Ridhwani: Kikwete hana ugomvi na Lowassa

Ridhwani: Kikwete hana ugomvi na Lowassa

Lisemalwo lipo kama halipo laja,ninavyo mfahamu mh lowasa ni mtu wa karibu sana na mh rais"jk mrisho kikwete

Nimewai kumsikia mh:edwadi lowasa akisema yeye na mh rais ni marafiki wakubwa sana na awajakutana mtaani tu,kwa maana hiyo ni watu waliokuwa karibu sana kabla hata jk hajachaguliwa kuwa rais, sasa swali ni kweli lowasa amekosana na jk?

Huku mitaani kuna habari za chini chini kuwa mh rais na lowasa awaelewani je ni kweli?
 
wakosane,wapatane,ufisadi unawasumbua ila hii ni movie, wanajuana kuindani na wana mipango ya pamoja
 
Usilolijuaa ni sawa na usiku wa giza ""urafiki wetu haujaanzia mitaani "" hyo kauli umeilewa inatoshaaa tu kukujibu
 
Rais Kikwete ni rafiki wa watanzani wote, haya ya kukosana na baadhi ya wananchi wake mnayatoa wapi kama siyo kukosa kazi.
 
Usilolijuaa ni sawa na usiku wa giza ""urafiki wetu haujaanzia mitaani "" hyo kauli umeilewa inatoshaaa tu kukujibu
Afadhali hata umemjibu, lakini pia anapaswa kujua JK ni rais wa watanzania wote, hana sababu yoyote ya kuwa na adui miongoni mwa watu ambao ana dhamana ya kuwatumikia.
 
Lowassa & kikwete wanajua urafiki wao ulipoanziaa toka miaka ya nyuma huko kama ni 60,70, 80, 90,
ila huwezi jua zaidi wakati hufanyi kazi ndani ya chama chao wala karibu yao pia umezaliwa juzi kama mimi
 
Rais Kikwete ni rafiki wa watanzani wote, haya ya kukosana na baadhi ya wananchi wake mnayatoa wapi kama siyo kukosa kazi.

Ndugu yanasemwa mitaani kwenye vijue vyetu,ndio maana tunauliza ili tupate majibu
 
Lisemalwo lipo kama halipo laja,ninavyo mfahamu mh lowasa ni mtu wa karibu sana na mh rais"jk mrisho kikwete

Nimewai kumsikia mh:edwadi lowasa akisema yeye na mh rais ni marafiki wakubwa sana na awajakutana mtaani tu,kwa maana hiyo ni watu waliokuwa karibu sana kabla hata jk hajachaguliwa kuwa rais, sasa swali ni kweli lowasa amekosana na jk?

Huku mitaani kuna habari za chini chini kuwa mh rais na lowasa awaelewani je ni kweli?

Nimewahi
Hawajakutana
Hawaelewani
Tukipe kiswahili heshima yake!
 
hawajawahi kukosana, Karibu sana Rais wetu mpya mheshimiwa Lowasa
 
kwa mtazamo wangu hawajakosana ila makundi ya urais yanataka kutuaminisha kuwa hao jamaa wawili hawapikiki chungu kimoja
 
Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete, amesema kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa na ugomvi na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, asingeshindwa kumshughulikia kwa kuwa anayo mamlaka na vyombo vyote vya ulinzi vipo chini yake.

Ridhiwan, ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete alisema hayo kupitia kipindi cha wanasiasa kinachorushwa na kituo cha televisheni ya StarTv.

Alisema Rais anayo mamlaka na kwamba, hawezi kuwa na ugomvi mkubwa na kiongozi akamshindwa na kutolea mfano namna viongozi wa nchi nyingine wanavyofanya kwa wapinzani wao wa kisiasa.

Mbunge huyo, ambaye hivi karibuni aliingia mgogoro na vyombo vya habari akiwatuhumu waandishi kuwa ni makanjanja na watu wanaoandika vitu vya ovyo ovyo, alisikika akisema kwamba, wanasiasa hao hawana ugomvi mkubwa badala yake unakuzwa na watu.

Alisema hayo baada ya kutakiwa kuzungumzia makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na uhusiano kati ya baba yake, Rais Kikwete na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Lowassa.

Aliongeza kuwa mambo hayo yanakuzwa na kimsingi hakuna ugomvi mkubwa kama inavyodaiwa na kukuzwa na watu wengi.

Alisema Lowassa na baba yake wamekuwa marafiki kwa miaka mingi na kwamba, watu wanajaribu kuwachonganisha wawili hao.

“Edward (Lowassa) akiwa na shida huwa anafika Ikulu na kufanya mazungumzo na Rais huo mgogoro unaosemwa unakuzwa na watu,” alisema Ridhiwan.

Akizungumza na NIPASHE kuhusu kauli hiyo aliyoitoa katika kipindi cha Star Tv, Ridhiwan alimsikiliza mwandishi swali lake lake na kisha akasema hawezi kujibu kwa kuwa alikuwa kwenye kikao.

“Nipo kwenye kikao, siwezi kujibu kitu. Ndiyo maana ulikuwa unapiga, nakata. Na ndiyo maana nimetoka nje kukusikiliza mara moja,” alisema Ridhiwan.

Ridhiwani alijibu madai hayo kwa kifupi, huku akikataa kutoa ufafanuzi wa kile alichoulizwa na kisha akakata simu.


Chanzo: Nipashe


Hana ugomvi naye kweli, Kwa kuwa wote Wana Juana. Mwizi hawezi mchukia mwizi mwenzie
 
Rizi moko bwana!! Hapa ametoa tafsiri ya mambo kama ifuatavyo:-
  1. Ugomvi upo ila si mkubwa.
  2. Ukiwa na mahusiano mabaya na Raisi vyombo vya dola vinakuhusu (Whaaat???!!)

Kazi kwenu wanajamvi. Hiyo namba 2 inawahusu wengi wenu humu si mnatafuta bifu na JK teh.

ni Tanzania pekee ambapo rais anaweza kutumia majeshi kwa manufaa yake binafsi.
 
Wewe ni hoperess. Mimi ni kiongozi wa familia. Kwa nini nisielezwe kama Lowassa alikuwa adui mkubwa wa Mwalimu.
 
Kama ulikuwepo ugomvi,ugomvii huo ulikuwa unahusu jambo gani? Kama sasa hivi ni common knowledge mitaani kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa hapatani kabisa na Lowassa. Ipo kashfa ya Richmond ambapo Lowassa amegombana na Bunge,lakini Mwalimu Nyerere hakuwepo.

From the horse mouth
 
Back
Top Bottom