Ridhiwan Kikwete: Mimi si fisadi

Ridhiwan Kikwete: Mimi si fisadi

Na UDOM je? dini moja ndo wanaqualify
...Hii labda umfahamishe Vizuri Fundi Mchundo na Lole Dini inayoqualify hapo UDOM...
So far ushauri wangu Bwana Mdogo RIZ akae pembeni aachane na SIASA kwa sasa. sio kwamba tunamwima uhuru wake kama mtanzania mwingine lkn ktk kujenga na kuweka Mipaka ya SIASA na Familia. na mengine ambayo kwa namna moja au Nyingine yanaharibu haiba ya JK ktk Jamii.

Ninaloliona si RIZ, ni Kundi lake alilokuwa nalo UDSM ambalo linampush aende front na kufanya vitu vya visivyoeleweka.
 
huyu ridhiwani ni nani kwani????
Hivi Kikwete si anamtoto anaitwa Miraji mlaunga.....
 
75 - 80% ya wanaoqualify UDOM ni dini moja na RIZ ONE, sio wanafunzi tu hata wafanyakazi wengine wa kawaida. Nilipododosa kwa nini hakuna sababu za msingi zilizotolewa zaidi ya kuambiwa kwamba msaada mkubwa ulitolewa na waarabu, sijui kama ilikuwa ni one of the attached conditions au vp. Lakini cha kushangaza ni kwamba mifuko yetu ya jamii imecontribute kwa kiwango kikubwa ubaguzi unakujaje sijui. Nilipomuuliza muadhiri mmoja katika chuo hicho alikubaliana na madai haya bila kusita !
 
Mimi nawashangaa wana JF hamna cha kujadili ,bali mnamsakama Ridwan Kiwete alipokemea udini . Nawaomba muende mkasome katiba ya TANZANIA ibara ya 18 imbayo inampa mamlaka kila mtanzania uhuru wa kutoa maoni yake. Mimi nam surpport kwa 100% udini si kitu kizuri tukiuegemea utapeleka Taifa letu pabaya .

Mpe kura za ndio Mhe . DK JAKAYA KIKWETE tarehe 31 Oktoba 2010
 
.....:violin:ACHA KIJANA AJIMWAGE BWANA, BABA AMEMTUMA AKAMPIGIE KAMPENI KUSINI.
NDIYO MAMLAKA ANAYO YA KUKEMEA KWANI WEWE HUJUI KUWA RAIS JK ,
URAISI WAKE UNA UBIA NA FAMILIA YAKE.

Itabidi aanze huko nyumbani kwao kumkemea baba yake aache unafiki wakujidai kuwa sio mdini kumbe yeye ndiye kinara wa kupendelea dini moja katika kugawa vyeo vya serikali!! Wajifunze huko kwao kuwa URAIS ni institution na wala sio ngoma ya UNYAGO wa familia!!
 
Tatizo kubwa ni kuwa vijana wanakwenda shule kupata shahada na sio kuelimika. Huyu kijana angekuwa ameelimika kwa kusoma historia ya dunia asingeingia siasa kwani angegundua yaliyompata mtoto wa Saddam Hussein kwa kutumia cheo cha baba yake na kisha kupata umauti kikatili!!
 
mbona hajamkemea baba yake kikwete kwa kuweka mahakama ya kadhi kwenye ilani ya ccm..........haamini au hajui kuwa hayo ni mambo ya dini?....udini anao kikwete kwa vitendo wengine ni propaganda tu za siasa angeanza kwa kutoa boriti jichoni mwa babake mwenyewe kabla ya kukurupuka na kuwanyooshe vidole wengine.......
 
75 - 80% ya wanaoqualify UDOM ni dini moja na RIZ ONE, sio wanafunzi tu hata wafanyakazi wengine wa kawaida. Nilipododosa kwa nini hakuna sababu za msingi zilizotolewa zaidi ya kuambiwa kwamba msaada mkubwa ulitolewa na waarabu, sijui kama ilikuwa ni one of the attached conditions au vp. Lakini cha kushangaza ni kwamba mifuko yetu ya jamii imecontribute kwa kiwango kikubwa ubaguzi unakujaje sijui. Nilipomuuliza muadhiri mmoja katika chuo hicho alikubaliana na madai haya bila kusita !
75-80% wanafuzu UDSM ni wadini moja na Mkapa, Na > 80% wafanyakazi wa UDSM ni wadini hiyo je hapo kuna upendeleo? Mpaka masisita wa katoliki ni wahadhiri na wafanyakazi pale UDSM. Kwahiyo tatizo sio UDOM tu.
 
Na hiyo ndiyo iliyokutoa CCM mwaka huu? Na wale wa kanisani kuacha kutuhubiria kuwa JK ni chaguo la Yesu na kutuletea MWONGOZO wa kumchagua padri? Kweli nyani haoni kikalio chake.
 
75-80% wanafuzu UDSM ni wadini moja na Mkapa, Na > 80% wafanyakazi wa UDSM ni wadini hiyo je hapo kuna upendeleo? Mpaka masisita wa katoliki ni wahadhiri na wafanyakazi pale UDSM. Kwahiyo tatizo sio UDOM tu.

Hawa watu wa kanisani hawana jipya. Sasa huyo hata umwambie nini, MWONGOZO ushamuingia na lazima atampigia kura padri.
 
75-80% wanafuzu UDSM ni wadini moja na Mkapa, Na > 80% wafanyakazi wa UDSM ni wadini hiyo je hapo kuna upendeleo? Mpaka masisita wa katoliki ni wahadhiri na wafanyakazi pale UDSM. Kwahiyo tatizo sio UDOM tu.

Kuna mtu aliwakataza Masheikh kuwa wahadhiri? Mwalimu wangu mzuri kabisa wa Statistics ni mzanzibari na yuko fit kweli, unamkumbuka mussa Assad? na wengine weeeengi tu waliingia pale kutokana na umakini wa kazi zao na uwezo wao mkubwa sio dini. Mbona kuna maprofesa wengine wakristo ovyo tu, wengine kazi yao kununua mabenzi na kutembela na machangudoa.....my point is dini hapa sio issue issue ni uwezo wa mtu. Kama kuna mashehe na masista wa waislamu wanaweza kuja tu mlimani bila kujali dini yao.
 
Mwandishi mwingine MCL apata misukosuko Send to a friend Saturday, 25 September 2010 10:26 0diggsdigg

mwananch.jpg
Mwandishi Wetu, Songea

MWANDISHI mwingine wa magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), amepata misukosuko kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwandishi huyo Kwirinius Mapunda alipata mkasa huo, baada ya kuwekwa kizuizini mjini Songea, na walinzi wa CCM wakati wa ziara ya Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana (UVCCM) Ridhiwani Kikwete.

Ridhiwani alifika Songea mjini akitokea Namtumbo akifanya kazi ya kuomba kura kwa wagombea wa CCM.

Waandishi wengine wa Mwananchi ambao walishakumbwa na misukosuko katika kampeni za CCM ni Frederick Katulanda na Ray Naluyaga, wote wa Mwanza.

Katika tukio hilo Mapunda aliwekwa chini ya ulinzi na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya CCM mkoani Ruvuma, ambaye alimzuia kutekeleza majukumu yake

Mbali na kujitambulisha kuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya mkoa, mtu huyo pia alidai kuwa ni mmoja wa mwanafamilia wa mgombea wa urais kupitia CCM, Jakaya Kikwete.

Mara baada ya kuwasili kwa mgeni huyo wa UVCCM, mtu huyo alianza kumhoji mwandishi wa Mwananchi akitaka kujua ataandika nini kwenye ziara hiyo.

Mwandishi alimjibu kwamba ataandika atakayoyasikia na kuona na kwamba baada ya maelezo hayo , ofisa huyo alimtaka mwandishi wa habari apande gari alilokuwa akiliongoza yeye.

Msafara ulianzia ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma na kwamba ulipofika ofisi ya CCM Wilaya ya Songea mjini, ofisa huyo alizidi kuwa karibu huku akimzonga wakati wa kupiga picha.
Ridhiwani Kikwete pamoja na wenyeji wake waliingia kwenye ukumbi ambapo, naye mwandishi aliingia.

Lakini ghafla baada ya muda mfupi kijana wa CCM aliyevalia mavazi yaliyoandikwa Green Guard, alifika na kumweleza mwandishi kwamba alikuwa akiitwa nje ya ukumbi.

Mwandishi alinyanyuka kwenda nje ambako hakumkuta mtu yeyote na kwamba alipochunguza zaidi aligundua kwamba gari alilopangiwa lilikuwa limeondoka likiwa na mfuko wake wa kamera na vifaa vingine.

Mapunda alianza kusaka namba ya simu ya ofisa wa CCM ambapo baadaye aliipata na kumpigia simu.

Ofisa wa CCM huyo alijibu kwamba gari analo na kwamba mzigo wake upo salama, lakini akasisitiza kwamba asubiri nje.

Mwandishi alipojaribu kuingia ndani , aliambiwa na vijana wa CCM kwamba haruhusiwi kuingia kwenye mkutano wa ndani jambo ambalo lilimshtua zaidi.

Lakini kibaya zaidi yule ofisa aliyetoweka na gari likiwa na mfuko wa mwandishi , naye hakurudi na baadaye alipiga simu kwamba mzigo wa mwandishi ulikuwa kwenye Hoteli Top In One iliyopo maeneo ya Msamala.
Kufuatia hali hiyo Mwandishi aligundua kwamba tukio lilikuwa la makusudi.

Katibu wa UVCCM wa Mkoa wa Ruvuma, Mwajuma Rashid, alipoulizwa kama anafahamu lolote juu ya tukiuo hilo alisema safari ya Ridhiwani Kikwete iliratibiwa na ofisi yake na kwamba aliyemsumbua mwandishi hakumuona.
 
Taaanzania Tanzaniaaaaaaaa, nakupenda kwa moyo wooooote, nnnnnchi yangu Tanzaniaaaaa,jina lako ni tamu sanaaaaaaaa!!!!!!
Mzigo wa Bilioni 3 ------>>> ......kwa Sheikh.....ufalmeni,jirani na Waajemi....teh...teh...teh...
 
:confused2:
 
kwa muda mrefu sana watanzania walishaupiga vita usultani wa kuzaliwa hata wa kuchaguliwa. Najiuliza huu mshikamano wa familia moja kupigania utawala wa kisiasa hatima yake ni nini?

Ridhiwani na mama yake wamekuwa na nguvu kubwa sana ndani ya CCM hata makatibu wa CCM wa mikoa na Wilaya hawakohoi mbele yao. swali la kujiuliza hatima ya taifa letu itakuwaje huko tuendako, kwenye mikono ya hii familia ya Kikwete?
 
usultani unarudi taratibu Tanzania

Pia kuna Makamba na January wake
 
kwa muda mrefu sana watanzania walishaupiga vita usultani wa kuzaliwa hata wa kuchaguliwa. Najiuliza huu mshikamano wa familia moja kupigania utawala wa kisiasa hatima yake ni nini?

Ridhiwani na mama yake wamekuwa na nguvu kubwa sana ndani ya CCM hata makatibu wa CCM wa mikoa na Wilaya hawakohoi mbele yao. swali la kujiuliza hatima ya taifa letu itakuwaje huko tuendako, kwenye mikono ya hii familia ya Kikwete?

Mkuu 'senksi' yangu nakugongea kwa nje kwa kuwa nina swali hapo juu......Ridhiwani na mama yake!?...unamaanisha mama yupi huyo??? hapo tu mkuu, sina neno na mada...imetulia.
 
kwa muda mrefu sana watanzania walishaupiga vita usultani wa kuzaliwa hata wa kuchaguliwa. Najiuliza huu mshikamano wa familia moja kupigania utawala wa kisiasa hatima yake ni nini?

Ridhiwani na mama yake wamekuwa na nguvu kubwa sana ndani ya CCM hata makatibu wa CCM wa mikoa na Wilaya hawakohoi mbele yao. swali la kujiuliza hatima ya taifa letu itakuwaje huko tuendako, kwenye mikono ya hii familia ya Kikwete?
Jakaya, Salma, Miradji, Ridhiwan Kikwete = Tanzania sultanate of kikwete
 
Back
Top Bottom