Ripoti ya Kifo cha Mwangosi

Ripoti ya Kifo cha Mwangosi

Duuuuuuh,

Bora hii kamati ya MCT...ile ya Nchimbi ndo imekuja na vituko kabisa...

TBC1 wameonesha kwenye taarifa ya saa 2 usiku, kamati ikielezea ripoti yake kwa waandishi. Mwenyeketi wa Tume anasema kuwa mauaji hayakutokana nguvu kubwa ila hawawezi kutaja sababu ya kifo kwa sababu kuna kesi mahakamani.

Hawa jamaa wamefanya usanii wa kupindukia!!
 
uchunguzi uliofanywa na tume kutoka jukwaa la wahariri wamedai polis ndio walimuua mwandishi huyo huku kamati ya dr. nchimbi ikidai polisi haiusiki moja kwa moja.
source:itv
 
I don't like stories, I hate longolongo..! Hakuna lolote la maana zaidi ya kulitia taifa hasara
 
Nipo na shangaz yangu hapa nae ameniuliza imekuwaje???nimekosa jibu,,,,
walio kwenye system watuambie,maana maelezo ya NCHIMBI SIYAELEWI
 
Well sijaifungua hii lkn taarifa nilizopata ni kwamba hawajadisclose chochote kwa madai kwamba wataingilia uhuru wa mahakama kwa kuwa suala liko ktk chombo hicho. So siku 30 za kazi plus posho walizolamba ndo hatima yake

Hii siyo ile ripoti ya Nchimbi dont confuse things, ripoti ya serikali ndo ina hang haina wala haijasema nani kamuua mwangosi ila imesema Jeshi la police haliusiki na mauaji ya David Mwangosi.
 
sidhani kama ni saplaiz kwa sababu ni kitu ambacho kilitarajiwa...inawezekana police ikawa haihusiku moja kwa moja kama wanavyodai wakati ushahidi wa picha na video zinaonyesha kwa uzuri sababu au chanzo cha kifo cha mwangosi (r.i.p)
 
Hiyo ya kamati ya nchibi bora hata isingeundwa. Naona imeleta report ya kuwasafisha PoliCCM kiaina!!!!
 
Dah yani hii kamati imeboa sana mbona viongozi wanapenda kutuona sisi ni mazuzu eti polisi hawakuhusika ktk mauaji ya mwangosi, jamani hata picha zimeonesha sijui tatizo lipo wapi.

Nchimbi anasema kuna baadhi ya taarifa zimefichwa ili kupunguza mgongano na mahakama. Mungu atusaidie
 
Wanajamvi,
Naona kuna kuchanganyikiwa kwa aina fulani. Ningependekeza Mod watenganishe taarifa hizi ili watu waelewe.
1. Kuna taarifa ya kamati iliyoundwa na MCT na Jukwaa la habari(TEF). Ipo katika kiingereza na kiswahili.
2. Kuna taarifa ya 'kamati' ya Nchimbi kama ilivyoletwa katika post# 129.

Maoni yangu
Taarifa ya MCT imeeleza kwa ufasaha yale tuliyokuwa tunayajua. Tofauti ni kuwa upo mpangilio maalumu wa tukio muda na wahusika. Taarifa hiii ilizama kwa kina katika kutoa habari za nini kilitokea.

Licha ya kina cha habari taarifa ya MCT na TEF ina mapungufu katika eneo la majumuisho (conclusion)
Eneo hilo halikuwa na mkazo wa nini wanapendekeza. Ukisoma taarifa utaona wametumia neno 'cover up' kuonyesha kuwa kuna 'kulindana'. Ukisoma jedwali utaona linaonyesha majina ya wahusika waliotoa taarifa potofu ili kufanya hiyo cover up.
Nilidhani walitakiwa waende moja kwa moja kwa akina nani wawajibishwe na kwasababu zipi.

Taarifa ya kamati ya Nchimbi
Hii taarifa ni ya kupuuza sana, siamini kuwa umeandaliwa chini ya usimamizi wa jaji mstaafu Ihme.
Hii inaonyesha tatizo kubwa kwa wataalam wa mambo ya kisheria.

Tatizo linalofanana na hilo ni la Theophil Makunga. Tulitahadharisha sana hapa JF kuwa, ili jamii ya wanahabari ipate heshima ni wajibu wa Theophil kujitoa. Kwanza kutoshiriki kamati inayofanana na ya harusi kwa vile haina meno na imeundwa kisiasa zaidi.

Tulisema hii ilikuwa mbinu ya Nchimbi kufunika kombe. Kwa bahati mbaya Theophil Makunga akaamua kuwatosa na kuitosa taaluma pengine kwa ujira kidogo. Nasema hivi kwasababu ukisoma taarifa ni ya kiwango cha chini, cha ajabu na cha kusikitisha. Kama Theophil ameshiriki vema basi tuna tatizo kubwa katika fani ya habari pia kama ilivyo ya sheria.

Ukisoma utaona kuwa taarifa hiyo ilikwenda kukusanya maoni ya watu na si uchunguzi. Sikutegemea taarifa hiyo ichukue nukuu za akina Shibuda na watu wengine mitaani tena kwa kuchagua ili iwe sehemu ya taarifa.

Taarifa inaonyesha wazi kuwa kifo cha Mwangosi kilitokana na uelewa mdogo wa kuandika habari katika maeneo ya hatari. Inapoandikwa kuwa waandishi wapewe mafunzo ni dhahiri taarifa inaonyesha tatizo kwao.
Hapo ndipo Theophil Makunga anapojikuta akiwasaliti wenzake na taaluma

Taarifa imejikita katika kutupa lawama kwa CDM. Eti mikutano ya siasa inawapunguzi watu muda wa kufanya kazi!
Inaongeza kuwa vyama vya siasa viache siasa za kibabe.
Hakuna nguvu kubwa iliyotumika
Kuwanukuu akina shibuda wa CDM kama ushahidi wa CDM kuwa chanzo cha mauaji
n.k.

Nitashangaa sana kama CDM watakaa kimya dhidi ya tuhuma walizotupiwa ili kukwepa ukweli wa mauaji ya Mwangosi.
Hakuna tulichotarajia na kama tulivyowahi kusema, Nchimbi kwanza alitakiwa aondoke ili apishe uchunguzi huru.

Tume ya Nchimbi ni ya kisiasa, haikuja na jipya, imepoteza pesa za uma na kutuletea taarifa ya kipuuzi sana.
Tutaendelea kubabaishwa hadi pale tutakaposiamama kwa pamoja na kudai haki zetu.
Kwa mara nyingine tumefanywa wendawazimu na Nchimbi, Jaji Ihema, Theophili Makunga, Chagonja, Kaumhanda, Mwema na kundi lao. Tutairejea taarifa ya Nchimbi aya moja hadi nyingine ili muone ujuha na uhayawani uliofanyika

Sasa tukae kimya kwasababu ndio njia tuliyochagua.

Inasikitisha sana!
 
Ripoti ya Nchimbi imekiri mwangosi ameuawa na askari aliyetumia bomu la mlipuko ambalo hutakiwa kupigwa degree 45 hewani!!! Na imependekeza askari wote walipmuzingira kumpiga wachukuliwe hatua

Tena baada ya operation ya polisi keisha

Huko iringa tijuzeni kama tayari wapo lupango,
 
Wanajamvi,
Naona kuna kuchanganyikiwa kwa aina fulani. Ningependekeza Mod watenganishe taarifa hizi ili watu waelewe.
1. Kuna taarifa ya kamati iliyoundwa na MCT na Jukwaa la habari(TEF). Ipo katika kiingereza na kiswahili.
2. Kuna taarifa ya 'kamati' ya Nchimbi kama ilivyoletwa katika post# 129.

Maoni yangu
Taarifa ya MCT imeeleza kwa ufasaha yale tuliyokuwa tunayajua. Tofauti ni kuwa upo mpangilio maalumu wa tukio muda na wahusika. Taarifa hiii ilizama kwa kina katika kutoa habari za nini kilitokea.

Licha ya kina cha habari taarifa ya MCT na TEF ina mapungufu katika eneo la majumuisho (conclusion)
Eneo hilo halikuwa na mkazo wa nini wanapendekeza. Ukisoma taarifa utaona wametumia neno 'cover up' kuonyesha kuwa kuna 'kulindana'. Ukisoma jedwali utaona linaonyesha majina ya wahusika waliotoa taarifa potofu ili kufanya hiyo cover up.
Nilidhani walitakiwa waende moja kwa moja kwa akina nani wawajibishwe na kwasababu zipi.

Taarifa ya kamati ya Nchimbi
Hii taarifa ni ya kupuuza sana, siamini kuwa umeandaliwa chini ya usimamizi wa jaji mstaafu Ihme.
Hii inaonyesha tatizo kubwa kwa wataalam wa mambo ya kisheria.

Tatizo linalofanana na hilo ni la Theophil Makunga. Tulitahadharisha sana hapa JF kuwa, ili jamii ya wanahabari ipate heshima ni wajibu wa Theophil kujitoa.
Kwanza kutoshiriki kamati inayofanana na ya harusi kwa vile haina meno na imeundwa kisiasa zaidi.

Tulisema hii ilikuwa mbinu ya Nchimbi kufunika kombe. Kwa bahati mbaya Theophil Makunga akaamua kuwatosa na kuitosa taaluma pengine kwa ujira kidogo. Nasema hivi kwasababu ukisoma taarifa ni ya kiwango cha chini, cha ajabu na cha kusikitisha. Kama Theophil ameshiriki vema basi tuna tatizo kubwa katika fani ya habari pia kama ilivyo ya sheria.

Ukisoma utaona kuwa taarifa hiyo ilikwenda kukusanya maoni ya watu na si uchunguzi. Sikutegemea taarifa hiyo ichukue nukuu za akina Shibuda na watu wengine mitaani tena kwa kuchagua ili iwe sehemu ya taarifa.

Taarifa inaonyesha wazi kuwa kifo cha Mwangosi kilitokana na uelewa mdogo wa kuandika habari katika maeneo ya hatari. Inapoandikwa kuwa waandishi wapewe mafunzo ni dhahiri taarifa inaonyesha tatizo kwao.
Hapo ndipo Theophil Makunga anapojikuta akiwasaliti wenzake na taaluma

Taarifa imejikita katika kutupa lawama kwa CDM. Eti mikutano ya siasa inawapunguzi watu muda wa kufanya kazi!
Inaongeza kuwa vyama vya siasa viache siasa za kibabe.
Hakuna nguvu kubwa iliyotumika
Kuwanukuu akina shibuda wa CDM kama ushahidi wa CDM kuwa chanzo cha mauaji
n.k.

Nitashangaa sana kama CDM watakaa kimya dhidi ya tuhuma wazlizotupia ili kukwepa ukweli wa mauaji ya Mwangosi.
Hakuna tulichotarajia na kama tulivyowahi kusema, Nchimbi kwanza alitakiwa aondoke ili apishe uchunguzi huru.

Tume ya Nchimbi ni ya kisiasa, haikuja na jipya, imepoteza pesa za uma na kutuletea taarifa ya kipuuzi sana.
Tutaendelea kubabaishwa hadi pale tutakaposiamama kwa pamoja na kudai haki zetu.
Kwa mara nyingine tumefanywa wendawazimu na Nchimbi, Jaji Ihema, Theophili Makunga, Chagonja, Kaumhanda, Mwema na kundi lao. Tutairejea taarifa ya Nchimbi aya moja hadi nyingine ili muone ujuha na uhayawani uliofanyika

Sasa tukae kimya kwasababu ndio njia tuliyochagua.

Inasikitisha sana!

Hivi hawa jamaa wanadhani kwamba sisi Watanzania ni wajinga kiasi hicho au wenyewe ndio wamejifanya wehu na kutuletea taarifa ya kipuuzi namna hiyo.

Ila nadhani sasa kuna haja ya kumfahamu vizuri huyo traitor wa waandishi wa habari (T. Makunga)!!
 
Naomba kujuzwa hili.. Yule RPC Kamuhanda bado yuko na wadhifa wake hapo Iringa..?
Aende wapi?Aujiuzulu kwa lipi?wangapi wameshajiuzuli kwa matatizo ya nchi hii?Alitaka astaafu kwa amani sasa ngoja laana ya kukandamiza demokrasia imuangukie yeye na watoto wake,'Mtoto wa mwangosi ukikua usisahau kuwatafuta watoto wa Kamanda Kamuhanda,Yeye ndio aliesababisha baba yako afe'
 
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake aliwahi kusema kuwa, “ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne ambavyo ni watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Watanzania kila mtu mahali pake, tunahitaji kuwa na siasa safi yenye kujenga ustawi, tija, mshikamano, amani, maendeleo na afya kwa taifa letu”.
Mh! hapo kwenye hitimisho kwa serikali ya CCM imepavuruga kabisa
1. Watu - watu tupo lakini hatuthaminiwi
2. Ardhi - Ipo tena eneo ni kubwa sana lakini maeneo yote muhimu kwa ajili ya kuliendeleza Taifa hili yanamilikiwa na watu wachache ambao ni wageni na kwa wazawa ni wale Mafisadi
3. Siasa safi Hapo pia ni utata kama ndani ya CCM ambacho kinatakiwa kiwe chama cha mfano kila kukicha tunasikia malalamiko Rushwa na tunashuhudia ngumi na kuchapana kila siku
4. Uongozi Bora - Mh! hapa kazi ipo ndiyo chanzo cha haya yote yanayotokea ni pale baba unapokuwa dhaifu unategemea familia itakuwa imara?
 
wakuu ripoti ile imeandikwa kwa maelekezo makubwa kama kwaya iliyokaririshwa sauti soprano,bass,tenor,na pitch ya muziki na wakaifanyia mazoezi ili kauli zifanane na maneno ambayo waheshimiwa wamesharopoka hadharani kabla ya ripoti kutoka.Sasa nasoma hii ya MCT nione.Hii ya serikali ni sawa na dissertation ya kupatia shahada VYUO VIKUU KAMA COMMONWEALTH OPEN UNIVERSITY mmoja wao alivyosomea!
 
Back
Top Bottom