Ridhwani: Kikwete hana ugomvi na Lowassa

Ridhwani: Kikwete hana ugomvi na Lowassa

12STONE

Ridhiwani Kikwete ni millionare in US$, sidhani kama uyasemayo ni kweli

Pili Raisi wanaemtaka CCM ni Mzanzibari na ni rafiki yao hao Ridhiwani. Hilo halina mashaka mkuu

Ni Familia yenye Hila na Unafiki dhidi Lowassa,wanacheka modomoni moyoni wanalia.

Ridhiwani ni kiherehere juilizeni kwanini kuna baadhi ya Wakuu wa Wilaya wanawekwa kwa shinikizo lake?

Subiri muda Octoba sio mbali uchaguzi ukipita akapatikana RAIS MPYA utakuja eleza huo UKWASI/MALI MINGI umezipatapataje.

Fedha ulizokusanya isivyo halali ile iliyo ya WATANZANIA UTARUDISHA HATA SENTI YA MWISHO.
 
Hakuna mtu atakayetoka zanzibar aje atawale bara tena katika hilo tanganyika iko hai hawezekani nchi yote hii hasa wengi kutawawaliwa na wachache wazanzibar muda huo umeshakoma.
 
12STONE

Hilo ndio lililowekwa kichwani mwako wewe pengine na watanganyika wengi,

lakini kama hujui maana ya mchizo wa kuigiza basi siasa ni mcezo wa kuigiza, katika majina hayo unayoyasikia yakitajwa katika viongozi hakuna hata mmoja anayejali maslahi yako wewe na mimi walala hoi

kwahivo mutaekewa mzanibari mukitaka musitake, kwasababu wewe na mimi sio tunaochaguwa mkuu. Na wataomweka ni watanganyika wenzako.

Hakuna mtu atakayetoka zanzibar aje atawale bara tena katika hilo tanganyika iko hai hawezekani nchi yote hii hasa wengi kutawawaliwa na wachache wazanzibar muda huo umeshakoma.
 
Lakini kupitia UVCCM Bagamoyo alishawekawazi kuwa rais kupitia CCM hatatoka kaskazini!
 
12STONE

Hilo ndio lililowekwa kichwani mwako wewe pengine na watanganyika wengi,

lakini kama hujui maana ya mchizo wa kuigiza basi siasa ni mcezo wa kuigiza, katika majina hayo unayoyasikia yakitajwa katika viongozi hakuna hata mmoja anayejali maslahi yako wewe na mimi walala hoi

kwahivo mutaekewa mzanibari mukitaka musitake, kwasababu wewe na mimi sio tunaochaguwa mkuu. Na wataomweka ni watanganyika wenzako.

Hizo ni hisia zako za kutaka kutuaminisha uzanzibar/ukabila na udini/uislamu Nchi iko hoi kiuchumi hatuwezi kucheza na kumkabidhi mzenji awe anatokea huko huko visiwani ama awe ni pandikizi lenye mwonekano wa Tanganyika,KABURU NI KABURU TU HATA KAMA ANA NGOZI NYEUSI NI KABURU TUU!!!
 
12STONE

Jaribu kuukubai ukweli mkuu, mimi na wewe hatuna chaguo tz, tunalazimishwa tu. yaani hata hili huwezi kuliamini pia

Hizo ni hisia zako za kutaka kutuaminisha uzanzibar/ukabila na udini/uislamu Nchi iko hoi kiuchumi hatuwezi kucheza na kumkabidhi mzenji awe anatokea huko huko visiwani ama awe ni pandikizi lenye mwonekano wa Tanganyika,KABURU NI KABURU TU HATA KAMA ANA NGOZI NYEUSI NI KABURU TUU!!!
 
Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete, amesema kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa na ugomvi na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, asingeshindwa kumshughulikia kwa kuwa anayo mamlaka na vyombo vyote vya ulinzi vipo chini yake.

Ridhiwan, ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete alisema hayo kupitia kipindi cha wanasiasa kinachorushwa na kituo cha televisheni ya StarTv.

Alisema Rais anayo mamlaka na kwamba, hawezi kuwa na ugomvi mkubwa na kiongozi akamshindwa na kutolea mfano namna viongozi wa nchi nyingine wanavyofanya kwa wapinzani wao wa kisiasa.

Mbunge huyo, ambaye hivi karibuni aliingia mgogoro na vyombo vya habari akiwatuhumu waandishi kuwa ni makanjanja na watu wanaoandika vitu vya ovyo ovyo, alisikika akisema kwamba, wanasiasa hao hawana ugomvi mkubwa badala yake unakuzwa na watu.

Alisema hayo baada ya kutakiwa kuzungumzia makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na uhusiano kati ya baba yake, Rais Kikwete na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Lowassa.

Aliongeza kuwa mambo hayo yanakuzwa na kimsingi hakuna ugomvi mkubwa kama inavyodaiwa na kukuzwa na watu wengi.

Alisema Lowassa na baba yake wamekuwa marafiki kwa miaka mingi na kwamba, watu wanajaribu kuwachonganisha wawili hao.

"Edward (Lowassa) akiwa na shida huwa anafika Ikulu na kufanya mazungumzo na Rais huo mgogoro unaosemwa unakuzwa na watu," alisema Ridhiwan.

Akizungumza na NIPASHE kuhusu kauli hiyo aliyoitoa katika kipindi cha Star Tv, Ridhiwan alimsikiliza mwandishi swali lake lake na kisha akasema hawezi kujibu kwa kuwa alikuwa kwenye kikao.

"Nipo kwenye kikao, siwezi kujibu kitu. Ndiyo maana ulikuwa unapiga, nakata. Na ndiyo maana nimetoka nje kukusikiliza mara moja," alisema Ridhiwan.

Ridhiwani alijibu madai hayo kwa kifupi, huku akikataa kutoa ufafanuzi wa kile alichoulizwa na kisha akakata simu.

Chanzo: Nipashe

Huyo Dogo Anaomba Po Tu Kiaina Kwani Anajua Dhahama Inayomuijia Huko Mbele Yeye, Mshua Na Mazeri Wake Pamoja Na Maembe Wao.
 
Kama kuna kijana aliyejisahau kisiasa no huyu Mh. alitakiwa asilewe madaraka ambaye siyo yake. Atulie Kama watoto waviongozi waliotangulia ambao siku zote wamendelea kuwa wanyenyekevu mbele ya watanzania!
 
napata shida ya kujua nani msemaji wa rais wetu punde panapokuwa na hali ya kutoelewana na mtu mwingine....mm nikigombana na rafiki yangu mara nyingi namtumia mama au baba...je mkuu anamtumia RIDHIWAN kujibu iki kinachosemwa
 
Katikati ya mistari naona kikwete hana ugomvi mkubwa na lowasa, lkn huenda anaugomvi mdogo tu na lowasa waandishi wa habari ndio wanaoukuza,hivi huo mdogo ni upi,na kufuatia huo mdogo usiotosha kumshughurikia je?ataruhusu lowasa awe rais?maana kumshughurikia huenda ni kumtia korokoroni.
 
Back
Top Bottom