Hivi vyombo vya dola mbona kimya havijaanza kamata kamata wezi hawa? Najua tu siku wakianza, 90% ya wahusika watakuwa nje ya nchi. Ila wakumbuke kitu kimoja -- wakikimbilia marekani au EU watarudishwa tu ku-face justice here!
Duuh....hii kweli ni clue 1.
Wazungu huwa hawakurupuki asee. Mpaka wamechukua hatua nzito ya kusimamisha Budget support wameshafanya uchunguzi wao na wamejiridhisha uwepo wa ufisadi.
Ole wake sasa serikali wakijifanya kuingilia report hii na kuichakachua kama hawajaumbuka, watu wana facts zao siku nyiiingi.
Lakini ni aibu sana kwa Taifa hiki. Yaani mpaka mzungu ndo anakuja kuwa na uchungu na affairs za kwetu?. Sijui tumelaaniwa wapi hata hii nchi! Tanzania is tragedy country!
Asante mkuu kwa Taarifa, lazima serikali ivuliwe nguo kwa sababu imezoea ujinga kila siku na kila dakika yenyewe inawaza wizi tu wa pesa zetu.
Wenzetu Uganda wanatengeneza MAGARI kutuuzia sisi tunawaza kuiba na kuendeleza ujinga tu bila kuangalia maisha ya baadae ya TAIFA letu yatakuwaje.
Lazima Waziri Mkuu na wenzake wajiuzulu, nimechoka kusikia hizi habari za IPTL, RICHMOND, MEREMETA, EPA nk.
Mkuu MANI itakuwa poa sana hili likiwezekana maana wahuni na mafisadi ndani ya hii Serikali dhalimu hawalali ili kuhakikisha ripoti hii inachakachuliwa au haiwasilishwi Bungeni ili ijadiliwe kwa kina.
Na yule muhindi mmoja wa wahusika wa wizi huu mkubwa aliyeanza kutoa rushwa nchini haonekani tena hadharani si ajabu kishatoroka nchini.
Sakata la IPTL likiwekwa wazi Kama lilivyokuwa nchi inaweza kusimama....
mkuu nilikuwa najiuliza kwanini Werema anauwa mkali kiasi kile kwa kulazimisha swala hilo lisiongelewe, wakishirikiana na Makinda wali jitahidi sana kumzuia Kafulila asiliongelee swala hili, hadi Werema akamwita "TUMBILI"
Kwa nini wanaleta kila mara hii kinga ya kwamba hela siyo za umma - yaani hata EPA walisema siyo hela za umma. Haya, hata kama siyo za umma, basi ndiyo majizi machache wajichotee? Wizi wowote si wizi tu?
Wakiiba raia ndio wezi mkuu wao wana a.k.a wanajiita wala rushwa au mafisadi asee ila kwa hapa ni lazma pachimbike mkuu.
Hivi hii nchi ni yatima?!
Ziwekwe bilioni 306 halafu tanesco wadai bilion 321 kivipi wakati zilizokuwepo tangu mwanzo ni bilioni 306?
Sakata la IPTL likiwekwa wazi Kama lilivyokuwa nchi inaweza kusimama....
That not enough,this massive theft must go done with the government na chama chao,people this is it there is no tomorrow.
mwizi ni mwizi tu awe mkubwa au mdogo ilmradi kuna ushahidi wa hilo