Richard Tambwe Hizza kuzikwa makaburi ya Chang'ombe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,600
217,994
Hii ni taarifa iliyotolewa na mdogo wa Marehemu aitwaye Charles Hizza kama ilivyonukuliwa na Gazeti la Mwananchi , kwamba Mwili wa Kamanda Tambwe Hizza utahifadhiwa kwenye Makaburi ya Chang'ombe Maduka Mawili .

Ni mazishi ya Kikristo yatakayofanyika Leo hii , watu wote mnakaribishwa .

UPDATES
..........................................
FITNA ZAFANYWA ILI KUINYIMA CHADEMA UKUMBI WA TCC - CLUB CHANG'OMBE KUTUMIKA KUMUAGA MAREHEMU .
 
Mungu aibariki na kuwapa Amani yake familia nzima ya Richard Tambwe Hizza gwiji la siasa za dar es salaam hasa Temeke namkumbuka wkt wa uchaguzi wa mwaka 1995 alipotuletea mtu anaitwa Kihiyo ambaye alikuwa ni mbunge wa kwanza wa ccm kukutwa na vyeti vya kufoji na hiyo ikasabbabisha matoeko kutenguliwa na hivo kutokea uchaguzi mdogo uliopelekea Augustino Mrema kushinda kiti hicho kupitia NCCR MAGEUZI. Kwahiyo bila hiza huenda tusingekuwa na neno Kihiyo hivi leo.

R.I.P Tambwe Hizza
 
Mungu aibariki na kuwapa Amani yake familia nzima ya Richard Tambwe Hizza gwiji la siasa za dar es salaam hasa Temeke namkumbuka wkt wa uchaguzi wa mwaka 1995 alipotuletea mtu anaitwa Kihiyo ambaye alikuwa ni mbunge wa kwanza wa ccm kukutwa na vyeti vya kufoji na hiyo ikasabbabisha matoeko kutenguliwa na hivo kutokea uchaguzi mdogo uliopelekea Augustino Mrema kushinda kiti hicho kupitia NCCR MAGEUZI. Kwahiyo bila hiza huenda tusingekuwa na neno Kihiyo hivi leo
Taarifa zinadokeza kwamba KIHIYO ni miongoni mwa watakaohudhuria .
 
Daaah!
Buriani Tambwe hiza
Nimeanza kumjua tangu 1995 akiwa Mgombea Ubunge wa NCCR Mageuzi ya Mrema na Mabere Marando Jimbo la Temeke

Enzi hizo akiitwa Mshale wa Sumu dhidi ya CCM!

Nimekuwa nae Mara kadhaa kijiweni kwake pale Temeke bustani opposite na Temeke Hospital

Kwake Siasa ilikuwa Tasnia sio Uwanja wa Chuki

Alipohama NCCR Mwaka 1996 nikamuuliza sababu ya kuhama akanijibu kwa utani kuwa kagundua kirefu cha NCCR ni 'Nyerere Chagua Chama na Rais' na Chama cha Nyerere ni CCM so na Mrema ni CCM
 
Msiba wake umenishtua sana hasa ukizingatia kuwa na Mimi ni mwana ' Pumu / Asthma ' mwenzie. R.I.P Richard Tambwe Hizza.
Usistuke ndugu!
Cha Msingi chukua tahadhari husika kulingana na mazingira ya ugonjwa husika japo Siku ikifika haina baunsa

Prof Idrissa Mtulya alikuwa Daktari bingwa wa kwanza wa Moyo Tz na alikufa kwa Matatizo hayo Mwaka Jana
 
Ndiyo umezidi Kunitisha Mkuu.
 
Msiba wake umenishtua sana hasa ukizingatia kuwa na Mimi ni mwana ' Pumu / Asthma ' mwenzie. R.I.P Richard Tambwe Hizza.

Kama uko overweight jitahidi kupunguo na pia jitahidi kucheck afya kila baada ya kipindi fulani.

Mwisho kabisa mrudie Mungu wako kabisa hahahahahah (Just a Joke)
 
Tambwe hizi moja ya magwiji wa siasa za Dar es salaam, Pamoja na ukristo wake alikubalika sana na wana CUF kiasi cha vijana wa Temeke kuwa wendawazimu enzi za CUF ngangali, CUF jino kwa jino, CUF wanaume..

RICHARD TAMBWE HIZA, binafsi namuita mkali wa jukwaa maana ukimsikiliza kwa hisia unaweza kuingia msituni, mara nyingi hotuba zake hugusa sana vijana wa mtaani maana anajua namna ya kuongea nao na hisia zikawajia juu ya nchi yao.

RIP TAMBWE HIZA "mtoto wa mjini" Tandika sudani, Temeke mwembe yanga na TMK na wanaDarisalama tutakumiss sana, "Binafsi namuomba MWENYEZI MUNGU mkuu wa ardhi na mbingu zote akupumzishe mahala pema na akusamehe mazambi yako yote. "
 
Mwaka 2000 kwny Uchaguzi Mkuu alipambana na Hadija Kusaga Mgombea wa CCM, kwa kweli tulimshinda kwa taaabu kweli kweli, hasa maeneo ya Azimio, Mtoni kwa Azizi Ally
 
Mazishi yamefanyika salama na tumekusanyika nyumbani kwenye maombolezi nyumbani kwa marehemu Mbagala
 
Hadija kusaga hakumshinda tambwe bali alitangazwa mshindi tu .

Hata Kikwete pia "ilisemwa" hakumshinda Slaa bali alitangazwa Mshindi tu 2010

Hata 1995 kwa Watu wazima wenzangu wanakumbuka pia Wapinzani walienda Mahakamani kusema Mkapa Kawaibia kura

Hakuna Mbunge wa CCM alieshinda bila ya 'kusemekana' aliiba kura

kwa kifupi Majimbo yote 'inasemekana' CCM ilishindwa ila tu ilitangazwa Washindi
 
Kama uko overweight jitahidi kupunguo na pia jitahidi kucheck afya kila baada ya kipindi fulani.

Mwisho kabisa mrudie Mungu wako kabisa hahahahahah (Just a Joke)
"Atubu" ?
Mmoja aliambiwa "Atubu" lakini aliyekumbushia hilo alianza kuchunguzwa kama analipa kodi.

Sasa wewe unashauri mutuz ikapime afya.
 
Back
Top Bottom