WOWOWO
JF-Expert Member
- Aug 3, 2011
- 599
- 457
Nimeisoma kwa makini ripoti hii ya kifo cha Mwangosi hakika imeniliza, imeniuma sana. Hakika pamoja na machozi yangu nukuu hizi zimenichefua sana.
Baada ya kuvunjwa kwa ghasia,Mwangosi alikimbilia walipo polisi na kitu kama bomu kikarushwa na kundi la watu waliokuwa wanakimbia na kumlipua Mwangosi Gazeti la Habari Leo
Kilichosababisha kifo cha Mwangosi ni kitu kilichorushwa na kundi la watu.Polisi wanachunguza Gazeti la Mwananchi
Hii ni amri na polisi hairuhusu maswali zaidi kuhusu suala hili RPC Kamuhanda
Nukuu hizi katika ripoti hii zimenikera sana sana. Magazeti ya Mwananchi na Habari Leo yamemsaliti Mwangosi. Inakera sana. Inakuaje chombo cha habari tena chenye ripota kwenye eneo la tukio kije na nukuu kama hii iliyojaa utumbo na uzandiki? Yaani mazingira ya tukio yanavyoelezwa na ripoti hii gazeti linawezaje kuja na propaganda ya kipuuzi kabisa kuwa Mwangosi aliuawa kwa kutupiwa kitu kizito?
Lakini nukuu hiyo ya Kamuhanda ndiyo ujinga mkuu katika ripoti hii. Kwa mentality hizi za Jeshi la Polisi hakika tutegemee maafa makubwa zaidi.
Hakika MCT wamefanya kazi kubwa inayostahili pongezi na wameweka kumbukumbu sahihihi ingawa Jeshi la Polisi lililozoea kuua raia badala ya kuwalinda halitakoma kufanaya hivyo as far as limeweka weledi wote pembeni na kukubali kutumika kisiasa.
Madamu kasi ya CCM kudondoka ni kubwa kadri upinzani unavyozidi kuijitanua tutegemee msuguano na vifo vingine vingi maana Jeshi la Polisi sasa limebadilika na kuwa Idara ya Ulinzi ndani ya CCM na limejikabidhi jukumu kubwa la kudhibiti wapinzani.Tusubili tuone ingawa daina huwezi kushindana na umma unaotaka mabadiliko maana hakika umechoka.
Ripoti hii imeniliza, imeniuma sana. Siwezi kuendelea zaidi. R.I.P Mwangosi.