Ripoti ya Kifo cha Mwangosi

Asante kwa ripoti mkuu. Hii ni ile ya MCT na imejaribu kuweka mambo hadharani kiasi japo haikuweza kutaja moja kwa moja jina la yule askari aliyehusika na majina ya wale wengine wote walioshiriki kumuua Mwangosi. Anyway, tusubiri tuone mwisho wake na ile ya Nchimbi sijui inatoka lini!! Ila spelling error ni nyingi sana kwa ile ya Kiswahili ambayo tayari nimeshaisoma yote.
 
Hakika ni aibu kubwa kwa nchi hasa viongozi wa ngazi za juu polisi kupanga kuua, wana JF ripoti nimeisoma na kuelewa kabisa hongera tume iliyochunguza haya mauaji, sasa watz wamejuwa nani mbayawao ni hawa policccm na viongozi wao.

Mimi kama mtz naomba hawa polisi saba pamoja yule aliyetolewa kondoo wa kafara wote washughulikiwe. Kamwe tusiruhusu wahuni watuongoze.

Kamuhanda na wenzaka wawajibishwe hasa wale waliokuwa makao makuu ya polisi ambao wamejaribu kuficha ukweli.
 
Kama hiyo ripoti haijalaaani mauaji ya Mwangosi, itakuwa ni useless
Mkuu hiyo ni prediction tu.
Ukiisoma utaelewa kilichomo humo.

Tanzania bwana! sasa kwanini report ni ya kiingereza?
Zipo ripoti mbili ambapo moja ni kiswahili na nyingine ya kiingereza.

Kuliko niisome bora nichukue Novel nisome au niende jukwaa la MMU nikakutane na wakina Smile
Umeisoma?
Au ndiyo tuamini kwamba documents zinawanyima fursa Watanzania kuelewa zaidi? MCT wamefunguka sana kwenye hii ripoti. Naamini kamati ile nyingine inaweza kuja na maswali mengi zaidi. Lakini hii imevuka viunzi vingi vya kiutafiti
 
Sijaelewa bado. Sijaona conclusion na suggestions labda alieelewa anisaidie.
 
Sijaelewa bado. Sijaona conclusion na suggestions labda alieelewa anisaidie.

Hata mimi sijao ona mapendekezo kwamba serikal ifanye nn wameacha njia panda serijali hii ya ajabu sana ila kwa mwelekeo huo uenda nchi akatoa maamzi
 
They have tried kwa kweli! Though watanzania kwenye kuweka mambo wazi bado sanaaaaa!
 
Wakuu ripoti ya Mwangosi (MCT) imeshatolewa.
Fungua atachmenti hapo chini.
Nimeisoma inaumiza!! hata kipindi cha ubaguzi Africa Kusini hali haikuwa hivi. Eti Kamuhanda anapiga honi halafu uhai wa wa mtu unatoweka!! Who is Kamuhanda for heavens' sake! is this beast dwelling arround us? Kweli TZ ni NCHI ya ajabu! Eti anaombwa atoe amri ya kuacha mauaji yasiendelee anajifungia kwenye gari ya kiyoyozi nilichomnunulia mimi na wewe kwa kodi zetu! Eti polisi ninaowalipa mshahara kwa kodi yangu wanapiga na kuua bila huruma!! DAMN IT DAMN IT!! Do we have a country here?! NI kweli wewe JK ni dhaifu!! huna mamlaka wala huna nchi!!
Ninaomba ban!!
 
Ripoti nzuri with illustration ya picha - ila INAUMIZA SANA MOYO UNAPOSOMA - sasa nimeelewa ilivyo hatari kuuza silaha dukani kama njugu - kweli vitu kama hivi vinaweza kukupelekea ................................... [NAOGOPA BUN] ngoja niishie hapa.

Otherwise - nijulisheni hivi huyo Afande Kamuhanda bado yuko kazini???? mh! bora YESU ARUDI UPESI TWENDE MBINGUNI - THIS WORLD IS SO SCARY:shock::shock::shock::shock::shock::shock:
 
Naomba kujuzwa hili.. Yule RPC Kamuhanda bado yuko na wadhifa wake hapo Iringa..?
 
Mkuu mtoa uzi ahsante sana. Report hiko sawa to my eyes lakini. Nafijiri pia repoti itasadia kulinganishwa na repoti zitakazofuata. Nimeipenda na nasubili uwajibijakaji kwa waliohusika.
 
Loooooo, nimesoma hii riport, hawa "Zaidi ya Polisi saba chini ya uongozi wa RPC Michael Kamuhanda" walimuua mwangosi wote wafungwe maisha, waziri wa ulinzi ijiuzuru mara moja na "OCD Asseri Mwampamba alilalama kwauchungu kutokana na mlipuko wa bomu la machozi akisema: "Sasa,
umefanya nini " Hii ina maana alimzidi sana RPC akili, angalau huyu angeweza kuwa RPC sio majambaazi, kupewa vyeo vikubwa namna hii.

Nalaani sana kitendo cha kuwatumia Ma RPC kisiasa na kuwaharibu bongo zao.
 
Report imekaa vizuri na inaonesha wazi kuwa police ndo main KILLERS,So what next...................
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom