Revealing: TANESCO inaidai IPTL Tshs Bilioni 321...

Revealing: TANESCO inaidai IPTL Tshs Bilioni 321...

Ziwekwe bilioni 306 halafu tanesco wadai bilion 321 kivipi wakati zilizokuwepo tangu mwanzo ni bilioni 306?
 
Jesus....Akaunti ilikuwa na bilioni 306 ......good enough hizi zilikuwa ni fedha za umma.....mbaya zaidi Tanesco inaidai IPTL bilioni 321.......hakika nawaambia....hii ngoma italeta historia mpya nchi hii.........kama bado kuna Watanzania waliobaki na chembe za uzalendo lazima tusimama pamoja sasa kuliko wakati wowote......

Hakuna kitu kipya hapo ripoti imeshapikwa imeshapikwa kwa maelekezo mazito. Hii habari kutoka jikon lets wait
 
mhuuuu......!!!? mashaka makubwa .mkuu mjepo nilimweleza jana, yako wapi sasa aibu imemshika na anasoma uzi huu kama guest.

Nimejikuta nikicheka MKUU japo sio mazuri haya yanayotokea yani jamaa anasoma na hawezi kuchangia lolote itabidi afanye registration upya JF ili aweze kuchangia kwa jina jingine tofauti.

I see, kweli hii ndo HOME OF GREAT THINKERS.
 
Huyo bwe.ge wakutiwa ndani pamoja na majambazi wenzake waliohusika, tatizo bado watanzania hawajitambui

Watz bado sana kama richmond kwenyewe EL ndie aliekuwa kinara lakini sasa ndie wanampigia chapuo! huu upuuz wote unafanyka kwa upuuz wetu.
 
Hakuna kitu kipya hapo ripoti imeshapikwa imeshapikwa kwa maelekezo mazito. Hii habari kutoka jikon lets wait

Endeleeni kujidanganya ripoti wanayo wazungu sasa nyie tudanganyeni sisi nakwambia mpaka kieleweke lazima mrudishe hizi pesa lasivyo mnaiweka nchi kwenye matatizo makubwa mnayoyasikia yakitokea kwenye nchi za wwenzenu mtayasikia Tanzania.eti kisiswa cha Amani washenzi wakubwa.
 
Nahisi kwenda choo hii report imekaa vibaya kwa chama dume
 
Ziwekwe bilioni 306 halafu tanesco wadai bilion 321 kivipi wakati zilizokuwepo tangu mwanzo ni bilioni 306?

Soma maelezo vizuri utaelewa tu. Kwanza kuna overpayment 2002-2006, kuna overpayment 2006-2012 zilioenda Escrow account (hii ni tofauti na total payment iliyokuwa inaenda Escrow kutoka Tanesco) na kuna riba ya hizi cash.
 
Duuh....hii kweli ni clue 1.

Wazungu huwa hawakurupuki asee. Mpaka wamechukua hatua nzito ya kusimamisha Budget support wameshafanya uchunguzi wao na wamejiridhisha uwepo wa ufisadi.

Ole wake sasa serikali wakijifanya kuingilia report hii na kuichakachua kama hawajaumbuka, watu wana facts zao siku nyiiingi.

Lakini ni aibu sana kwa Taifa hiki. Yaani mpaka mzungu ndo anakuja kuwa na uchungu na affairs za kwetu?. Sijui tumelaaniwa wapi hata hii nchi! Tanzania is tragedy country!

Para ya mwisho, nasema hata Hon Kafulila anatakiwa apongezwe! Nakumbuka kuna watetea mafisadi walianzisha uzi humu kumdis Kafulila kuwa eti oooh kaumbuka. Sasa tuone nani atambuka!
 
wakati mwingine nikifikilia tz natamani kulia machozi

Ndugu yangu, mimi huwa machozi yananitoka kwa kweli. Yaani tunafanywa kama watoto wa chekechea. Nilikuwa sielewi kabisa inakuwaje watu wanaingia kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe… ni mambo kama haya.
 
Endeleeni kujidanganya ripoti wanayo wazungu sasa nyie tudanganyeni sisi nakwambia mpaka kieleweke lazima mrudishe hizi pesa lasivyo mnaiweka nchi kwenye matatizo makubwa mnayoyasikia yakitokea kwenye nchi za wwenzenu mtayasikia Tanzania.eti kisiswa cha Amani washenzi wakubwa.

mkuu mimi sio buku7 ila tetesi nlizosikia ndio hizo.
 
Back
Top Bottom