Revealing: TANESCO inaidai IPTL Tshs Bilioni 321...

Revealing: TANESCO inaidai IPTL Tshs Bilioni 321...

Nilikuwa Netherland nilikuwa nafanya MBA, nilishudia uchaguzi wa viongozi wao wa nchi katika ngazi mbalimbali.

Nilichojifunza, tofauti ya sisi na wao ni uadilifu (integrity) wao mtu anaomba nafasi ya kuongoza kwa sababu anakwenda kusimamia rasilimali zimfikie kila RAIA apate mahitaji yake ndiyo maana raia asiye name kazi ya kujiajiri au kuajiriwa analipwa name serikali fedha ya kumwezesha kumudu mahitaji ya msingi kama chakula, nyumba na mavazi, wagombea hawanunui uongozi.

Sisi wagombea wananunua uongozi na wanakwenda kupora Mali ya umma.
 
Kwa hiyo uadirifu ni tatizo linaloanzia ngazi ya familia, kukubali kuchukuwa ulanzi, sukari, kanga na vingine vyote vinavyptolewa kwa ajili ya kununua kura ni kukosa uadirifu kwa pande zote husika. Matokeo take ni haya tunakuwa taifa LA watu wa kuning'unika tu, tusio weza kuchukua hatua.
 
Tuondoe tofauti zetu tuipiganie Tanzania... tusidanganywe kwa watu kujiuzuru... Tuhakikishe fedha zinarudi na iundwe mahakama maalum ya kuwahukumu wahalifu hawa in a very short period of time.

Hii ni hatari......

Sheria zilizopo na mahakama zilizopo zinatosha kushughulikia makosa kama haya. Changamoto iliyopo ni uhaba wa watumishi waadilifu.

Ikibidi tunatakiwa kuanzisha Tanzanian fascism kupambana na waovu hawa! Hali hii haikubaliki na haitakiwi iendelee.
 
mimi naona iptl ni mzigo kwa tanesco hadi sisi watumiaji umeme.....wangeiondoa kabisa hiyo kampuni
ikiwezekana hata kibabe liwalo na liwe.
 
Bei ya umeme uniti 1= tsh.306.56/-
posho za ewura 1% = tsh. 3.07-
mchango REA 3% = tsh. 9.20/-
VAT 18% maVX = tsh. 55.18/-
tozo kila mwezi = tsh. 5,520/- (unalipa kila mwezi hata kama hujatumia)
JUmla LUKU Bei ya uniti 1 = tsh. 680/-

Kadirio la chini kabisa kwa nyumba ya familia ya watu watano walau wanahitaji uniti 1.5 kwa siku, gharama yake ni tsh.1020/- kwa siku.

Sababu ya gharama za uzalishaji umeme kuwa kubwa;
1.kila kukicha wakurugenzi wa TANESCO wanapiga dili, mfano Mhando.
2.kulipia tsh.5,520/- kila mwezi kwa ajili ya kukamilisha mikataba kama IPTL, Songas, RICHMOND, PAP, Dowans, Symbion

WANANCHI TUTAUTUA MZIGO HUU SIKU TUTAKAPOAMINI BILA CCM INAWEZEKANA, kama tutaendelea na CCM tutapigwa danadana na habari zisizo rasmi TANESCO wanaandaa DODOSO LA KUPANDISHA BEI UMEME. wakipandisha tu posho ya ewura, REA, VAT zote zitapanda kwa sababu upatikana kupitia bei itakayopandishwa na TANESCO. mfano bei ikipanda hadi kufikia 450/- mtumiaji wa umeme utalipia uniti moja kwa tsh. 927 tena hapo tsh.5,520/- ambayo unalipia kila mwezi ibaki kama ilivyo.

bila vurugu za ufisadi bei ya umeme ni tsh. 373/- kwa unit ka elfu kumi kako ungepata uniti 26.8

Kama ni kweli Wananch wa Watanzania wana uwezo mdogo sana wa kuchukuwa Maamuzi. wataendelea kukamuliwa na kutumika na wana siasa mpaka wakome.
 
lakini na sisi watanzania tumelala sana,yani hata kuungana na kuonyesha mgomo kidogo jamani tunaishia kwenye majukwaa kulalamika?hivi tunadhani hawa wezi wanaweza kutuhurumia?

Yote hatuna uchungu na mali yetu zaidi ya kuwa walalamikaji
 
Wote Mnadanganywa tu na kutumiwa, mnazungushwa huku na kule kama pia, hakuna yoyote kati yenu anayeujua UKWELI, tangu lini Wazungu wakawa watetezi wa Waafrika? kama tu wakiongezewa asilimia moja ya royalty wanayolipa kwenye madini kutoka 3-4% wanagoma, iweje leo hii waje watutetee ktk hili?

Kama wanajua kwamba Viongozi wa Kiafrika pmj na wa kwetu wameiba fedha na wameficha huko kwako hasa Uingereza mbona hawasemi kitu? Mbona hawawawekei kizuizi hata cha kusafiri tu? Mbona hawazirudishi hizo fedha?

Na kama kama wao wanawapenda sana kama mnavyodhani kwa nini hawawonyeshi mikataba ya Gesi waliyoingia na Serikiali? Kwa nini wasiwawekee Serikali vikwazo vya Kiuchumi iweje iwe kwenye hili swala tu?
Ukiona wanapiga kelele ujue kuna hela yao mahali ambayo hawajaipata na wakiipata watakaa kimya na hautasikia chochote, wala nyoko, ushahidi upo wazi Maandamano ya Gesi haitoki MT yaliishia wapi? Mnajua ni nani alikuwa nyuma yake? Ni hao hao wazungu baada ya kupewa cha juu na Serikali sasa kimya hakuna cha Gesi ya Mt wala mavi ya Gesi Mtwara!

Acheni kutumiwa, hakuna kati yenu anayeujua Ukweli, ila jambo moja ni Hakika Mzungu, hajawahi, na hatowahi kumtetea ngozi nyeusi hata siku Moja ilikuwa hivyo, iko hivyo na itabakia kuwa Hivyo!

Pamoja na ukweli wako kuhusu wazungu; lakini ukweli huo hauwezi kubadili jambo hili kwamba serikali imekosa uwajibikaji hata kufikia kuunyamazia wizi huo mkubwa wa mali za umma, wakati hatuna dawa hospitalini, hatuna hela za kujenga maabara ktk shule zetu, vijana wanakosa ajira, na mengineyo.

Ni ukweli usiopingika kwamba serikali iliyopo madarakani imefikia ukomo wa kufikiri na sasa inajiandaa kustaafu kwa kuiba chochote kinachoibika.

Huwa nafikiria sana kuhusu nchi yangu, kwamba ni siku gani tutapata viongozi wazalendo watakaofikiria kuhusu Tanzania yenye mafanikio na si hawa wanaofikiria kutuibia ili wakistaafu wawe matajiri!?
 
Ripoti ya CAG imebainisha kuwa Fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni za umma.

Aidha, ripoti hiyo imezidi kuonyesha kuwa akaunti hiyo ilikuwa na Bilioni 306.

Ripoti inazidi kuanika kuwa TANESCO walikuwa wanaidai IPTL Tshs bilioni 321 zilizotokana na malipo yaliyopitiliza (overpayments) katika 'Capacity Charge'.

attachment.php


Tumedokezwa kuwa kuna uchakachuaji unakaribia kufanyika; tungependa waache umma ufahamu kuwa si siri tena, hii ni kwa Maslahi ya Watanzania na si wanasiasa wala watawala tu.

-------- Update --------

- CAG inadaiwa ameshapeleka taarifa TAKUKURU ili hatua za kisheria zichukuliwe


- Juhudi zinaendelea Dodoma kuua mjadala juu ya sakata hili. Leo Kamati ya Nishati imekutana na Wizara na vyanzo vyetu vinabainisha wamelipwa posho ya Tshs milioni 3 kila mjumbe!


- Maswi na Werema hawabebeki; wanatakiwa kuwajibika. Muhongo kaponzwa na kauli zake. Ndulu, Likwelile hawana makosa (not ruling out)

Wakati huo huo hospital,vituo vya afya na zahanati zinakowa madawa.

Ndo mana nchi zingine nguvu ya unma hutumika coz watu wanakosa imani na serikali. Nimekata tamaa jamani na chama changu CCM kulinda wezi wa mchana.

Haya ndugu yangu Kangi hapo vipi???
 
Maskini watanzania wenyewe bado hawajitambui kama wangejitambua saa hizi majambazi yote ya ccm yangekuwa yameshaikimbia nchi hata yule aliyepasuliwa busha angechukuwa ukimbizi huko huko hospitalini ili akamuliwe vizuri busha lake. Lakini bado hawajajitambua kama walivyojitambua Burkina Faso, wanatiwa vidole vya macho na Magamba bado yamelala fofofo wala hayajitambui yamebakia umbea na udaku tu ndio wanayojua wao

Avatar yako ni ujumbe tosha sana kwa watanzania.
Tafsiri yake kwa kiswahili itakua nzuri sana kuchapishwa na kugawiwa bure Tanzania nzima!
 
Acha wamalizie tu mda wao, kama hakuna hatua zingine za kinidhamu za kuwachukulia. Wakijihudhulu wataongeza kupendwa kama white anavyopendwa siku hizi!
 
Ripoti ya CAG imebainisha kuwa Fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni za umma.
Aidha, ripoti hiyo imezidi kuonyesha kuwa akaunti hiyo ilikuwa na Bilioni 306.
Ripoti inazidi kuanika kuwa TANESCO walikuwa wanaidai IPTL Tshs bilioni 321 zilizotokana na malipo yaliyopitiliza (overpayments) katika 'Capacity Charge'.

attachment.php


Tumedokezwa kuwa kuna uchakachuaji unakaribia kufanyika; tungependa waache umma ufahamu kuwa si siri tena, hii ni kwa Maslahi ya Watanzania na si wanasiasa wala watawala tu.
-------- Update --------
- CAG inadaiwa ameshapeleka taarifa TAKUKURU ili hatua za kisheria zichukuliwe
- Juhudi zinaendelea Dodoma kuua mjadala juu ya sakata hili. Leo Kamati ya Nishati imekutana na Wizara na vyanzo vyetu vinabainisha wamelipwa posho ya Tshs milioni 3 kila mjumbe!
- Maswi na Werema hawabebeki; wanatakiwa kuwajibika. Muhongo kaponzwa na kauli zake. Ndulu, Likwelile hawana makosa (not ruling out)
wale Watanzania wenzetu waliokuwa wakimsaliti Mh Kafulila na kukimbilia kwa Kala-Sigh kwa ajili ya posho sijui wamejificha wapi maana hata huku Dodoma hawaonekeni tena
MUNGU ni mkubwa jamani hamfichi mnafiki hili sakata limefika mwisho kwani Spika Makinda alishasema hii taarifa ikifika Bungeni wengi wataondoka na maji

cc
MANKA MUSA pendolyimo optimus prime Apollo 11 shadow recruit assanal pitapiti
 
one down(escrow),two to go(mabilioni ya uswiss na mkataba kharam wa gesi)
 
Watz wenzangu mnapopitia mambo haya ya Escrow na Iptl,Mwenyezi Mungu awajalie kumbukumbu kuwa mwaka 2009 mlikuwa mkitoa sh 5000 mnapata kati ya 26 na 31 units za Luku.
Leo hii, only 5 years later unapata half of it!

Wakisema mgao hakuna ujue kesho yake unaanza,wakitangaza bei ya umeme itashuka,ujue 6 months later itapanda.

Mwenyezi Mungu awajalie "hasira kali" na maamuzi sahihi mnapokumbuka maudhi haya yaliyosababisha wengine mkafilisika biashara zenu.

Halafu unaambiwa shida zote hizo unapata kwa sababu walafi fulani hawaridhiki na ukwasi mwingi walionao,wanaamua kufilisi hadi shirika nyeti kama Tanesco!

Shirika hili la Tanesco huwa nalionea huruma sana watu wameanza kujipigia zamani sana mpaka kuna familia moja ilianza kuuza majenereta na jamaa walipewa order tu ya kukuata umeme kipindi hicho umeme wa Kidatu ulikuwa na nguvu za kutosha,lakini watu walisota na mgawo wa makusudi kabisa na mpaka yakaja haya madudu ya Songas,IPTL na mengine mengi watu wanavijiasilimia vya mgawo mpaka basi,maskani Tanesco sijui nani ataja kukuokoa labda atapatikana 201........
 
Huwa najiuliza kama kila wizi mkubwa unapotokea rais hajui au hana habari, hivi tulimuweka pale ikulu kulinda nini?

Ninahisi raisi hajui chochote kuhusu ufisadi sababu kila siku anaishi ktk airpoti za watu...
 
Back
Top Bottom