REVIEW: Makosa matano (5) yaliyoonekana kwenye video ya muziki ya Inauma ya msanii Aslay

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
Imechambuliwa na kuandikwa na Ally Nassor Px .

Tarehe 6 February 2023.

Sehemu ya kwanza kuipost ni hapa JF Lakini pia nitaipost Twitter.

____________________________________

Video imetoka majuzi Tarehe 3 mwezi wa pili mwaka 2023.

Ikiwa imeongozwa na director Majagi.

Mpaka sasa tarehe 6 mwezi wa pili 2023 video hii ina jumla ya watazamaji
385K

Twende moja kwa moja kwenye uchambuzi wa video yenyewe.

Video ni kali sana kwa upande wangu naipa rate ya 8.8 / 10. kuna baadhi ya makosa ya ufundi yalionekana kwenye video lakini hauwezi kuyaona mpaka utulie ila mimi nataka nikuoneshe.

.........................................................

1. AINA MOJA YA GARI KURUDIWA RUDIWA NDANI YA VIDEO MUSIC ZAIDI YA TANO (5)

Kama utakuwa mfatiliaji wa music video za Bongo fleva hilo gari sio geni sana kwenye macho ya wafatiliaji.

Hii gari kwanza kabisa imeonekana kwenye video hii ya ASLAY ~Inauma sekunde ya 1 (00:01)
Screenshot_20230205-233324.png


Gari imeoneka kwenye music video ya MWANA FA ft MAUA SAMA ~ Gwiji
Screenshot_20230205-225549.png


Gari imeonekana kwenye music video ya PATORAKING ft DIAMOND PLATNUMZ ~Kolokolo.
Dakika ya 1 ( 01: 37)
Screenshot_20230206-081827.png


_____________________
Gari imeonekana kwenye music video ya STAMINA ft BANANA ZORO ~ Ukizaliwa .
Dakika ya (4 :20)
Screenshot_20230205-222118.png


Lakini pia gari hii hii imeonekana tena kwenye music video ya STAMINA ft LODY MUSIC ~ Hayana maana sekunde ya kwanza tu (00:01)

Screenshot_20230205-221919.png


• Hapa kwa stamina sina maelezo nae zaidi maana story ya nyimbo ilitaka gari na mazingira yale yale
_____________________

hapa naona kilichofanyika ni kuchange plate na za gari tu

Kwenye Ukizaliwa ilisoma - T 125 DFF

Kwenya Hayana maana ikasoma - MBUZI MAKONGO JUU

Lakini kwenye Gwiji ikasoma tena - T 125 CFF.

Kwa upande wa gari moja kuonekana ndani ya video takribani 6 sijaelewa kuwa madirector au ni wasanii wanayapenda sana aina za magari sample moja au aina nyingine za magari hakuna au ni rahisi sana kulipata hili gari.
.........................................................................

2. MUHUDUMU MKUU KUONGEZA SAUTI TV NA KUSIKILIZIA SAUTI TV AMBAYO HAIJAWASHWA KABISA / OFF KABISA

Kama utakuwa makini sekunde ya 6 ( 00: 06 ) anaonekana yule muhudumu akiwa Mgahawani (restaurant), mama aliekuwepo counter akiongeza Sauti Tv.

Screenshot_20230205-152111.png


Lakini Sekunde ya 8 ( 00: 08) anaonekana anaisikiliza sauti ile Tv ambayo haijawashwa kabisa.
Screenshot_20230205-152121.png


...........................................................................

3. TV ILE ILE YA RESTAURANT INAONEKANA TENA SALON

Hapa inakuwa ngumu kuelewa ile TV ni ya kule restaurant au
IMG-20230205-WA0005.jpg


Salon
IMG-20230205-WA0006.jpg


na pia tena na huku haijawashwa. kulikuwa hakuna ulazima wa TV kuonekana tena salon japo sikuelewa pia kulikuwa na ulazima gani wa TV kuwepo sehemu mbili tofauti.

...........................................................................

4. LOCATION MOJA KWENYE VIDEO MBILI TOFAUTI

Kama mfatiliaji sana basi utagundua kuwa location ya restaurant moja imeonekana kwenye video mbili tofauti kwanza imeonekana kwenye Music video ya;

PHINA ft RUBY ~ Number one
IMG-20230206-WA0000.jpg


lakini pia location hii imejirudia tena kwenye hii video music ya ASLAY ~ Inauma.
IMG-20230206-WA0001.jpg

Hapa nashindwa kumuelewa director kuwa tuna uhaba sana wa location au alikuwa ajiamini kwenye kuchagua location.
_____________________

NB; Lengo la kuandika uzi huu sio kukosoa na kuishusha hadhi video ya msanii husika ila ni kukumbusha uwepo umakini zaidi kwa waongozi (Madirector) na Team crew nzima.

Nadhani Msanii husika hana kosa katimiza wajibu wake kwa asilimia kubwa sana kaimba nyimbo kali lakini pia ka act vizuri sana kwenye video kwa maelekezo ya director.
 
Katila kipengele cha Saloon nadhani kuna UNISEX SALOON ambazo huwa zinawajumuisha jinsi zote(Men& Women). So hapo sioni kosa sana, ila kwengine kunawezekana kweli kuwa na mapungufu.
 
Back
Top Bottom