By pcman
Hawa jamaa sijui kwa nini huwakuja android?!
Sent from my LT26i using Tapatalk 2
mkuu nokia amefanya maamuzi ya busara sana kwenda windows phone ila kwa akili ya haraka unaweza ukaona kama ni mistake.
Android kuna king mmoja tu samsung basi peke yake ndio anafaidi.
-htc kila siku faida zinashuka anatoa simu kali hamna anaenunua
-lg ana biashara nyingi ila part inayomuingizia hasara kubwa ni simu
-sony ameamua kuacha kutoa simu ndogo now anatoa flagship tu profit margin ndogo
nokia ameenda wp na sasa yeye ndo amekua king. Tofauti ya wp na android ni kwamba kwenye windows phone kila kitu anafanya microsoft wewe oem una deal na hardware tu. Wakati android inabidi uimprove na software.
Kutokana na nokia kutodeal na software amefanya improvement kubwa sanaaaaaa. Vitu hivi nokia kavofanya 2012
-camera ya 41mp
-lens inayostahamili mitikisiko
-wireless charging
-best night shot
-screen inayogusika hadi na gloves
-mashine ya 3d cover
-na vingine vingi
angalia na mapato 2012
-january hadi march- nokia hasara dola 1.7 billion
-april hadi june- hasara dola 1 billion
-july hadi september- hasara milion 700 dola
-october hadi december- faida milion 500
so mkuu tumpe nokia muda mengi yanakuja. Na ujio wa windows blue nokia atazidi kupaa