Ijue siku ya wapendanao - ”Valentine’s day”

Sep 14, 2014
65
45
Na Reagany Mchome

14 Februari kila mwaka ni siku inayopambwa kwa rangi nyekundu za maua ya waridi, makadi ya maamkizi, zawadi na alama ya “kopa” inayotambulika kuwakilisha upendo.

Ni siku maarufu inayotumika na watu wengi kudhihirisha upendo kwa wenzi wao na wapendwa wao wengine kwa kuwaeleza au kuwapatia zawadi zinazosisitiza upendo wao kwao.

Mtazamo juu ya siku hii umepitia mabadiliko ya karne nyingi tangu asili ya kuanza kwake hadi sasa katika karne hii ya 21. Hata hivyo pamoja na ugwiji wa siku hii ambayo karne za hivi karibuni imeonekana kama “siku ya mapenzi”, historia ya kuadhimishwa kwake imekuwa adimu kwa watu wengi.

ASILI

Siku ya Valentine (Valentine’s Day) au Siku ya Mtakatifu Valentine au pia Sikukuu ya Mtakatifu Valentine iliasisiwa kama siku ya heshima ya kumkumbuka Padre wa karne ya 3 wa Kanisa Katoliki aitwaye Valentine ambaye karne ya 5 alipewa rasmi hadhi ya kuitwa Mtakatifu na Papa Gelasius wa kwanza mwaka 496, kwa mujibu wa taratibu za Kanisa. Padre huyo aliuawa siku ya tarehe 14 Februari 269 na hivyo tarehe hiyo ilitengwa kwa heshima ya kukumbuka kifo chake. Maadhimisho ya siku yake yalianza punde baada ya kusimikwa utakatifu mwaka 496, karne mbili baada ya kifo chake.

Kuna watakatifu watatu wanaohusishwa na siku hiyo wenye majina ya Valentine ambao wote waliuawa tarehe 14 February. Mmoja ni Mtakatifu ambaye aliuawa katika jimbo la utawala wa Rumi lililokuwa Afrika (eneo la jimbo hilo lilihusisha eneo la sasa la nchi ya Tunisia, eneo la kaskazini mashariki mwa Algeria na eneo la pwani ya kaskazini magharibi mwa Libya). Hata hivyo hakuna maelezo mengi zaidi yanayomuelezea Mtakatifu huyo.

Wengine wawili wanaohusishwa na siku hiyo ni Paroko wa Interamna (Eneo ambalo kwasasa linaitwa Terni huko nchini Italia). Paroko Valentine wa Interamna aliuawa chini ya utawala wa Aurelian mwaka 273 na kuzikwa nje kidogo ya jiji la Roma katika eneo la Via Flaminia. Na wa mwisho anayehusishwa na siku hiyo ni Padre wa Kanisa Katoliki aliyeishi jiji la Roma ambaye aliuawa chini ya utawala wa Claudius wa pili mwaka 269, na kuzikwa nje kidogo ya jiji hilo katika eneo la Via Flaminia kwenye kanisa la San Valentino. Mabaki ya Padre huyu yalihamishiwa katika kanisa la Santa Prassede wakati wa utawala wa Nikolas wa nne.

Japo baadhi ya wanahistoria wanaamini kuwa Valentine wa Roma na Valentine wa Terni ni mtu mmoja kutokana na rekodi za kanisa kuonyesha uwepo wa Valentine mmoja tu aliyezikwa Via Flaminia, wawili hao wanasadikika kuzikwa katika makaburi mawili tofauti ya eneo la Via Flaminia.

DHANA MBALIMBALI ZA KIFO CHA PADRE VALENTINE

Kuna dhana mbalimbali zinazoelezea chanzo na kifo cha Padre Valentine. Hata hivyo zipo dhana tatu zinazofahamika zaidi.

• Inasemekana Mtawala Claudius wa pili aliweka msisitizo kwa vijana kutokuingia kwenye mahusiano ya ndoa na badala yake kujiunga na jeshi ili kupigana vita. Mtawala huyo aliamini kuwa askari wakiingia katika ndoa hupungua ufanisi wa kutumikia jeshini. Na badala yake askari wasio na majukumu ya ndoa huwa wafanisi zaidi jeshini.

Inasemekana kuwa Padre Valentine hakuunga mkono dhana hiyo, hivyo aliwasaidia vijana na kuwafungisha ndoa kwa siri. Mtawala Claudius II aligundua na hivyo aliamuru Padre Valentine kukamatwa na kusekwa gerezani. Padre huyo alihukumiwa kifo na kuuawa tarehe 14 Februari 269.

• Dhana ya pili, inasemekana kuwa Padre Valentine alikuwa akiwasaidia wakristo kutoroka mateso yaliyokuwa yakiwaandama kutoka kwa watawala wa rumi. Kuwasaidia wakristo ilikuwa kosa la jinai kwa watawala wakati huo hivyo alikamatwa na kuhukumiwa kifo, aliuawa tarehe 14 Februari mwaka 269.

• Dhana ya tatu, inasemekana kuwa Padre Valentine alikamatwa kwa ajili ya imani yake juu ya ukristo, akiwa mikononi mwa mtawala Claudius II alishawishiwa na mtawala huyo kuikana imani yake juu ya Yesu Kristo na kujiunga na imani za kipagani. Padre huyo alikataa na kumshawishi mtawala Claudius II kuiamini imani ya ukristo. Mtawala huyo alikasirika na kuagiza Padre Valentine afungwe na kuhukumiwa kifo. Aliuawa tarehe 14 Februari mwaka mwaka 269.

Ufafanuzi wa dhana zote tatu unaeleza kuwa wakati fulani wa kifungo cha Padre Valentine alifanikiwa kumuombea binti aliyekuwa na upofu aitwaye Julia, mtoto wa Jaji Asterio. Jaji Asterio ndiye aliyekuwa msimamizi wa gereza alimofungwa Padre Valentine. Baada ya binti huyo kupona upofu, Jaji Asterio aliipokea imani ya kikristo ya Padre Valentine na kuridhia kubatizwa pamoja na familia yake yote na watu wengine 44 waliokuwa katika himaya yake.

Inasemekana zaidi kuwa kabla ya kuuawa, Padre Valentine alimuandikia salamu Julia (Mtoto wa Jaji Asterio) ambaye hata hivyo alikuwa akimtembelea gerezani na Padre aliandika maneno “kutoka kwa Valentine wako” (From your Valentine) katika ujumbe huo. Maneno hayo yanasemekana kuwa chanzo kikubwa cha jumbe za siku ya wapendao hata leo.

UHUSIANO NA SIKUKUU YA LUPERCALIA

Sikukuu ya Valentine inahusishwa pia na sikuukuu ya kipagani ya lupercalia. Sikukuu ya lupercalia iliyokuwa ikifanyika tarehe 13 hadi 15 Februari ilikuwa sikuukuu maalum ya kipagani katika utawala wa rumi kwa ajili ya kufanya matambiko ya kufukuza roho chafu na kusafisha jiji la Rumi. Sikukuu hiyo pia ililenga kuleta afya njema na rutuba ya uzazi kwa wanajamii wote na mazao.

Matambiko hayo yalifanyika kama ibada kwa mungu wa kipagani “februus” ambaye mwezi huo ndio ulikuwa mwezi wake yaani “mwezi wa februus” ama kwa kiingereza “of february”. Mungu huyo wa kipagani ndiye chanzo cha jina la mwezi wa pili “february”. Matambiko pia yalielekezwa kwa waanzilishi wawili wa utawala wa Rumi ambao ni Romulus na Remus.

Matambiko yalihusisha kafara ya mbuzi, mbwa na keki. Wanawake waliotaka kupata ujauzito walichapwa kwa kutumia ngozi ya mbuzi aliyetolewa kafara. Kwa kuanza matambiko, viongozi wa dini ya kipagani walikutana katika pango linalodaiwa kuwa waanzilishi wa Rumi walikaa na kutunzwa na mbweha wa kike “lupa”. Viongozi hao walitoa kafara ya mbuzi kwa ajili ya rutuba na mbwa kwa ajili ya utakaso. Ngozi ya mbuzi ilizamishwa kwenye damu ya kafara na kwenda kuwachapa wanawake wote waliotaka kupata watoto, na mimea kwa ajili ya rotuba ili kupata mavuno makubwa.

Jioni ya siku hiyo wanawake wa rumi wasiokuwa kwenye ndoa wala mahusiano waliandika majina yao kwenye karatasi na kuyaweka katika chungu kikubwa ambako wanaume wangekuja na kuokota vikaratasi hivyo. Kila mwanaume alikuwa anamchukua mwanamke ambaye jina lake limo kwenye kiratasi alichookota. Wawili hao waliungana na kuwa wapenzi kisha baadaye wangeoana.

Hivyo sikukuu hiyo (13 — 15 februari) pamoja na kuwa na ibada ya kipangani ya utoaji wa kafara ilikuwa msimu muhimu kwa mahusiano mapya ya kimapenzi kwa wanajamii wa Rumi.

SIKU YA VALENTINE KAMA SIKU YA MAPENZI/ WAPENDANAO

Inasemekana kuwa sikukuu ya Lupercalia ilikuwa chanzo cha uhusiano wa siku ya kumuenzi Mtakatifu Valentino aliyeuawa 14 februari na siku ya wapendanao kama ambavyo tunaiadhimisha siku hizi.

Sikukuu ya kipagani ya Lupercalia ilififia zaidi katika utawala wa rumi mwishoni mwa karne ya tano (kati ya 492–496) na kufutwa/ kupigwa marufuku kuwa haikuwa ya kidini na Papa Gelasius I baada ya kutangazwa rasmi na kanisa kuwa 14 february itakuwa kumbukizi ya Padre Valentine ambaye mwaka 496 alitambuliwa rasmi kuwa Mtakatifu kwa mujibu wa taratibu za kanisa Katoliki.

Hata hivyo siku ya mtakatifu Valentino ilibaki kuwa siku ya kidini kwa kanisa katoliki pekee, baada ya kuamka kwa uprotestant, baadhi ya madhehebu ya kiprotestant yaliendelea kuienzi pia kwa mantiki hiyo hiyo. Kwa madhehebu ya Lutheran, Anglican, Kanisa la Uingereza (Church of England) na baadhi ya madhehebu mengine ya kiprotestant siku hiyo inaendelea kukumbukwa kidini kama siku ya mtakatifu Valentino katika tarehe 14 februari. Kwa madhehebu ya Kanisa la Eastern Othordox tarehe 6 July ndio hutumika kumuenzi Padre Valentine aliyeishi Roma na tarehe 30 July hutumika kumuenzi Paroko Valentine wa Terni.

Hamasa ya kuifanya siku ya valentine kuwa siku ya mapenzi au siku ya wapendanao iliongezeka zaidi katika zama za kati (karne ya 5 hadi karne ya 15). Katika nchi za Ufaransa na Uingereza ilitambulika kuwa februari 14 ilikuwa mwanzo wa msimu wa kujamiiana wa ndege. Hii iliongeza zaidi dhana ya kuifanya siku hiyo kuwa siku ya kimapenzi katika tawala za uingereza.

Mshahiri wa uingereza Goeffrey Chaucer ndiye wa kwanza kuinakili rasmi siku hiyo kama siku ya kimapenzi karne ya 14 (kati ya mwaka 1375 hadi 1382) kwenye ushahiri wake ulioitwa “Bunge la ndege” akiandika kuwa “Kwakuwa hii iliagizwa katika siku ya mtakatifu Valentine ambapo kila ndege huja kuchagua mwenzi wake”.

Shairi hilo liliandikwa kwa heshima ya kuenzi anivesari ya kwanza ya uchumba wa mfalme wa uingereza Richard II na mkewe Malkia Anne. Ushahiri huu ni miongoni mwa vielelezo vya mwanzo zaidi vilivyoifanya siku ya mtakatifu Valentine kuwa siku ya wapendanao.

Inasadikika kuwa kabla ya kipindi hicho hakukuwa na utaratibu rasmi ulioifanya siku ya kumuenzi mtakatifu Valentine kuwa siku ya wapendanao. Mwishoni mwa karne ya 15 (mwaka 1400) mfalme Charles VI wa Ufaransa aliandika waraka rasmi “Waraka wa Mahakama ya Mapenzi” ulioanzisha mahakama ya mapenzi na ulioorodhesha sikukuu za upendo ambazo zingepaswa kuhudhuriwa na wajumbe wa mahakama ya kifalme.

Waraka huo uliiorodhesha tarehe 14 februari kama sikuukuu ya wapendanao, ambapo sherehe ingefanyika na kungekuwa na mashindano ya kuimba nyimbo, kusema mashairi na kucheza. Katika sikukuu hiyo wanawake waliohudhuria wangesikiliza kesi na migogoro ya wapendanao (watu waliokuwa kwenye mahusiano) na kuzitatua. Mahakama hivyo ilihudhuriwa na malkia Isabeau (mke wa mfalme Charles VI)

SIKU YA WAPENDANAO KATIKA KIPINDI HIKI CHA UTANDAWAZI

Mabadiliko ya kimtazamo juu ya siku hii yamebadilika zaidi katika kipindi hiki cha utandawazi. Siku hii imezidi kuhama kutoka kwenye asili yake (karne ya 5) na kutoka kwenye mtazamo wa mahusiano ya kimapenzi pekee (karne ya 15) na sasa hutumika zaidi kuwakilisha upendo zaidi ya ule wa kimahusiano. Wengine huitumia kuwasilisha upendo kwa marafiki, ndugu na wazazi. Siku hii pia huambatana na zawadi za maua, makadi, jumbe za upendo na sherehe za kujivinjari ama mitoko ya kwenda kufurahi pamoja.

Mpaka kufikia karne ya 17 siku hii ilishika kasi zaidi katika maeneo ya utawala wa uingereza. Karne ya 18 watu walikuwa wakipeana kadi za kuandika kwa mkono zikiwa na jumbe za upendo kwa ajili ya marafiki na wapendwa wao. Kuanzia mwishoni mwa karne ya 19 hadi karne ya 20 kadi za kuchapishwa zilianza kutumika na watu walikuwa wakinunua na kuwazawadia wapendwa wao. Esther A. Howland ndiye alianzisha kadi za kwanza za kuchapisha nchini marekani mwaka 1840, mama huyo anajulikana kama “Mama wa Valentine” nchini humo.

Makadi kwa ajili ya siku hii hutumia nembo ya kerubi mtoto aliyeshika upinde na mshale aitwae “cupid”. Cupid ambaye ni mungu wa kipagani aliwakilisha upendo, mvuto na hisia za mapenzi. Wazazi wake ni mungu mars wa kipagani na mama yake ni mungu wa kike wa upendo aitwaye venus. Cupid anafahamika zaidi kama mungu wa mapenzi katika dini za kipagani na kigiriki.

Siku hii ya wapendao pia hutumika kibiashara katika mataifa mengine. Nchini Marekani matumizi kwa ajili ya zawadi za Valentine yanatarajiwa kuweka rekodi mwaka huu 2020 na kufikia dollar billion 27.4 (trillion 6.3 za kitanzania) na hivyo kuvuka rekodi ya matumizi ya mwaka jana dollar billion 20.7 (trillion 4.8 za kitanzania).

Hatua hiyo imepelekea kuinuka kwa wanaharakati wanaopinga kuadhimishwa kwa siku hiyo katika nchi hiyo. Wanaharakati hao pia wameangazia matumizi mabovu ya siku hiyo baada ya mara kadhaa kukamatwa kwa maboksi ya maua ya waridi yanayotumika kusafarisha madawa ya kulevya.

Nchini Tanzania, siku ya wapendao hutumika zaidi kutakiana heri, na kukumbushana upendo kwa ndugu jamaa na marafiki. Hutumika pia na wapenzi kujivinjari katika maeneo ya starehe na kwa ajili ya shughuli za kijamii na kutoa huduma za kijamii.

Pamoja na udhahiri kuwa katika maeneo mengi siku hii imetelekeza dhana ya awali ya kuanzishwa kwake, kwa wanajamii wengi imeendelea kuwa siku ya kielelezo cha upendo kwa wenzi, ndugu, jamaa na marafiki.

Ni muhimu pia kujielemisha kuwa ni vyema kutumia kila siku kuonyesha upendo kwa watu waliokuzunguka, kuwaeleza juu ya nafasi waliyonayo kwako na kuwazawadia wakati wowote upatapo fursa ya kufanya hivyo. Upendo wako kwa wanajamii wenzio usisubiri 14 februari pekee, utawanye kila siku ya maisha yako.

(Unaweza kuandika maoni yako au ushauri katika eneo la “response” hapo chini. Ahsante kwa kupitia andiko hili.)
 
Upendo, upendo, upendo ndiyo amri kuu kwetu sisi Wakristu tunayopaswa kuitekeleza hapa Duniani. Ahsante kwa chapisho zuri hakika sijatoka kapa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom