MCL kumejaa majungu, fitna, chuki na Kuna Kujuana Mno, Kiasi Kwamba Kuna Watu Pale Hawaajiriwi Huu Mwaka Wa 10 Sasa, Wanafanya Tu Kama Correspondents. Huku Wengine Wakiwa Retainers Kwa Miaka 9 Sasa, Lakini Cha Kushangaza Anakuja Mtu Leo Baada Ya Miezi 3 Tu Kaajiriwa.
Ila Kwa Kitendo Cha MCL Kununuliwa Waziwazi Na EL Na Kwa Jinsi Alivyo Richard Mghamba, Nilijua Tu Asingeweza Kudumu Pale Kwani Hakuna Kitu Ambacho Richard Mghamba Anakichukia Duniani Kama " RUSHWA " Na " UFISADI " Na Labda Niwakumbusheni Tu Mwandishi Wa Habari Bingwa, Nguli Na ALIYETUKUKA Katika Kuandika Habari Za KIUCHUNGUZI ( Investigative Journalism ) Tanzania Nzima Ni Bwana Richard Mghamba.
Na Miaka Ya 90 Huko Aliwahi Hata Kuhukumiwa Na Mahakama Baada Ya Kuripoti Masuala " NYETI " Ya Nchi.
Waandishi Wengi Wa Sasa Kama Akina Deudetus Balile, Saed Kubenea Na Hata Marehemu Mtani Wangu Edson Kamukara, Wote Walikuwa Wanapita Katika Njia Iliyojengwa Na Richard Mghamba. Hilo Jamaa Ni Jembe Balaa Na Namkubali Hakuna Mfano.
Ushauri Wangu Tu Kwake Ni Kwamba Aijenge Upya The Guardian Limited, Ili Ishindane Na Magazeti Mengine Na Kubwa Zaidi Awajali Wafanyakazi Kwa Kuwajengea Upendo Na Umoja Huku Akiwaboreshea Maslahi Yao. Otherwise Namtakia Kila La Kheri Katika Nafasi Yake Hiyo Mpya. Mkoa Wa Mara Kunapatikana Kila Kitu " Kizuri " Na " Chema ".