BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,849
Ridhiwan Kikwete: Mimi si fisadi
na Charles Mullinda
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
MTOTO mkubwa wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete, amesema hahusiki kwa namna moja au nyingine na tuhuma za ufisadi zinazowaandama baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi na viongozi waandamizi wa serikali.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili jana kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake katika siku za karibuni kuwa mmoja wa watu waliohojiwa na timu iliyoteuliwa na Rais Kikwete kuchunguza watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA pamoja na kukusanya fedha hizo, alisema hajawahi kuhojiwa na timu hiyo.
Ridhiwan alisema tuhuma zinazoelekezwa kwake sasa kuwa katika kipindi kisichozidi miaka miwili ya kuwa kazini amejilimbikizia ukwasi wa kutisha, ikiwa ni pamoja na kumiliki magari na nyumba kadhaa za kifahari, zina malengo ya kisiasa ili kumpunguza nguvu katika kampeni anazoshiriki sasa ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM.
Alisema katika kipindi chote alichofanya kazi ya uwakili katika Kampuni ya uwakili ya IMMMA, akiba ya fedha alizonazo benki hazizidi shilingi milioni 10, jambo linalothibitisha kuwa yeye si fisadi wala hajawahi kumuibia mtu.
"Watu wanapenda sana kusemasema, lakini mimi kama nilivyosema, sipendi kusema sema, ndiyo maana niko mbali na vyombo vya habari. Mimi si fisadi, simwibii mtu, nafanya mambo yangu mwenyewe.
"Ninatambua ninachokifanya na nina malengo. Ninachohangaika nacho kwa sasa ni kijishamba changu nilichoachiwa na babu yangu, nataka nikope fedha nikiimarishe. Sina fedha jamani, akaunti yangu haina hata milioni 10. Lakini nayajua madhara ya kuwa mwanasiasa ni kama haya, kuzushiwa. Sitasema kitu na hutanisikia nikisema kitu kuhusu hili," alisema Ridhiwan kwa sauti ya masikitiko.
Ridhiwan ametoa kauli hii ikiwa ni siku chache baada ya kuibuka kwa minong'ono kuwa aliitwa na kuhojiwa na timu ya rais inayochunguza kashfa ya EPA.
Katika minong'ono hiyo, Ridhiwan anatajwa kama mmoja wa watu waliofaidika na fedha zilizochukuliwa Benki Kuu ya Tanzania katika akaunti ya EPA na kwamba katika kipindi kifupi alichofanya kazi amejikusanyia ukwasi wa kutisha, ambao haulingani na umri wake katika ajira.
Taarifa hizo zilieleza kuwa Ridhiwan ambaye hajatimiza hata miaka miwili katika ajira yake, anamiliki mamilioni ya shilingi katika benki mbalimbali nchini pamoja na magari kadhaa ya kifahari, na nyumba za kifahari, ambazo hazilingani na kipato chake, madai ambayo yeye ameyakanusha na kuyahusisha na mapambano ya kisiasa ndani ya chama katika kipindi hiki cha uchaguzi wa viongozi wa UVCCM.
Hata hivyo, Ridhiwan katika kukanusha tuhuma hizo, alisema zinatokana na vita ya kuwania madaraka ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), ambayo imeanza kushika kasi mpya, baada ya kujitokeza kwake kumuunga mkono mmoja wa marafiki zake anayegombea uongozi ndani ya umoja huo.
Ridhiwan alisema uchaguzi huo umembana kwa sababu anatumia muda mwingi kumsaidia rafiki yake aliyejitosa kugombea, kwa kuwa anapata upinzani mkali kutoka katika kambi nyingine ndani ya umoja huo.
Bila kumtaja jina rafiki yake huyo wala nafasi ya uongozi anayowania, Ridhiwan alisema baadhi ya wagombea wanaopambana na rafiki yake wameanza kumzushia tuhuma ili kumtisha aache kumuunga mkono rafiki yake.
"Sipendi kuzungumza na ‘media' (vyombo vya habari), kwa sababu tuko katika mapambano ya uchaguzi mkuu wa UVCCM. Ninapambana chini kwa chini kwa sababu ndivyo zilivyo siasa zetu.
"Kinachonishangaza, watu wananiangalia tofauti kabisa kama vile mimi sipaswi kushiriki katika kampeni au siasa, mimi sigombei, anayegombea ni rafiki yangu na kweli ninamuunga mkono. Ninatumia muda mwingi sana kwa sababu kambi tunayopambana nayo inatoa upinzani mkali kwa rafiki yangu," alisema Ridhiwan.
Akizungumza kuhusu uamuzi wake wa kumuunga mkono rafiki yake huyo alisema, unatokana na kuwa karibu naye kwa muda mrefu tangu wakiwa wanafunzi, na kuwataka wanaodhani kwamba alijiunga na kambi isiyostahili, wafahamu kuwa anamfahamu mgombea huyo tangu wakiwa watoto, hivyo anaamini anaweza kuwa kiongozi wa juu wa umoja huo.