TANZIA Kagera: Padre Ireneus Mbahulira(79) amezikwa leo katika makaburi ya mapadre Seminarini Rubya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
MAMIA WAMLILIA PADRE IRENEUS MBAHULIRA

Padre Ireneus Mbahulira(79) amezikwa leo katika makaburi ya mapadre Seminarini Rubya Jimbo Katoliki la Bukoba.

Mazishi yake yameudhuriwa na Maaskofu Desiderius Rwoma, Methodius Kilaini na Askofu Almachius Rweyongeza wa Jimbo Katoliki la Kayanga. Kuliudhuriwa pia na mapadre wapatao 70, masista 50 na mamia ya waombolezaji.

Ibada ya misa ya mazishi iliyoongozwa na Askofu Rwoma. Ilianza majira ya saa 5.15 asubuhi. Kwaya ya Seminari ya Rubya iliongoza nyimbo. Waliimba misa ya Kilatini.

Katika mahubiri yake yaliyochukua dakika 14 askofu Rwoma alimshukuru Mungu kwa maisha ya padre Irene na kusisitiza haja ya kila mtu kujiandaa.

Masomo yalitoka Kitabu cha Wamakabayo, Waraka kwa Wathesalonike na Injili ya Mathayo kuhusu Wanawali kumi. Askofu Rwoma alisema kwa Mungu hakuna kifo cha ghafla.

Padre Ireneus alizaliwa kijijini Igurugati Parokia ya Bugandika tarehe 16.10.1942 na kufariki tarehe 22.01.2021 hospitalini Mugana alikokuwa amelazwa kutokana na matatizo ya kubanwa kifua. Hadi mahuti yake Padre Irene alikuwa Paroko Msaidizi Parokia ya Minziro, parokia aliyoamia akitokea parokiani Rukindo mwezi Septemba mwaka jana. Padre Irene alirejea jimboni Bukoba akitokea Jimbo Kuu la Dar es Salaam alikofanya utume wake kwa miaka mingi. Padre Irene katika maisha yake kama padre amehudumu katika Parokia 17 katika majimbo ya Bukoba, Arusha na Dar es Salaam.

Pia katika maisha yake alisomea Uandishi wa Habari na Utangazaji huko Kenya miaka ya 70. Aliporejea Tanzania alifanya kazi katika Kitengo cha Habari Baraza la Maaskofu Tanzania.

Katika hotuba zao walioongea hapo kanisani Rubya baada ya Misa akiwemo Askofu Kilaini na Padre Faustine Kamugisha(Paroko Minziro) walimwelezea marehemu Padre Irene kama mtu aliyekuwa mcheshi na mtu mwema wa kuishi naye.

Padre Faustine Kamugisha alipopata nafasi ya kuongea alisimulia mengi kuhusiana na maisha ya marehemu wakati wa uhai wake hapo Minziro, kuugua kwake alivyopelekwa Hospitali ya Kajunguti, baadae kurudishwa Minziro na hatimaye kupelekwa hospitalini Mugana ambako alifia. Haya yote yametendeka kwa kipindi kifupi sana. Padre Faustine amekabidhi shilingi 200,000/= kwa Askofu Rwoma kama rambirambi ya Parokia ya Minziro kwa Baba Askofu. Waliotoa rambilambi wengine ni Umoja wa Mapadre ambao walikabidhi bahasha ya pesa kwa mwakilishi wa familia ya marehemu Bwana Richard Muyungi, ingawa kiwango cha pesa hakikutajwa.

Askofu Kilaini wakati wa kutoa neno lake alitoa maneno ya rambirambi Kutoka kwa mapadre kadhaa wa Dar es Salaam na maaskofu mbalimbali kutoka majimbo ya Tanzania.

Askofu Alimachius Rweyongeza naye alitoa neno lake la pole kwa wafiwa na rambirambi kwa Askofu Rwoma.

Msemaji wa familia ya marehemu Bwana Richard Muyungi katika neno laki alisema kuwa Padre Ireneus ameiinua familia yao. Maneno hayo yamedhihirishwa na uchungu ulioonyeshwa na baadhi ya wanafamilia wakati wa kushuhudia na kumuaga marehemu na kutoa mchango misa. Wanafamilia wengine walipiga mayowe na wengine kutolewa nje na kuzimia.

Katika kushughulikia mwili wa marehemu hapo kanisani Sr, na muhudumu mwingine kutoka hospitalini Mugana na pia mapadre wa Seminari waliobeba mwili wa marehemu kuuweka kwenye gari baada ya misa hapo kanisani kuupeleka makabulini walivalia barakoa.
Kutoka Minziro lilikuwa ni kundi kubwa la watu. Minziro walikuja na kikundi cha kwaya ambacho kilikuwa kimevalia nguo nyekundu. Kilipata nafasi ya kuimba wimbo mmoja wakiganda baada ya komunyo.

Kaburi alimozikwa marehemu Padre Irene lilikuwa limejengwa vyema. Kuweka udongo ilikuwa ni kupitia wawakilishi.

Mapadre waliwakilishwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Mapadre jimboni Pd Paschal Mutegaya, Pd Adeodatus RWEHUMBIZA (Chancellor), maaskofu, masista wakuu wa Mashirika na baadhi ya wanafamilia akiwemo Pd Benezeth Rwegoshora, Achilleus RWEHUMBIZA, Sr Amelberga, na Sr Praxeda.

Baada ya shughuli za mazishi hapo makaburini kulifuatia huduma ya chakula kwa maaskofu, mapadre, masista na wanafamilia.

Shughuli ya mazishi imemalizika majira ya saa nane kasoro dakika mbili mchana. Hapo kesho majira ya saa tano asubuhi itasaliwa misa ya kuanua matanga nyumbani kwao Igurugati kwa Mzee Nazari marehemu babake. Na Pd Charles RWEHUMBIZA.

2675743_FB_IMG_1611611762374.jpg
 
FB_IMG_1611611781628.jpg

Tungepata picha ingekuwa vizuri zaidi. Apumzike kwa amani
Rev. Fr. Ireneus Kaganda Mbahulira was born at Igurugati Bugandika Parish in Bukoba diocese on 16 October 1942. After Std, IV he joined Bunena preparatory Seminary, then Rubya junior Seminary up to STD XII (Now known as Form IV). In 1964 he joined Ntungamo the newly built Major Seminary in Bukoba. In 1967 when Ntungamo became a national Major Seminary he moved to Kipalapala where he finished his theology.

He was ordained a priest on 7 December 1969. He did his pastoral work in Bukoba, he was parish priest of Buyango parish for some years; when he moved to Dar es salaam he worked in Changombe parish, was Parish priest of Mafia parish and for a number of years he worked in Kibiti parish.

On 22ndDecember 2018 he decided to come back to his home diocese of Bukoba to finish his pastoral there. He first worked in Rukindo parish and now he was in Minziro Parish.

He attended the last priests retreat and on 9thJanuary 2021 at the closure of the retreat the young priests were joking with him asking him to do push ups. He responded joyfully rising up and down. This was the last time many of us saw him alive and vigorous.

He was a very friendly priest, ready to do any job he was given. He had wonderful relations with all and the people appreciated him.
He was admitted in Mugana hospital but soon his situation worsened and the priests gave him the last sacraments. On 22 December night he passed away.

As for me I knew him as he was my table prefect when I was in STD VIII and he was in STD IX. He was very kind and considerate. From then on we were close friends as we were both of the Baihyuzi clan our families linked up. Goodbye dear Mbahulira may the L
 
Ufu 14:13

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

Tujitahidi kufanya mazoezi.
 
Back
Top Bottom