Ridhwani: Kikwete hana ugomvi na Lowassa

Ridhwani: Kikwete hana ugomvi na Lowassa

Bila shaka alichokitaka Kijana ni kule kuandikwa magazetini kwa kupewa sifa kama alizozitoa mwandishi wa gazeti kuwa yeye ni mwanasiasa maarufu, mahiri, machachari na mkongwe (bila shaka kuliko umri wake). Hajajua kuwa hizo ni sifa wanazompa ili wapate kumlia pesa tu.

Haha haaaaa "mocking bird"..
 
acheni kuchukia watoto wa wenzenu kwa ajili ya fitina za kijinga kujinga.tengenezeni wa kwenu sio mnawafundisha kunywa viroba na maandamano.waacheni vijana wanamea kisiasa.

kwani ni nani anayemchukia? kumnukuu mtu ni CHUKI?
 
Ridhiwani ni BLUBBER MOUTH yaani yeye anaongea hata sidhani kama anakjua repercussion ya maneno yake. Mara katoa tamko la yanga mara urafiki wa baba yake na watu wengine mara chadema,..... huwezi kudhani huyu ni mwanasheria jamani..... people look bright until they open their mouths...Hakuna mtu wakufundisha etiquette huko ikulu?:angry::angry:

Uanasheria kapewa tu sbb ya baba rahisi hamna kitu kabisa humo.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete, amesema kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa na ugomvi na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, asingeshindwa kumshughulikia kwa kuwa anayo mamlaka na vyombo vyote vya ulinzi vipo chini yake.

Ridhiwan, ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete alisema hayo kupitia kipindi cha wanasiasa kinachorushwa na kituo cha televisheni ya StarTv.

Alisema Rais anayo mamlaka na kwamba, hawezi kuwa na ugomvi mkubwa na kiongozi akamshindwa na kutolea mfano namna viongozi wa nchi nyingine wanavyofanya kwa wapinzani wao wa kisiasa.

Mbunge huyo, ambaye hivi karibuni aliingia mgogoro na vyombo vya habari akiwatuhumu waandishi kuwa ni makanjanja na watu wanaoandika vitu vya ovyo ovyo, alisikika akisema kwamba, wanasiasa hao hawana ugomvi mkubwa badala yake unakuzwa na watu.

Alisema hayo baada ya kutakiwa kuzungumzia makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na uhusiano kati ya baba yake, Rais Kikwete na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Lowassa.

Aliongeza kuwa mambo hayo yanakuzwa na kimsingi hakuna ugomvi mkubwa kama inavyodaiwa na kukuzwa na watu wengi.

Alisema Lowassa na baba yake wamekuwa marafiki kwa miaka mingi na kwamba, watu wanajaribu kuwachonganisha wawili hao.

"Edward (Lowassa) akiwa na shida huwa anafika Ikulu na kufanya mazungumzo na Rais huo mgogoro unaosemwa unakuzwa na watu," alisema Ridhiwan.

Akizungumza na NIPASHE kuhusu kauli hiyo aliyoitoa katika kipindi cha Star Tv, Ridhiwan alimsikiliza mwandishi swali lake lake na kisha akasema hawezi kujibu kwa kuwa alikuwa kwenye kikao.

"Nipo kwenye kikao, siwezi kujibu kitu. Ndiyo maana ulikuwa unapiga, nakata. Na ndiyo maana nimetoka nje kukusikiliza mara moja," alisema Ridhiwan.

Ridhiwani alijibu madai hayo kwa kifupi, huku akikataa kutoa ufafanuzi wa kile alichoulizwa na kisha akakata simu.

Chanzo: Nipashe
Aloyasema Ridhwan ndio ukweli na viongozi hawa sii wajinga hivo kama viongozi wengine ambao walichonganishwa kidogo tu tayari wakaanza hata kutosalimiana na wengine kufukuzana. Ule msemo wao Boyz to Men unajionyesha wazi maana wamekua kisiasa, sio wengine bado wamo ktk kundi la Boyz japo midevu kibao.

Kama huijui tabia ya wanafiki itakusumbua sana lakini JK na Lowassa wanajua hayo na wamepitia mengi zaidi ya haya. Kikwete na Lowassa hawana ugonvhi japo Lowassa kaharibu sana kiasi kwamba ingekuwa hakuna Urafiki basi Lowassa asingekuwa CCM, bungeni wala mwenyekiti wa tume za bunge. JK is the President!

Hawa wapo pamoja na kwa pamoja watamchagua mgombea Urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CCM ambaye ni.....naawachia!
 
Mlitaka awajibu nini hao waliomuuliza.? Jakaya yupo tena kucha kutwa mabarabarani humu bongo star tv hawamuoni.? Mbona hawamuulizi ilihali wanamripoti kila uchao! Wabongo sijui tunaumwa nini?! Mh.rais yuko ruvuma hapo star tv na makamera yenu mko naye muulizeni basi.....

Story ya ajabu sana hii?
 
Aloyasema Ridhwan ndio ukweli na viongozi hawa sii wajinga hivo kama viongozi wengine ambao walichonganishwa kidogo tu tayari wakaanza hata kutosalimiana na wengine kufukuzana. Ule msemo wao Boyz to Men unajionyesha wazi maana wamekua kisiasa, sio wengine bado wamo ktk kundi la Boyz japo midevu kibao.

Kama huijui tabia ya wanafiki itakusumbua sana lakini JK na Lowassa wanajua hayo na wamepitia mengi zaidi ya haya. Kikwete na Lowassa hawana ugonvhi japo Lowassa kaharibu sana kiasi kwamba ingekuwa hakuna Urafiki basi Lowassa asingekuwa CCM, bungeni wala mwenyekiti wa tume za bunge. JK is the President!

Hawa wapo pamoja na kwa pamoja watamchagua mgombea Urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CCM ambaye ni.....naawachia!

wewe naye ndo walewale....mara fulani kaharinu...mara watachagu mgombea fulani.....peanuts contributions ndani jf
 
Kwa kauli hii "kama Rais Jakaya
Kikwete angekuwa na
ugomvi na Mbunge wa
Monduli (CCM), Edward
Lowassa, asingeshindwa
kumshughulikia kwa kuwa
anayo mamlaka na vyombo
vyote vya ulinzi vipo
chini yake" yafaa tuhoji ni wangapi amewashughulikia. Na je vema kujigamba na vyombo vya dola kwa masilahi au ugomvi binafsi? Je hii kauli haidhibitishi malalamiko kuwa ikulu inahusika na kupiga, kutesa na kung'oa meno na kucha wakosoaji wa serikali ya ccm ka kina mwangosi?
Tafakarini hata wachawi hukosea wakajitaja!!!
 
Mkuu sikubaliani hata chembe kuwa Lowassa kaharibu sana! JK aliharibu sana alipokubaliana na fitna za Sitta na Membe... Since then Serikali yake imepwaya ile mbaya...
Aloyasema Ridhwan ndio ukweli na viongozi hawa sii wajinga hivo kama viongozi wengine ambao walichonganishwa kidogo tu tayari wakaanza hata kutosalimiana na wengine kufukuzana. Ule msemo wao Boyz to Men unajionyesha wazi maana wamekua kisiasa, sio wengine bado wamo ktk kundi la Boyz japo midevu kibao.

Kama huijui tabia ya wanafiki itakusumbua sana lakini JK na Lowassa wanajua hayo na wamepitia mengi zaidi ya haya. Kikwete na Lowassa hawana ugonvhi japo Lowassa kaharibu sana kiasi kwamba ingekuwa hakuna Urafiki basi Lowassa asingekuwa CCM, bungeni wala mwenyekiti wa tume za bunge. JK is the President!

Hawa wapo pamoja na kwa pamoja watamchagua mgombea Urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CCM ambaye ni.....naawachia!
 
How? Ulitaka aseme kuwa ni kweli JK ana ugomvi Mkubwa na Lowassa? Zile kura za marohani zilikuwa neutralized baada ya Lowassa kubuni mkakati wa kupiga kura kwa majimbo na mikoa! Otherwise hali ya hewa ingechafuka ile mbaya!! Ukweli ni kuwa Lowassa ana watu wengi sana nyuma yake! Wengi wanamuona kama mtendaji na reformer for better or for worse... kwake kufanya maamuzi ni issue ndogo sana tofauti na wanao lia lia kwa kuwang'oa watu kucha na meno huku kila sekta ikiwa kwenye usingizi mzito wa pono... JK anamiss sana Lowassa kama PM....
Jamaa mdomo wake hauna break hata kidogo
 
...ingawa ameulizwa swali lisilo muhusu ingawa ukweli unaonekana aliposema unakuzwa,inamaana upo...
 
Hakuna ugomvi mkubwa kama inavyodaiwa inaamanisha uko ugomvi, pili hakukua na sababu Rz1 kusema rais angeweza kumshughulikia kama angekuwa ana ugomvi nae! Majibu kama haya ni ya vitisho!
 
Kwa kauli hii "kama Rais Jakaya
Kikwete angekuwa na
ugomvi na Mbunge wa
Monduli (CCM), Edward
Lowassa, asingeshindwa
kumshughulikia kwa kuwa
anayo mamlaka na vyombo
vyote vya ulinzi vipo
chini yake" yafaa tuhoji ni wangapi amewashughulikia. Na je vema kujigamba na vyombo vya dola kwa masilahi au ugomvi binafsi? Je hii kauli haidhibitishi malalamiko kuwa ikulu inahusika na kupiga, kutesa na kung'oa meno na kucha wakosoaji wa serikali ya ccm ka kina mwangosi?
Tafakarini hata wachawi hukosea wakajitaja!!!

words....
 
Back
Top Bottom