Ripoti Maalum: Kupotea kwa Ben Saanane

Ripoti Maalum: Kupotea kwa Ben Saanane

JMP Mchungu

Member
Joined
Jun 30, 2015
Posts
49
Reaction score
127
Dar es Salaam. Ni kimya kimetawala Kitongoji cha Hiti kilichojificha katikati ya mashamba ya migomba, kahawa na miti mikubwa. Ni katika miteremko ya Mlima Kilimanjaro wilayani Rombo ndiko kinakopatikana Kijiji cha Mrere. Sauti pekee unayosikika ni ya upepo unaovuma katika migomba, sauti za wanyama na watoto wanaocheza maeneo ya karibu. Renatha Saanane, 54, mama mzazi wa Ben Saanane, anaendelea na shughuli zake za kila siku za nyumbani, lakini inambidi asimame na kumkaribisha mgeni ambaye ujio wake ametaarifiwa dakika chache zilizopita. Uso wake hauna tabasamu ya kawaida anayopaswa kuwa nayo kwa wageni. Uchungu alioubeba moyoni mwake kwa zaidi ya miezi tisa baada ya kutoweka kwa mtoto wake wa kwanza, Ben Saanane, unasomeka waziwazi usoni kwake.

“Sijui kama ameuawa, ametekwa au anashikiliwa na vyombo vya ulizi na usalama. Hili naiachia serikali,” anasema Bi Saanane. Baadaye machozi yanachuruzika kwa muda lakini anajikaza na anajipa nguvu na kuendelea kujadili fumbo la kupotea mwanaye. Mara ya mwisho kuongea na mwanaye ilikuwa ni Novemba 11 mwaka jana, siku tatu tu kabla Ben hajatoweka. Waliongea masuala mbalimbali, ikiwamo maandalizi ya harusi ya ndugu yao aishiye Dodoma. “Hayo ndiyo mawasiliano yangu ya mwisho na yeye,” anasema, na kuongeza kuwa kwa kawaida hakuwahi kuingiwa hofu kuhusu ukimya wa muda mrefu wa mwanaye, ikizingatiwa kuwa nafasi yake kama msaidizi wa karibu wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ilimfanya awe na shughuli nyingi.

Kwa siku kadhaa zilizofuata baada ya kuongea na mwanaye kwa simu kwa mara ya mwisho, Bi Saanane aliendelea kumpigia Ben mara kwa mara lakini hakufanikiwa kumpata. Alichukulia hali hiyo kama jambo la kawaida. Hata hivyo, anasema, kwa mshangao alijua baadaye kuwa hata mdogo wa Ben aitwaye Erasto na dada yake Agripina ambao pia wanaishi Dar es Salaam, pia hawakuweza kumpata kwa njia ya simu licha ya kumpigia mara kwa mara. “Hapo wote tukaanza kuwa na wasiwasi lakini wengine wakaamini anaweza kuwa amesafiri nje ya nchi au maeneo yasiyofikiwa na mtandao wa simu ukizingatia uanaharakati wake wa kisiasa,” alisema Renatha.

“Bado hatukuweza kupata jibu, lakini wasiwasi wetu ulizidi baada ya suala la kutoonekana Ben liliripotiwia polisi Dar es Salaam na baadaye kuanza kuandikwa magazetini.” Mama Saanane hafichi juhudi zilizofanywa na familia yake kumtafuta mwanaye baada ya taarifa za vyombo vya habari kujirudiarudia kwamba anaweza kuwa ametekwa. Mara ya mwisho mwanasiasa huyo kijana wa upinzani kufika kijijini kwao, kwa mujibu wa mama yake, ilikuwa kati ya Agosti au Septemba mwaka jana alipokwenda kumzika bibi yake. Suala la kupotea kwa Ben halikuchukuliwa kwa urahisi katika kijiji chake cha Mrere kilicho Kata ya Mashati, takriban kilomita 60 kutoka Moshi na Wilaya ya Rombo kwa jumla. Wananchi wa kawaida katika eneo hilo wana ufahamu wa kutosha kuhusu hali ya kisiasa nchini na mara nyingi viongozi wa kisiasa wamejikuta wakikamatwa na kushtakiwa wakituhumiwa kutotii mamlaka, uchochezi na mambo kama hayo.

Ben mwenyewe hakuwa mgeni na siasa za Rombo. Wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aligombea ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema na kushika nafasi ya pili baada ya kushindwa na mbunge wa sasa, Joseph Selasini (Chadema) katika kura za maoni. “Anajulikana na watu wengi kwa sababu alikuwa machachari wakati wa kampeni,” anasema mama yake, akiongeza kuwa kutoweka kwake kuliwagusa watu wengi pia. Baba yake, Focus Saanane, 63, anasema anaumizwa na kutoweka kwa mtoto wake lakini anainyooshea Serikali kidole cha lawama kwa jinsi walivyoshughulikia suala hilo.

“Tunaiachia Serikali kila kitu. Taarifa kutoka mamlaka hazijawahi kuwa za kuaminika,” anasema katika mahojiano mjini Moshi anakofanya biashara. Anaonyesha kuwa familia yake inazidi kupoteza matumaini ukizingatia juhudi walizofanya bila ya mafanikio za kumtafuta kijana wao, ambaye licha shughuli zake ndani ya Chadema alikuwa pia akisomea shahada ya uzamivu ya uchumi. Mzee Saanane anasema japokuwa Ben alilelewa na kukua kama mtu mwenye uhuru wa kwenda popote alipotaka, anazidi kukerwa na taarifa zinazokinzana kuhusu kutoweka kwake. “Hatujui kama yuko hai au la. Mara ya mwisho kukutana naye ilikuwa wakati wa mazishi ya bibi yake,” anasema. ”Na ilikuwa mara ya mwisho kusikia kuhusu mwanangu.

Familia inaumia sana lakini hatuna la kufanya. Mama yake ana uchungu mkubwa kijijini. Sisi kama familia kubwa tumejaribu sana kumsaka lakini hakuna mafanikio Mzee Saanane anasema namba ya simu ya Ben ya Vodacoma imezuiwa na hawezi kujua mwanaye aliwasiliana na nani mara ya mwisho kabla ya kutoweka. Suala la kupotea kwake liliripotiwa kituo cha polisi Tabata jijini Dar es Salaam. Anaisihi Serikali isaidie katika kumtafuta mtoto wake na kuwaondolea wasiwasi wa wapi alipo na usalama wake, akisema hata maofisa wa Chadema hawajatoa msaada wa kutosha katika kumtafuta
mwanaye kama wanavyoonekana pia kuchanganyikiwa.

Godbless Lema, mbunge wa Arusha Mjini ni kiongozi pekee wa juu wa Chadema aliyewahi kumtembelea Mzee Saanane nyumbani kwake Moshi kumtuliza na kujaribu kutafuta namna ya kulifumbua fumbo hilo, anasema mzee huyo.
 
Hapa ndipo uwa namwelewa Joyce Kiria kwanini alikuwa hataki mumewe aandamane kipindi kile...
 
""Godbless Lema, mbunge wa Arusha Mjini ni kiongozi pekee wa juu wa Chadema aliyewahi kumtembelea Mzee Saanane nyumbani kwake Moshi kumtuliza na kujaribu kutafuta namna ya kulifumbua fumbo hilo, anasema mzee huyo.""

Seriously kama hii statement ya huyu mzee ni kweli, Viongozi wa Chadema, wa juu zaidi ya Lema, sauti zenu zinahitajika juu ya hili.
 
Inauma kama Mzazi Mwanao kapotea kimazingara hivo
 
""Godbless Lema, mbunge wa Arusha Mjini ni kiongozi pekee wa juu wa Chadema aliyewahi kumtembelea Mzee Saanane nyumbani kwake Moshi kumtuliza na kujaribu kutafuta namna ya kulifumbua fumbo hilo, anasema mzee huyo.""

Seriously kama hii statement ya huyu mzee ni kweli, Viongozi wa Chadema, wa juu zaidi ya Lema, sauti zenu zinahitajika juu ya hili.
Aulizwe vizuri mwenyekiti anaweza akawa anajua ben alipo maana si kwa rohombaya hivo
 
Makonda akisema anajiamini wanaume wa Dar mnashangaa!
Zirro kapandishwa na Makonda mpaka sasa
 
Godbless Lema, mbunge wa Arusha Mjini ni kiongozi pekee wa juu wa Chadema aliyewahi kumtembelea Mzee Saanane nyumbani kwake Moshi kumtuliza na kujaribu kutafuta namna ya kulifumbua fumbo hilo, anasema mzee huyo.
All animals are equal, but some animals are more equal than others.
 
Seriously hii siasa yetu inapoelekea sio kuzuri kabisa, somebody must do something BTW
Pray for Ben, Pray for Tz
 
Aulizwe vizuri mwenyekiti anaweza akawa anajua ben alipo maana si kwa rohombaya hivo
huna akili, unajua ni kwanini hawataki kutoa mawasiliano ya mwisho ya saanane? unafikiri ni msg za nani zilimtishia maisha siku chache kabla ya kupotea? unafikiri ni kwanini hawaruhusu wachunguzi toka nje?

we mdada utakua mjamzito wewe
 
Hawa watu waliousika kumpiga risasi ben inabidi washitakiwe kwa makosa ya ukiukaji wa haki za binadamu,kama mtumishi wetu chahali kathibitisha kwamba alipigwa risasi kwanii wasichunguzwe hao watu waliosika tukianza na BASHITE?

Kwanini BASHITE alikuwa anataka kukutana na BEN SAA8 na walikuwa wakutane siku mbili before Kupotea?

Katika tukio la kupigwa risasi lissu kwanini ushahidi wa kimazingira unaonyesha ushiriki wa BASHITE?

Huyu BASHITE sio wa Kuachwa hivi hivi inatakiwa wadau wanaopenda haki wamshitaki hata ICC maana matendo anayofanya ni zaidi ya mauaji ya kivita.
 
Mtu huyu mwenye rekodi ya mwanamkakati wa Pm-7 alizaliwa 13/12/1983
Mkuu Tutashinda, kauli huumba, na lisemwalo lipo kama halipo, linakuja!.
Angalia heading ya bandiko lako hili, na tarehe ya bandiko hili, halafu angalia nini kilikuja kutokea kwa Ben Saanane.

Wana jf tuanze kujifunza kuchunga kauli zetu, kauli nyingine zinaumba, ukisema mwisho wa fulani, bila hata wewe kumaanisha ni mwisho kwa kutoweka, kwenye heading ulisema

"ben-saanane-mwisho-wake-umefika-rasmi",
Wewe bila kujua kuwa kauli hii ina powers, baada ya kutolewa bila kuwekewa any caveat ya mwisho wa nini, then powers zimeanza ku act kuutengeneza mwisho wa Ben.

Maadam kwenye bandiko hili, ulidhamiria mwisho wa Ben Saanane ni mwisho kwenye uchaguzi wa Bavicha, then the headline yako should have said so, " Ben Saanane Mwisho Wake Kugombea Bavicha Umefika Rasmi " ili zile powers za kauli yako iwe limited kwa Bavicha tuu, kitendo cha kutoa open ended statements bila kinga, ndicho kimepelekea kuchangia kufika mwisho kwa Ben Saanane.

Kwenye bandiko hili mimi pia nilichangia
Japo mimi sio Chadema na sina chama, ila tukubali tukatae, ukiondoa mapungufu yake ya kibinaadamu, (hakuna binaadamu mkamilifu), Ben Saanane, is the type of leaders BAVICHA, should have had long ago, and had it been, he had been there, BAVICHA would not have been the same again, it would have been far far ahead, by now CCM ingekuwa bize kukusanya kusanya kilicho chake kupisha njia!.

Thanks.
Pasco.
From no where, jana nimetokea tuu kumkumbuka Ben Saanane, sikujua kwanini, hivyo nilipoamka nikaanza kupitia baadhi ya mabandiko humu ndipo nikakutana na bandiko hili la 2014, nilipolisoma ndipo nikagundua kumbe jana ndio tarehe ya kuzaliwa ya Ben Saanane.
Happy Birthday Ben Saanane.
P
 
Dar es Salaam. Ni kimya kimetawala Kitongoji cha Hiti kilichojificha katikati ya mashamba ya migomba, kahawa na miti mikubwa. Ni katika miteremko ya Mlima Kilimanjaro wilayani Rombo ndiko kinakopatikana Kijiji cha Mrere. Sauti pekee unayosikika ni ya upepo unaovuma katika migomba, sauti za wanyama na watoto wanaocheza maeneo ya karibu. Renatha Saanane, 54, mama mzazi wa Ben Saanane, anaendelea na shughuli zake za kila siku za nyumbani, lakini inambidi asimame na kumkaribisha mgeni ambaye ujio wake ametaarifiwa dakika chache zilizopita. Uso wake hauna tabasamu ya kawaida anayopaswa kuwa nayo kwa wageni. Uchungu alioubeba moyoni mwake kwa zaidi ya miezi tisa baada ya kutoweka kwa mtoto wake wa kwanza, Ben Saanane, unasomeka waziwazi usoni kwake.

“Sijui kama ameuawa, ametekwa au anashikiliwa na vyombo vya ulizi na usalama. Hili naiachia serikali,” anasema Bi Saanane. Baadaye machozi yanachuruzika kwa muda lakini anajikaza na anajipa nguvu na kuendelea kujadili fumbo la kupotea mwanaye. Mara ya mwisho kuongea na mwanaye ilikuwa ni Novemba 11 mwaka jana, siku tatu tu kabla Ben hajatoweka. Waliongea masuala mbalimbali, ikiwamo maandalizi ya harusi ya ndugu yao aishiye Dodoma. “Hayo ndiyo mawasiliano yangu ya mwisho na yeye,” anasema, na kuongeza kuwa kwa kawaida hakuwahi kuingiwa hofu kuhusu ukimya wa muda mrefu wa mwanaye, ikizingatiwa kuwa nafasi yake kama msaidizi wa karibu wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ilimfanya awe na shughuli nyingi.

Kwa siku kadhaa zilizofuata baada ya kuongea na mwanaye kwa simu kwa mara ya mwisho, Bi Saanane aliendelea kumpigia Ben mara kwa mara lakini hakufanikiwa kumpata. Alichukulia hali hiyo kama jambo la kawaida. Hata hivyo, anasema, kwa mshangao alijua baadaye kuwa hata mdogo wa Ben aitwaye Erasto na dada yake Agripina ambao pia wanaishi Dar es Salaam, pia hawakuweza kumpata kwa njia ya simu licha ya kumpigia mara kwa mara. “Hapo wote tukaanza kuwa na wasiwasi lakini wengine wakaamini anaweza kuwa amesafiri nje ya nchi au maeneo yasiyofikiwa na mtandao wa simu ukizingatia uanaharakati wake wa kisiasa,” alisema Renatha.

“Bado hatukuweza kupata jibu, lakini wasiwasi wetu ulizidi baada ya suala la kutoonekana Ben liliripotiwia polisi Dar es Salaam na baadaye kuanza kuandikwa magazetini.” Mama Saanane hafichi juhudi zilizofanywa na familia yake kumtafuta mwanaye baada ya taarifa za vyombo vya habari kujirudiarudia kwamba anaweza kuwa ametekwa. Mara ya mwisho mwanasiasa huyo kijana wa upinzani kufika kijijini kwao, kwa mujibu wa mama yake, ilikuwa kati ya Agosti au Septemba mwaka jana alipokwenda kumzika bibi yake. Suala la kupotea kwa Ben halikuchukuliwa kwa urahisi katika kijiji chake cha Mrere kilicho Kata ya Mashati, takriban kilomita 60 kutoka Moshi na Wilaya ya Rombo kwa jumla. Wananchi wa kawaida katika eneo hilo wana ufahamu wa kutosha kuhusu hali ya kisiasa nchini na mara nyingi viongozi wa kisiasa wamejikuta wakikamatwa na kushtakiwa wakituhumiwa kutotii mamlaka, uchochezi na mambo kama hayo.

Ben mwenyewe hakuwa mgeni na siasa za Rombo. Wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aligombea ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema na kushika nafasi ya pili baada ya kushindwa na mbunge wa sasa, Joseph Selasini (Chadema) katika kura za maoni. “Anajulikana na watu wengi kwa sababu alikuwa machachari wakati wa kampeni,” anasema mama yake, akiongeza kuwa kutoweka kwake kuliwagusa watu wengi pia. Baba yake, Focus Saanane, 63, anasema anaumizwa na kutoweka kwa mtoto wake lakini anainyooshea Serikali kidole cha lawama kwa jinsi walivyoshughulikia suala hilo.

“Tunaiachia Serikali kila kitu. Taarifa kutoka mamlaka hazijawahi kuwa za kuaminika,” anasema katika mahojiano mjini Moshi anakofanya biashara. Anaonyesha kuwa familia yake inazidi kupoteza matumaini ukizingatia juhudi walizofanya bila ya mafanikio za kumtafuta kijana wao, ambaye licha shughuli zake ndani ya Chadema alikuwa pia akisomea shahada ya uzamivu ya uchumi. Mzee Saanane anasema japokuwa Ben alilelewa na kukua kama mtu mwenye uhuru wa kwenda popote alipotaka, anazidi kukerwa na taarifa zinazokinzana kuhusu kutoweka kwake. “Hatujui kama yuko hai au la. Mara ya mwisho kukutana naye ilikuwa wakati wa mazishi ya bibi yake,” anasema. ”Na ilikuwa mara ya mwisho kusikia kuhusu mwanangu.

Familia inaumia sana lakini hatuna la kufanya. Mama yake ana uchungu mkubwa kijijini. Sisi kama familia kubwa tumejaribu sana kumsaka lakini hakuna mafanikio Mzee Saanane anasema namba ya simu ya Ben ya Vodacoma imezuiwa na hawezi kujua mwanaye aliwasiliana na nani mara ya mwisho kabla ya kutoweka. Suala la kupotea kwake liliripotiwa kituo cha polisi Tabata jijini Dar es Salaam. Anaisihi Serikali isaidie katika kumtafuta mtoto wake na kuwaondolea wasiwasi wa wapi alipo na usalama wake, akisema hata maofisa wa Chadema hawajatoa msaada wa kutosha katika kumtafuta
mwanaye kama wanavyoonekana pia kuchanganyikiwa.

Godbless Lema, mbunge wa Arusha Mjini ni kiongozi pekee wa juu wa Chadema aliyewahi kumtembelea Mzee Saanane nyumbani kwake Moshi kumtuliza na kujaribu kutafuta namna ya kulifumbua fumbo hilo, anasema mzee huyo.
Bandiko hili la Nov. 2017 halijafikisha michango 20!.
RIP Ben Saanane!.
P
 
Back
Top Bottom