Familia ya Nyerere ni nani kabaki? Madaraka ndie spokesman sasa hivi ambae nae amesha anza kupoteza gololi.
Madaraka anasema Baba yake ni mpenda amani ambaye angekuwepo angeshamsamehe Amini. Baba yake si mtu wa kusamehe maadui, hakwenda hata kwenye msiba wa Kambona, mpaka Makongoro akaona aibu akaenda.
Madaraka anatoa misahama kwa waanzilishi wa vita vya Kagera eti kwa vile ni mambo yalitokea zamani. Anadhani vile ni vita kati ya baba yake na Amin. Watu wamekufa kwa ajili ya kutetea nchi, na kwa kuheshimu siasa na matakwa ya Amiri Jeshi Mkuu. Havikuwa visa vya wanaume wawili kugombea kimada vile.
Lakini sitegemei Madaraka awe amerithi na kujifunza mengi kutoka kwa baba. Ameiambia BBC kwamba Nyerere alikuwa anawafunga midomo kujadili maswala ya kazi yake na siasa wakiwa kwenye meza ya chakula. Madingi wetu wa Kibongo tena, mambo ya kazi ni mambo ya kikubwa. Watoto hakuna kuuliza uliza mambo ya kikubwa.
Makongoro nae alishaanza kupoteza gololi kwenye pombe, akarudi CCM. John anaumwa, kafungiwa ndani maisha yake yote. Magige mwanakijiji Butiama ambako hata radio signals hazifiki, hayuko in touch na nini kinaendelea duniani. Rosemary na Mama Maria wanawasikiliza Madaraka na Makongoro, mfumo dume.
Anaefuatia, ambae bado hajapoteza goroli pale, ni Butiku. Lakini Butiku nae hawezi kujifanya kama ni mtoto wa Nyerere, inabidi aende ende na kina Makongoro wanavyotaka, japo siku zote kina Makongoro walikuwa hela yao ya kula anaishika Butiku, Kambarage hakuwa na muda na watoto. Sasa kwa Butiku, Makongoro hawezi kuwa mtu huru, alishahongwa hongwa fadhilia na Mkapa, mlezi wa familia. Mkapa ana bifu la damu na Butiku, maana Nyerere alipokufa Mkapa akawaweka pembeni watu wa Nyerere, Butiku hakupenda, akaona huyu afisa wa mambo ya nje asiye na jina tumempandisha kwenye magari ya wazi kumuuza Tanzania nzima leo hanisikilizi? Akamwita Mkapa fisadi hadharani. Kumbe Mkapa aliwahi kumnunua mmoja wa familia akijua atamhitaji mbeleni. Mgawanyiko. Makongoro na Mkapa na Butiku na Madaraka. Mkorogo wa uongozi pale Butiama.