Ridhwani: Kikwete hana ugomvi na Lowassa

Ridhwani: Kikwete hana ugomvi na Lowassa

Adui wa Rais ni adui wa Taifa. Hivyo maadui wa taifa wanashughulikiwa na vyombo husika kwa mujibu wa sheria zilizopo
 
Udaku unaduzi. Habari hii ungepeleka Tanzania Daima wangekuona wa maana

Najua ungependa habari ya kusifia magamba tu. Yaani cha ajabu wenzako wakuongea tukiwanukuu hamtaki. Kwa taarifa yako Chombo cha habari kilichokuwa kinamhoji ni cha mwanaccm sio upinzani. StarTv ndo source yenyewe
 
Adui wa Rais ni adui wa Taifa. Hivyo maadui wa taifa wanashughulikiwa na vyombo husika kwa mujibu wa sheria zilizopo

Una uhakika???!!!
Kuweni makini na maneno yanayoonekana kama ya kisiasa wakati ni ya Kitaifa!!!
 
Taasisi ya Urais ktk Taifa ina hadhi kubwa na heshima ya pekee.
Office ya Rais, wasemaji wapo, ni matumaini yangu ndiyo wangeweza kuzungumzia mamlaka ya Rais na marafiki zake au Mh Rais mwenyewe.
Hi hali ya mtoto wa Mh Rais, kuwa msemaji wa Mh Rais na marafiki wa Mh Rais, Mamlaka ya Rais etc etc inatia doa hadhi ya Office nyeti na yenye heshima kubwa ktk taifa.

Awamu zilizopita, mambo haya sikuwahi kuyaona na kuyasikia..., Mfano. Mh Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, alikuwa na wanae but watoto waliheshimu nafasi ya baba yao kama Rais, pamoja na ss wananchi wa Taifa hili.

Daima ninaipenda Tanzania yetu.
 
Kunya anye kuku akinya bata kaharisha mbona jk hana ugomvi na yeyote ni maneno tu ya wapinzani uchwara
 
Amejichanganya sana kwenye haya maelezo yake..

1.Kwa mamlaka aliyonayo angeshamuwajibisha..Je wangapi wameshafanyiwa hivyo? Je Vipi kama Jk ndiyo aliye mkosea EL ??

2.Ugomvi siyo mkubwa kama vyombo vya habari vinavyosema..Je Maana yake Ugomvi upo ila ni mdogo?

3.EL akiwa na shida anaenda Ikulu kuonana na Mh.Jk.. Hapa akili Mukichwa..
 
kwani huko ccm kuna kijana anayejitambua , au wote ni hopeless na useless .........
acheni kuchukia watoto wa wenzenu kwa ajili ya fitina za kijinga kujinga.tengenezeni wa kwenu sio mnawafundisha kunywa viroba na maandamano.waacheni vijana wanamea kisiasa.
 
Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete, amesema kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa na ugomvi na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, asingeshindwa kumshughulikia kwa kuwa anayo mamlaka na vyombo vyote vya ulinzi vipo chini yake.

Ridhiwan, ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete alisema hayo kupitia kipindi cha wanasiasa kinachorushwa na kituo cha televisheni ya StarTv.

Alisema Rais anayo mamlaka na kwamba, hawezi kuwa na ugomvi mkubwa na kiongozi akamshindwa na kutolea mfano namna viongozi wa nchi nyingine wanavyofanya kwa wapinzani wao wa kisiasa.

Mbunge huyo, ambaye hivi karibuni aliingia mgogoro na vyombo vya habari akiwatuhumu waandishi kuwa ni makanjanja na watu wanaoandika vitu vya ovyo ovyo, alisikika akisema kwamba, wanasiasa hao hawana ugomvi mkubwa badala yake unakuzwa na watu.
Chanzo: Nipashe
Kuna haja ya wapambe wa Rais wetu kumfunga domo gavana huyu kijana, Ridhiwani.
Anaweza kutengeneza tatizo pasipokuwa na tatizo.
Bado hajawa gwiji la kisiasa na si msemaji wa taasisi ya urais.
Domo huponza kichwa.
 
Ridhiwani ni BLUBBER MOUTH yaani yeye anaongea hata sidhani kama anakjua repercussion ya maneno yake. Mara katoa tamko la yanga mara urafiki wa baba yake na watu wengine mara chadema,..... huwezi kudhani huyu ni mwanasheria jamani..... people look bright until they open their mouths...Hakuna mtu wakufundisha etiquette huko ikulu?:angry::angry:
 
Udaku unaduzi. Habari hii ungepeleka Tanzania Daima wangekuona wa maana

mkuu, wakati mwingine uwe unaficha upumbavu wako. kunya anye kuku, akinya bata uharo?
 
Kama kweli kasema hayo basi anatakiwa sasa ashauriwe na kuambiwa nini cha kusema na wapi pa kusema nini

Bila shaka alichokitaka Kijana ni kule kuandikwa magazetini kwa kupewa sifa kama alizozitoa mwandishi wa gazeti kuwa yeye ni mwanasiasa maarufu, mahiri, machachari na mkongwe (bila shaka kuliko umri wake). Hajajua kuwa hizo ni sifa wanazompa ili wapate kumlia pesa tu.
 
Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete, amesema kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa na ugomvi na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, asingeshindwa kumshughulikia kwa kuwa anayo mamlaka na vyombo vyote vya ulinzi vipo chini yake.



hopeless RIDHIWANI.....!! mshauri ajaribu kuviamuru hivyo vyombo vimshughulikie Lowasa ndipo utaona ikiwa kweli viko chini yake au la.
 
Back
Top Bottom