Richard Mgamba awa Boss mpya wa The Guardian Ltd

Richard Mgamba awa Boss mpya wa The Guardian Ltd

Siyo kweli soma hapa!

Kampuni ya The Guardian Ltd wapata mkurugenzi mpya.

itv02.jpg





Mkurugenzi mtendaji wa ITV na Radio One amekabidhi rasmi ofisi ya The Guardian baada ya kupatikana kwa mkurugenzi mpya Bwana Richard Mgamba ambaye atakuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya The Guardian Ltd, kazi ambayo ameianza mara moja.
Wakizungumza mara baada ya mkurugenzi mpya kukabidhiwa ofisi na kuanza kazi mara moja, baadhi ya viongozi wa kampuni ya The Guardian Ltd wamesema kuteuliwa kwa Bwana Richard Mgamba kuwa mkurugenzi mtendaji wa The Guardian itasababisha kampuni hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi kutokana na uwezo mkubwa wa mkurugenzi huyo.

Baadhi ya wafanya kazi wa kampuni ya The Guardian Ltd wamepokea kwa mikono miwili uteuzi wa mkurugenzi Richard Mgamba huku wakisema kuwa kutokana na uwezo mkubwa wa Bwana Richard Mgamba, mabadiliko ya kampuni yao yatakuwa makubwa katika tasnia ya habari hapa nchini.

Uteuzi wa Bwana Mgamba umefanywa na mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dakta Reginard Mengi baada ya aliyewahi kuwa mkurugenzi wa kampuni hiyo Bwana Kiondo Mshana kustaafu mwishoni mwa mwaka jana 2014, ambapo mkurugenzi mtendaji wa ITV Radio One Joyce Mhavile alishika nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi sita yaani kuanzia mwezi January hadi June 2015 kabla ya kuteuliwa kwa mkurugenzi mpya Richard Mgamba anayeanza kazi rasmi.
Source ITV habari 02/07/2015

 
Mkuu GENTAMYCINE, Jamaa ulipaswa kumelewesha kwa Lugha yakawaida tu angekuelewa! Kwa mfano yy ameweka Link ya Makala aliyoandika Mgamba, ww aidha ungekanusha kuwa haikuandikwa na yeye au vinginevyo Ila namna hii, daah, Nway
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwa namna hii migogoro kwenye Jamii zetu za kiAFRICA hazitaisha huyo Jamaa ulipaswa kumelewesha kwa Lugha yakawaida tu angekuelewa! Kwa mfano yy ameweka Link ya Makala aliyoandika Mgamba ww aidha ungekanusha kuwa haikuandikwa nayy au vinginevyo Ila namna hii daah Nway

Nimweleweshe Vipi? Alitaka Ligi Na Mimi Wakati Na Mimi Ndiyo Mpenda Ligi " NILIYETUKUKA ".
 
Nilijua Tu Kuwa Poti Wangu Richard Mghamba Asingeweza Kukaa au Kudumu MCL Kwani Ni Mtu Mwenye Misimamo Ya Kimusomamusoma Hivi.

Acha Kukariri Wewe POPOMA! Na Siyo Musoma Sema " Mara ".

1. Sasa hapo POPOMA ni nani?
2. Narudia tena, huyo bwana hana misimamo yoyote ile. Tegemea kupata makala za Kagame kutoka newtimes kwenye Nipashe na Guardian coming soon!
 
Tulimumu, Atii nung'ayembe kwa kiswahili ndo nini?
 
Last edited by a moderator:
kheeee mkuu hebu nijuze kwani aliwafanyaje maaana wengine tuko kushoto na media hizi
Laana Ya Mikidadi Mahmoud Na Hayati Julius Nyaisanga Sasa Zinaanza Kufanya Kazi Kwake. Aliyowafanyia Mwenyezi Mungu Anajua Na Anawalipia Sasa.
 
Wakuu tuwe waelewa jamani tusome bila kukurupuka,Joyce Mhavile anabaki kuwa mkurugenzi wa Itv na Radio one hajaondolewa ila alikua anakaimu nafasi ya Mkurugenzi wa The Guardian .Mtofautishe nafasi hizi jamani mtaumbuka bure.
 
Bad timing kwa Mengi, very bad timing.

Hana uhakika kama Lowassa atapitishwa au la, what if lowasa asipitishwe na huyo atakaepitishwa atamuweka kwenye nafasi gani mengi?

Angesubiri baada ya mchakato wa kuteua mgombea halafu akajiunga na lowasa.

Kwa mfanyabiashara kama Mengi...na aina za biashara anazofanya....ni too powerful to colapse hata aje rais mwenye akili ya Musollini....alichokifanya ali go with the flow....
 
Mimi nina uhakika wa ninachokiongea. Kama nawe una uhakika basi alitoka MCL akaenda The Guardian, akarudi MCL, na sasa anaenda tena The Guardian. Usinitishie mambo ya tasnia wakati unaandika kwa kutumia 'Title case' ktk kila aya. Hii ni makala ya Mgamba akiwa IPP mwaka 2012 I`m ready for peace or war-any time - IPP Media

Mkuu anatumia title case katika kila aya au neno? Kwa kiswahili ambacho nilifundishwa nikiwa darasa la kwanza AYA ni mkusanyiko wa sentensi nyingi nyingi au kwa kiinglishi paragraph. Labda unisaidie kunijuza vizuri inawezekana mi ndo nimesahau maana toka la kwanza miaka ileeeeee ya 47
 
Wakuu tuwe waelewa jamani tusome bila kukurupuka,Joyce Mhavile anabaki kuwa mkurugenzi wa Itv na Radio one hajaondolewa ila alikua anakaimu nafasi ya Mkurugenzi wa The Guardian .Mtofautishe nafasi hizi jamani mtaumbuka bure.

Wameumbuka tayari. Wanahamaki na hawasomi na kuelewa.
 
MCL kumejaa majungu, fitna, chuki na Kuna Kujuana Mno, Kiasi Kwamba Kuna Watu Pale Hawaajiriwi Huu Mwaka Wa 10 Sasa, Wanafanya Tu Kama Correspondents. Huku Wengine Wakiwa Retainers Kwa Miaka 9 Sasa, Lakini Cha Kushangaza Anakuja Mtu Leo Baada Ya Miezi 3 Tu Kaajiriwa.

Ila Kwa Kitendo Cha MCL Kununuliwa Waziwazi Na EL Na Kwa Jinsi Alivyo Richard Mghamba, Nilijua Tu Asingeweza Kudumu Pale Kwani Hakuna Kitu Ambacho Richard Mghamba Anakichukia Duniani Kama " RUSHWA " Na " UFISADI " Na Labda Niwakumbusheni Tu Mwandishi Wa Habari Bingwa, Nguli Na ALIYETUKUKA Katika Kuandika Habari Za KIUCHUNGUZI ( Investigative Journalism ) Tanzania Nzima Ni Bwana Richard Mghamba.

Na Miaka Ya 90 Huko Aliwahi Hata Kuhukumiwa Na Mahakama Baada Ya Kuripoti Masuala " NYETI " Ya Nchi.

Waandishi Wengi Wa Sasa Kama Akina Deudetus Balile, Saed Kubenea Na Hata Marehemu Mtani Wangu Edson Kamukara, Wote Walikuwa Wanapita Katika Njia Iliyojengwa Na Richard Mghamba. Hilo Jamaa Ni Jembe Balaa Na Namkubali Hakuna Mfano.

Ushauri Wangu Tu Kwake Ni Kwamba Aijenge Upya The Guardian Limited, Ili Ishindane Na Magazeti Mengine Na Kubwa Zaidi Awajali Wafanyakazi Kwa Kuwajengea Upendo Na Umoja Huku Akiwaboreshea Maslahi Yao. Otherwise Namtakia Kila La Kheri Katika Nafasi Yake Hiyo Mpya. Mkoa Wa Mara Kunapatikana Kila Kitu " Kizuri " Na " Chema ".
Ngoja tutaona lakini kwa ninavyomjua Mengi huyu bwana hatadumu pale..Mengi ni kinyonga na bandidu wa kutupwa unamkumbuka yule mama wa kihindi(nimemsahau jina) jinsi walivyokuja kutafautiana baadae?
 
Back
Top Bottom