarifa hiyo iwasilishwe bungeni kwa ajili ya kujadiliwa Jumatatu .

ITV imemtafuta kamanda wa polisi mkoa wa dodoma David Misime na katibu wa bunge Dr.Thomas Kashilillah ambao wamesema nao wanazisikia taarifa hizo na wanazifanyia kazi ili kutoa taarifa yao. Mia

Chanzo:ITV
 
Kuvujisha report mapema ni kuwapa watu nafasi ya kuisoma ili kwenye mjadala waje na tafsiri zao zisizokuwa na influence ya waandishi au nini?? Anayefahamu atujuvye athari zake ni zipi.

Nionavyo mimi, huku ni kutapatapa lakini hakuzuii mjadala wa taarifa hiyo hata kama kuna watu watakuwa mahakamani kwa ajili ya hilo taarifa.

Kwanza walichokamatwa nacho, wanachokitawanya siyo report, ni kipande cha taarifa ambacho si taarifa kamili.

Kesi inayowakabili siifahamu, lakini ninadhani wanatakiwa wafunguliwe kesi ya kukutwa na nyaraka za serikali kinyume cha sheria. Watasema ni nini kimewapa uwakala wa kutawanya hizo nyaraka.

Na hili halitazuia mjadala wa report kwa sababu report kamili bado ipo na naamini hakuna distortion imefanywa ambayo ingeleta utata wa kujadili taarifa hiyo.

Cha msingi hoja zijadiliwe bila ushabiki, visasi, wala kulindana.






Redio One Breaking news: ripoti ya ESCROW imepatikana ikisambazwa mitaani dodoma huku kurasa tatu za mwisho zenye maazimio zikiwa zimenyofolewa. watu kadhaa wanashikiliwa kwa sakata hili.
 
Kwahiyo sisi tufanye nini make hiyo ripoti walipewa PAC haya mengine sisi hatuelewi.
 
Taifa linaelekea pabaya sana , huu utakuwa muda na wakati muafaka ambao watanzania kwa ujumla wetu kutafakari ama tuendelee kutawaliwa na hiki kikundi kichache cha walafi na waroho wa keki ya Taifa au kuiondoa hii Serikali ya kifidadi madarakani.
 
Mkuu Informer kama ipo si mtuwekee na sisi tuipate hapa jamvini. JF siku zote imekuwa ndiyo inapata nyaraka kabla ya watu wengine, sasa hii inakuwaje inasambazwa huko Dodoma lakini JF hatujapata nakala, tumechoka siku hizi?

Litakuwa jambo jema kabisa.
 
Last edited by a moderator:
#Habari Mtu wa karibu na waziri wa nishati na madini Prof.Sos
peter Muhongo ni miongoni mwa wanaoshikiliwa na polisi kwa tuhuma za Escrow.
CPA kwani polisi washaanza kamata kamata kwenye hili swala, au ipoje hiyo?
 
Last edited by a moderator:
Jamani mbona ata hapa JF juzi zimetumwa page zina majina jumla yake pg28 zimetoka wapi? mi nadhan ni kazi bure since records zipo tutaprint nyengine. me nilifikiri wamefanikiwa kuwa report isisomwe bungeni
 
Back
Top Bottom