Ridhwani: Kikwete hana ugomvi na Lowassa

Ridhwani: Kikwete hana ugomvi na Lowassa

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,412
Reaction score
28,457
Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete, amesema kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa na ugomvi na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, asingeshindwa kumshughulikia kwa kuwa anayo mamlaka na vyombo vyote vya ulinzi vipo chini yake.

Ridhiwan, ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete alisema hayo kupitia kipindi cha wanasiasa kinachorushwa na kituo cha televisheni ya StarTv.

Alisema Rais anayo mamlaka na kwamba, hawezi kuwa na ugomvi mkubwa na kiongozi akamshindwa na kutolea mfano namna viongozi wa nchi nyingine wanavyofanya kwa wapinzani wao wa kisiasa.

Mbunge huyo, ambaye hivi karibuni aliingia mgogoro na vyombo vya habari akiwatuhumu waandishi kuwa ni makanjanja na watu wanaoandika vitu vya ovyo ovyo, alisikika akisema kwamba, wanasiasa hao hawana ugomvi mkubwa badala yake unakuzwa na watu.

Alisema hayo baada ya kutakiwa kuzungumzia makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na uhusiano kati ya baba yake, Rais Kikwete na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Lowassa.

Aliongeza kuwa mambo hayo yanakuzwa na kimsingi hakuna ugomvi mkubwa kama inavyodaiwa na kukuzwa na watu wengi.

Alisema Lowassa na baba yake wamekuwa marafiki kwa miaka mingi na kwamba, watu wanajaribu kuwachonganisha wawili hao.

"Edward (Lowassa) akiwa na shida huwa anafika Ikulu na kufanya mazungumzo na Rais huo mgogoro unaosemwa unakuzwa na watu," alisema Ridhiwan.

Akizungumza na NIPASHE kuhusu kauli hiyo aliyoitoa katika kipindi cha Star Tv, Ridhiwan alimsikiliza mwandishi swali lake lake na kisha akasema hawezi kujibu kwa kuwa alikuwa kwenye kikao.

"Nipo kwenye kikao, siwezi kujibu kitu. Ndiyo maana ulikuwa unapiga, nakata. Na ndiyo maana nimetoka nje kukusikiliza mara moja," alisema Ridhiwan.

Ridhiwani alijibu madai hayo kwa kifupi, huku akikataa kutoa ufafanuzi wa kile alichoulizwa na kisha akakata simu.


Chanzo: Nipashe
 
Mbunge wa Chalinze, kada wa CCM na mwanasiasa nguli, Mh Ridhwani Kikwete ameweka hadharani kwamba Rais Kikwete hana ugomvi na Lowasa hata kidogo. Ridhwani ametoa ufafanuzi huo kufuatia tuhuma za baadhi ya watu wanaomtuhumu Kikwete kumtosa Lowasa wakati akiandamwa na tuhuma za ufisadi wa Richmond.

"Kama angekuwa na ugomvi naye angemshughulikia kwa kuwa anayo mamlaka, nguvu na uwezo wa kufanya hivyo", alisema Ridhwani. Mbunge huyo machachari pia alitumia fursa hiyo kuelezea urafiki wa muda mrefu kati ya Kikwete na Lowasa, marafiki ambao hawakukutana barabarani.

Source:Nipashe

:israel:

Ridhwani ni Jembe
 
nadhan ridhiwani nae ni kama january makamba, hopeless. Chama inabid kiwachunge sana vijana hawa media zinawafuata sana na ni wepesi wa kuropoka
 
nadhan ridhiwani nae ni kama january makamba, hopeless. Chama inabid kiwachunge sana vijana hawa media zinawafuata sana na ni wepesi wa kuropoka

dogo anapenda kuropoka sana, na huu uropokaji wake utakuja kumtokea puani siku moja.
 
Ridhiwani alinukuliwa akisema baba yake Kikwete hana uadui na Lowassa na angekuwa na uadui naye angemshulikia maana vyombo vyote vya ulinzi vipo chini yake.
Je, alimaanisha nini?
Ina maana JK akimchukia mtu anatumia vyombo vya ulinzi kumshughulikia?
Nini hasa undani wa kauli hii nzito?
Ridhiwani wewe ni member hapa jf jitokeze ujibu tafadhali.
 
Kama kweli kasema hayo basi anatakiwa sasa ashauriwe na kuambiwa nini cha kusema na wapi pa kusema nini
Mkuu alishayasema hayo na vyombo vya habari vikamnukuu hadi leo hii habari ipo magazetini.
 
Udaku unaduzi. Habari hii ungepeleka Tanzania Daima wangekuona wa maana
 
Dogo ni bonge la mburula sijui hana washauri wa kumwambia cha kusema na jinsi ya kujibu maswali? yaani sasa ndio naamini kauli ya Mbowe kuwa uingereza Riz alikuwa hasomi kazi yake ilikuwa mademu tu..........then kwa hizo thinking ndio wanajidanganya na mama salma kuwa watatupatia Membe kuwa rais.....
 
Back
Top Bottom