Ripoti maalum ya sekta zinazoongoza kwa ufujaji na matumizi mabovu ya pesa za vijana wa Kitanzania

Ripoti maalum ya sekta zinazoongoza kwa ufujaji na matumizi mabovu ya pesa za vijana wa Kitanzania

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,451
1)Idara ya uzinzi

Ni sekta namba Moja Ambayo ,imeonekana Kuwa na matumizi mabovu mno ya Fedha ,vijana wamekengeuka ,Wanahonga sana michepuko na girlfriends ukilinganisha na bei Elekezi.

Kijana anaamua kujilipua kuingia mahusiano yenye gharama kubwa sana kwasababu ya kupagawishwa na shepu na sura, jambo linalo mlazim kutumia Fedha nyingi mno.

Hata wale wanainunua dada poa nao hawajasalimika, kuwapata angalau wenye quality ni kuanzia elf 15 na kupata lodge utagharamika zaidi ya 20.

Hata wanaojichukulia sheria mkononi hawajasalimika, wanaingia gharama ya kununua mabando kila siku ya kuchekia videos au picha pamoja na gharama za ziada za vifaa kama mafuta, toys na sabuni.

2)Sekta ya Unywaji Pombe

Sekta Hii imebainika kua ya pili Kwa Ufisadi mkubwa na Matumizi mabovu ya Fedha, Mtu ametoka zake Nyumbani kafika bar ,Badala anywe Bia mbili na kuondoka ,kijana anaanza kununulia madada poa na washkaji, Kama alipaswa atumie bill ya Ef 10k Akiwa pekeyake , analazimika kutumia sio chini ya Elf 50k mpk 100k Jambo linalo pelekea kuharibu uchumi.

3)Sekta ya Mavazi

Sekta Hii imeonekana kua ya Tatu Katika Utumiaji wa Fedha nyingi ,na Ufisadi mkubwa, kijana unaitaguta badala ya kununua nguo unazozimudu, Anakwenda maduka makubwa Kununua T-shert Moja ya Elf 25k ,cadet 40k, n.k..

Sekta ya viwalo imegharimu sana uchumi wa vijana,

4)Sekta ya Ulaji Chakula

Hii imekua Sekta ya nne Kwa Ufisadi na Matumizi mabovu ya Fedha ,Vijana Wanashindwa kujishikiria Asubuhi TU wale hata andazi na chai, anakimbilia Mgahawani kula Supu na chapati

Imebainika kuna vijaa wanaojitafuta wanatumia hadi elf 10 na zaidi kwa Siku, Haya nimatumizi mabovu ya Fedha na niuhujumu uchumi.

5)Sekta ya vifurushi.

Sekta Hii imekua ya nne Kwa matumizi mabovu ya Fedha ,vijana wamebainika kutumia Fedha nyingi mno Kwa kugharamia vifurushi vya data.

Kijana kila siku anatumia Bando la Buku 2 na zaidi kuangalia tiktok, insta, kudownload na kustream

6)Sekta ya Kamali

Get rich quich hizi zimefanya vijana wengi sana waendelee kubaki nyuma, nilikuwa naichukulia kamali po ani mpaka siku moja nilipomuona kijana wa miaka kama 30 hivi katoka kwenye kibarua cha tangu asubuhi hadi jioni kalipwa elf 20, kabana buku 3 kama ya chakula, nyingine yote ikaishia kwenye kamali na kipigo juu. Mwengine nilimshuhudia kaveti savings zake kama laki 7 kwenye mpira ikaenda yote na kilio juu. Vijana wengi wana asira za kurudisha pesa walizopoteza kwenye kamari lakini hujikuta wakizika zaidi pesa zao
 
Back
Top Bottom