RIP: Shaaban Mloo is no more.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RIP: Shaaban Mloo is no more..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 15, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mwananchi

  MWANASIASA mashuhuri na muasisi wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaaban Khamis Mloo, amefariki dunia katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja jana ambako alikuwa akitibiwa maradhi ya moyo.



  Mloo alifariki dunia saa 2:00 asubuhi ambapo katika kipndi cha siku tatu alikuwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) alipokuwa akipata matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.


  Mloo alianza kuugua muda mrefu lakini hali yake ilikuwa haitabiriki na mara kwa mara alijikuta akilazimika kupelekwa hospitali.



  Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha CUF, Salim Rashid Bimani amethibitisha kutokea kwa kifo hicho akifafanua kuwa marahemu Mloo alizikwa jana Shambani kwake katika kijiji cha Mfenesini, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.



  “Marehemu Mloo mwishoni mwaka jana, alilazwa ICU katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam kutokana na kusumbuliwa na maradhi hayo hayo ya moyo.


  Alipata nafuu, lakini mwanzoni mwa wiki hii akazidiwa tena na ikabidi apelekwe Hospitali ya Mnazi Mmoja na kulazwa ICU pia,” alisema Bimani katika hali ambayo ilionyesha kuwa ana majonzi.



  Alisema wanachama wa CUF wanatoa mkono wa pole kwa Mwenyekiti wa Chama cha CUF na familia ya marehemu, Mzee Mloo na wananchi wote wa Tanzania kwani kifo chake kitakuwa kimeacha pengo kubwa ndani ya chama hicho cha upinzani.


  Alimuelezea Mloo kuwa alijitolea wakati wote kukitumikia chama chake cha CUF na changamoto zake zilikiwezesha kuwa na nguvu visiwani hapa.



  Alisema licha ya kustaafu, Mzee Mloo alikuwa mstari wa mbele katika kutoa ushauri wa chama hicho na kukosoa kila alipobaini kuwa mwelekeo wa chama unakwenda isivyo.


  Katika uhai wake, Mzee Mloo aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali na katika Chama cha Mapinduzi (CCM), ikiwa ni pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.



  Mzee Mloo alikuwa ni miongoni mwa Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar, kabla ya Mapinduzi na baada ya kuanza kwa Baraza la Wawakilishi, alikuwa Mjumbe wa Baraza hilo kwa vipndi kadhaa.



  Mwanasiasa huyo mkongwe wa Zanzibar, akiwa na wenzake aliongoza harakati za kudai mageuzi ya kisiasa wakati huo akiwa na Ali Haji Pandu aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Hayati Maulid Makame, na Soud Yusuf Mgeni.


  Kwa pamoja waliunda Kamati Huru ya Mageuzi ya Kisiasa (Kamahuru) kwa lengo la kuishinikiza SMZ ikubali mabadiliko ya kisiasa na kufuta mfumo wa chama kushika hatamu.

  ?Hata hivyo, Chama hicho baadaye kiliungana na Chama cha Wananchi Tanzania (CCWT) kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wake, James Mapalala na kuzaliwa CUF ambapo hadi anamaliza uhai wake, Mzee Mloo alikuwa mwanachama wa chama hicho na kiongozi analiyeheshimika.



  Mwanasiasa huyo maarufu Zanzibar kwa jina la “Kuchi”, alijiuzulu mambo ya siasa CUF mwaka 2002 na kubakia kama mwanachama wa kawaida na mshauri wa ngazi za juu wa chama hicho.



  Mara baada ya kuanzishwa kwa Chama cha CUF, Mloo alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Chama hicho kabla ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF.


  Marehemu Mloo ni miongoni mwa wanachama waliofukuzwa na CCM mwaka 1988 baada ya kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar.



  Wengine waliofukuzwa ni Maalim Seif Shariff Hamad, Ali Haji Pandu, Khatib Hassan, Hamad Rashid Mohamed, Soud Yussuf Mgeni, Masoud Omar, Maulid Makame na Machano Khamis Ali.



  Bimani alisema marehemu Mloo ataendelea kukumbukwa na CUF kuwa ni mfano wa mwanamageuzi asiyeyumba ambaye kwa wakati wote alitetea haki na usawa mbele ya jamii huku akiwa anajali sana kazi zake katika chama hicho.


  Naye, Patricia Kimelemeta anaripoti kuwa Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba alisema kuwa Mzee Mloo alikitumikia chama hicho zaidi ya miaka nane, tangu mwaka 1992 hadi 2000 alipochukua nafasi ya umakamo mwenyekiti hadi alipostaafu mwaka 2004.



  Taarifa hiyo ilieleza kuwa, CUF inamtambua Mzee Mloo sio tu kama kiongozi mstaafu wa Chama, bali mwasisi, mwanzilishi na mwanachama imara na shupavu katika siku zote za uhai wake.


  "Atakumbukwa daima ndani na nje ya nchi kama mjuzi wa siasa za Zanzibar na za Tanzania kwa ujumla, mchapakazi na mtu aliyekuwa na ujasiri," alisema Profesa Lipumba kupitia taarifa hiyo.


  Alifafanua kuwa kikao cha mwisho kuhudhuria ni mkutano mkuu wa nne wa CUF uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Februari 23 hadi 27 Februari, mwaka huu.


  Taarifa hiyo ilieleza kuwa, kabla ya kustaafu aliwaaga wajumbe wa mkutano mkuu huo, februari 2004 kwa kuwapatia waraka maalum ambao uliandikwa ulisema:



  “Nakuachieni Chama wajumbe wote wa mkutano mkuu huu wa leo, mukiwa na jukumu moja kubwa sana.


  "Ingawa sisi tunastaafu, lakini tutaangalia kwa macho mawili utendaji wenu katika kata, matawi, majimbo, wilaya na taifa. Nakuachieni Chama kilichokamilisha theluthi mbili ya mtandao wake katika mikoa 26 ya Tanzania.


  "CUF imeenea kila mkoa. Katika wilaya 130, CUF iko wilaya 117, katika vitongoji 38,000, CUF ina 20%, katika vijiji 11,600, CUF ina 15%. Mitaa yote 3,080, CUF ina 20%”,ilieleza sehemu ya waraka huo.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 15, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Rest In Peace
   
 3. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenyezimungu amweke mahali pema na atuletee viongozi watakaoiga au kuwa na mfano kama wake.
   
 4. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mmungu amhufirie madhabi yake na amuweke katika pepo karibu na yeye
  Amin
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Inna lillah wa inna ilayhi rajiuun, hakika sisi sote tunatoka kwa Muumba na kwake tutarejea.
  Mungu amlaze mahala pema peponi, Mzee Mloo, ambaye ameondoka wakati tukiwa bado tunasubiri mapambazuko na mawio ya haki ya kweli visiwani.
   
 6. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2009
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Mungu libarikiwe. Amen
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  RIP Mzee wetu Mloo!
   
 8. C

  Chuma JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sisi ni M/Mungu na kwake sote tutarejea!!!
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mzee wetu Mungu ailaze roho yako mahala pema peponi
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  R I P Mzee Mloo....
   
 11. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  R I P Shaaban Mloo. Poleni sana familia kwa msiba!
   
 12. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inna lillah wa inna ilayhi raji'oon
   
 13. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  RIP Shaaban Mloo, mpiganaji wa mabadiliko ya kweli Tanzania. Pole kwa ndugu na marafiki.
   
 14. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mbele yako nyuma yetu, Mungu atupe amani ktk hili zito kwa nchi yetu,Amen
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  RIP Mzee Mloo
   
 16. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  RIP Mzee Mloo... Ahsante mwanakijiji kwa taarifa hii...
   
 17. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Inna lillahi wa inna ilahi rajoon.
   
 18. N

  Nsesi JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2009
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 374
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  RIP Mzee Mloo, tutakukumbuka kwa mengi, ikiwemo busara, upendo na upole wako
   
 19. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Pole kwa ndugu, jamaa na marafiki.
   
 20. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  RIP Mzee Mloo
   
Loading...