Ridhiwani: Tumeishi na RC Makonda vizuri ila kutajwa kwenye madawa, kama familia tunamwachia Mungu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Dar es Salaam. Baada ya kuitwa kuhojiwa kuhusu tuhuma za kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema taarifa hizo zilitingisha familia yake, lakini baba yake Jakaya Kikwete alimtia moyo.

Tofauti na watuhumiwa wengine waliohojiwa kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya, Ridhiwani hakutangazwa hadharani badala yake aliitwa kimyakimya na kuhojiwa na baadaye kuruhusiwa aendelee na shughuli zake baada ya kuonekana hana hatia.

Katika mahojiano maalumu na Mwananchi Digital yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Ridhiwani amesema JK hakushtushwa na badala yake alimpa nguvu ya kwenda kueleza ukweli .

“Pengine aliamua kuficha hofu yake ili kunitia nguvu,” amesema Ridhiwani.

Pia soma:
 
Mbona aliwahi kusema roho yake ilisuuzika kwa kuhojiwa, maana hiyo ilikata mzizi wa fitina wa tuhuma? Kwa maneno mengine alihitaji sana uwepo wa Tume ya kuwaambia ukweli watanzania juu yake na tuhuma zisizokuwa na kichwa wala miguu! Sasa anamlaumu vipi Makonda?
 
Back
Top Bottom