Return of Queen Nkamba wa Nyakayenze

Return of Queen Nkamba wa Nyakayenze

Hii stori inahusu utawala wa busambilo kabla ya wakoloni. Ni miaka ya nyuma sana. Miaka 3000 iliyopita. Afrika tulikuwa tunajitawala na maendeleo yalikuwa juu sana kupita hao wazungu.

Hata ujio wa Magufuli ulitabiriwa humu kwa tunaojua mila za kisukuma
 
Kwasababu nimebanwa kidogo na shughuli. Tutaendelea kesho na series. SE01 EP02
 
Hadithi inashabihiana na mila na mazingira yetu kiukweli umeleta ladha tofauti ambayo hainichoshi kuisoma keep it up ndugu.
 
riwaya nzur sana na ya kipekee inayosawili mila na destur za kiafrika
 
Episode 02

Ngaya waliwafanyia mafunzo watu wao ili kuhakikisha kwamba wanaingia busambilo na kuzima nguvu taratibu.

Baada ya miaka miwili tayari watu walikuwa wameandaliwa vyema kwenda kuingia Busambilo na kuanza kupunguza nguvu za utawala.

Aliandaliwa binti mzuri mwenye umri wa miaka 9 na alipewa mafunzo maalumu kuhakikisha kwamba anaolewa na mtoto wa Kapera ili kwamba utawala wa Busambilo uchanganyikane.

Watu wale walifundishwa mawasiliano mbali mbali wanayotumia watu wa Busambilo. Kwa kweli haikuwa rahisi kupata watu mahili maana ilibidi watumie miezi mitatu hivi kupata watu mahil wenye uwezo na akili kuweza kufundishwa namna ya kuteka Busambilo.

Kiongozi wa kikundi hicho alifundishwa namna ya kujikinga ili mbinu za uchawi alizofundishwa zisijulikane. Waliambiwa kwamba wajifanye watu wasiojua kitu chochote na wawe tayari kufundishwa na wawe wanaelewa haraka.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 9 walimpatia jina la Nyamiji ili kwamba jina lake liendane na watu wa Busambilo.

Basi safari ya watu hao ilianza, walipitia maeneo ya Busiya. Walipofika busiya walidai kwamba wamefukuzwa kutoka Ngaya na kwamba hawana sehemu ya kwenda. Basi waliona sehemu ambayo wanaweza kuwa salama ni katika nchi ya Busambilo.

Basi Mwanangwa wa busiya aliwaruhusu na kuwapatia sehemu ya kukaa. Basi mkuu wa wale watu walifurahi sana maana hatua ya kwanza imefanikiwa. Akafungua kitabu chake cha mipango na kuweka alama ya vema kwenye mpango namba moja.

Mpango wa pili ni kuhakikisha Nyamiji anazoeana na mtoto wa mwanangwa ili kwamba apate nafasi ya kwenda nae Ikoulou kwenda kuonana na watoto wa Mfalme.

Kweli mipango ilianza kusukwa kuhakikisha kuwa mtoto wa Mwanangwa wa busiya aitwae Milembe wanazoeana na Nyamiji.
 
Nyamiji alikuwa amefundishwa michozo mbali mbali na alikuwa anajua kuimba vizuri sana. Basi siku moja kama kawaida ya watoto wan nchi ya Busambilo. Walienda kwenye chuo cha mafunzo ya watoto ambacho huwa kinafanyika mara tatu kwa mwaka, kwa kipindi cha wiki mbili mbili.

Watoto wote wa busiya walienda kwenye chuo chao cha busiya kwaabiri ya kujifunza mila na tamaduni za busambilo.

Katika vyuo vya watoto; watoto hufundiswh, kupika, kushona, mavazi, uchoraji na kilimo bora. Basi kipindi hicho kilikuwa ni kipindi cha msimu wa pili watoto hugawanywa makundi makundi kulingana na umri wao.

Mafunzo hutofautiana kulingana na rika la watoto. Basi msimu huo nchi ilikuwa imeamuru watoto wafundishwe mila na tamaduni za watu wa Busambilo. Katika mafundisho hayo ni pamoja na Uimbaji, Uchoraji, Hadith na mengine mengi tu.

Milembe alikuwa na umri wa miaka kumi kwa hiyo alikuwa kwenye rika la watoto namba mbili wenye umri kati ya 8 mpaka 12. Hao watoto walikuwa kwenye kundi namba mbili yaani akili zao zimeanza kuelewa mazingira.

Ilikuwa mara ya kwanza Nyamiji kuenda kwenye chuo hicho. Kilikuwa kimejengwa kwa ustadi. Nyumba zilizotengenezwa kwa miti na zimepambwa vizuri sana. Madarasa yale yenye hewa safi na viti vya kukalia vilivyo chingwa kwa ustadi wa hali ya juu. Njuu yalikuwa yameezekwa kwa nyasi zilizopambwa vizuri sana kwa michoro mbali mbali.

Kusema kweli alishangaa sana maana Ngaya hawana chuo kizuri kama hicho alicho kiona.

Basi kabinti kamoja kakamuona na kakasema “heee unashangaa nini sasa je ukienda chuo kikuu si unaweza ukazimia jinsi kilivyo jengwa!!!”

Nyamiji akasema kwa kweli kwetu hakuna chuo kizuri kama hiki. Kwanza kwetu chakula cha shida sana lakini huku nyie mnakula na kusaza. Kwa kweli huku mna raha sana.

Kile kibinti kikamuuliza kwani wewe umetoka wapi. Huku akiwa amejifunika machoni. Sisi tumefukuzwa kutoka nchi ya Ngaya eti wanasema sisi tuna sababisha ukame.

Kale kabinti kakasema pole sana usiogope basi mimi nitakuwa rafiki yako.
 
Kale kabinti kakasema mimi naitwa Nyanzobe kwani wewe unaitwa nani. Akasema mimi naitwa Nyamiji. Basi Nyanzobe akasema twende basi darasani.

Basi walipo kuwa wakielekea darasani Nyanzobe akamuona Milembe. Nyanzobe akiwa na furaha akaita Milembeee! Milembee! Njoooo hapa!!.

Milembe alikuwa binti mcheshi, mzuri wa sura na mashacu yake yalikuwa na vimashimo na meno yake yalikuwa meupe pe, huku yakipambwa na mwanya mzuriiii!!.

Basi Milembe alitazama huku na kule iliajue sauti inatoka wapi, Baadae alimuona Nyanzobe amenyosha mkono wake juu. Milembe alipomuona Nyanzobe alitabasamu na kukimbia kwenda kumlaki.

Walikutana na kusalimiana, baadae Nyanzobe alimtambulisha Nyamiji kwa Milembe.

Nyanzobe akasema hapa chuo rafiki yangu mkubwa ni huyu Milembe. Milembe ni mtoto wa Mwanangwa wetu huku Busiya. Baba yake Milembe na baba yangu ni marafiki sana.

Nyamiji alitabasamu na kusema ninashukuru sana nimekutana na rafiki ambao tunaweza kushirikiana.

Basi Nyanzobe alimusimulia kila kitu Milembe kuhusu Nyamiji. Baada ya hapo waliingia darasani.

Mwalimu alianza kufundisha uchongaji wa viti. Alifundisha aina ya viti na namna ya vitit vinavyochongwa.

Baada ya kumaliza kufundisha aliwaambia basi siku ya leo tutaanza kuchongwa kwa vitendo. Baada ya wiki hizi mbili kila mmoja awe amemaliza kuchonga kiti kimoja na hivi viti tutakavyo vichonga vitabaki hapa chuoni kwa ajili ya kukalia darasani.

Basi wanafunzi wato walisema sawa. Waliyoka darasani na kwenda kwenye kambi waliyofikia kwaajiri ya kupata uji na kujiandaa na somo la mchana kwaajiri ya uimbaji.
 
Kipindi cha mchana kilipofika mwalimu aliingia darasani na kuwataka kila mwanafunzi aimbe wimbo wowote anaoujua.

Kila mwanafunzi aliimba wimbo wake.

Basi ikafika zamu ya Nyamiji, Nyamiji akasimama na kusema ninaomba niimbe halafu baadae tutaimba wote. Nyanzombe akasema kwa sauti ya juu sawaaaaaa!

Basi nyamiji alianza:-

“Sumbili ungw’ana wa wise wizaga na butemi wakwex2

Abalalile lalagi ungw’ana wizaga kubusola ubutemi wakwex2

Mishagi lulu mishagi ikanza lya kubusola ubutemi bokwex2”

(Mpokeeni mtoto wa kwetu amekuje na ufalme wake x2

Waliolala laleni mtoto amekuja kuuchukua ufalme wakex2

Amkeni sasa amkeni mda wa kuuchukua ufalme wakex2)

Wanafunzi walifurahi sana na kila mmoja alipiga makofi na wote wakaanza kuuimba huo wimbo.

Nyamiji alisifika sana pale chuo kila mmoja alikuwa akiimba huo wimbo.

Wimbo huo ulitapakaa Busiya yote na hatimae ulienea Busmbilo nzima. Kila mtu akiwa anafanya kazi alikuwa akiuimba huo wimbo. Vijana wakiwa kwenye vikundi vyao vya kilimo walikuwa wakiuimba wimbo huu.

Jina la Nyamiji lilisifika sana kila sehemu watu walikuwa wakizungumza kuhusu Nyamiji. Wakisema nchi yetu imepata mwimbaji mzuri sana. Itabidi huyu binti apelekwe kwa mfalme ili awe anamwimbia mfalme wakati anamawazo. Vilevile aweze kuwaimbia wageni wa mfalme wanapokuja kumtembelea.

Watu walimpenda Nyamiji alikuwa akiitwa kila sherehe kuimba.

Basi kiongozi wa watu kutoka Ngaya alifungua kitabu chake na kuweka vema kwenye hatua yake ya pili.
 
Tengeneza movie ili iwasilishwe kwa njia hiyo itakuwa nzuri zaidi angalia zile movie za kihistoria zinajikita kwenye asil ya mazingira ya zamani mfano spartan ,harcules n.k
 
Baada ya mda wake kuisha kukaa Malakal, Nyamhindi na wale waliomsindikiza walianza safari kuelekea Misri.

Watu wa Malakal waliwasindikiza na kuwapatia ngamia watakao wasaidia kupita jangwani. Waliwafungashia chakula kingi na nguo za kuvaa njiani.

Basi safari yao ilianza.

Baada ya siku tano walikuwa tayari wamefika Kharga. Ikabidi wapumzike kwenye mji huo.

Walifika kwenye nyumba za kulala wageni na kuomba sehemu ya kupumzika.

Kwa taratibu za mji huo, unapoingia nyumba za wageni ni lazima kuandika jina lako na sehemu uliotoka.

Basi haikuwa taabu kwao kuandika majina yao na sehemu waliotoka. Basi waliandika na kuwakabidhi wahusika. Baadae walitafuta chakula.

Basi muhudumu alichukua majina ya wageni hao na kupeleka kwa bosi. Bosi alianza kupitia majina ya wageni wote walioingia kwenye nyumba yake ya wageni.

Baadae akaona watu kutoka Busambilo. Ikabidi ashituke, imekuwaje tena!!.

Akaangalia jina kwa jina akaona Jina la Nyamhindi. Dah! bosi alianza kutetemeka na kusema itakuwaje sasa maana huyu mtu nimesikia habari zake kuwa kawapiga watu wa Asosa. Nifanye nini sasa?

Bosi alituma watu kwenda kutoa taalifa kwa watawala kwamba kunawavamizi wamekuja kwenye nyumba yake ya kulala wageni. Amepata taarifa kuwa hao watu sio wazuri.

Kwa jinsi yule bosi alivyokuwa naheshimika katika mji huo; watawala walituma askari kuzunguka jengo hilo na kuwakamata waharifu hao.

Ili bosi atoe ushahidi unaokubarika alijichana chana na kisu mkononi ili kuhakikisha watu hao wanakamatwa.

Basi msafara wa Nyamhindi ulikamatwa nay eye pia alikamatwa na kufungiwa kawenye chumba chenye giza.
 
Tengeneza movie ili iwasilishwe kwa njia hiyo itakuwa nzuri zaidi angalia zile movie za kihistoria zinajikita kwenye asil ya mazingira ya zamani mfano spartan ,harcules n.k
Baada ya hapa hatua ya movie itafuata. Hebu ngoja kwanza tuanza na Hadith. Kutengeneza movie inahitaji gharama kubwa ikiwamo wahusika. Hii hadith inawahusika wengi mno. Na ikumbukwe ipo na Season nne.
 
Nyamhindi na wendake hawakuelewa kwanini wamekamatwa. Walianza kuulizana ni nini sasa hii. Mbona hatuelewi?

Nyamhindi akawaambia nyie tulieni tu tutajua nini kinaendelea hapa.

Baada ya muda kidogo askari walikuja huku wakiwa na fimbo mkononi na kuanza kuwapiga huku mikono yao ikiwa imegungwa kwenye miti iliyokuwa ndani ya kile chumba.

Askari walijitahidi sana kuwapiga. Huku Nyamhindi na wenzake wakiuliza hivi sisi tumekosa nini mbona mnatupiga tu na hatuelewi mnatupiga kwa sababu gani.

Baada ya hao askari kutosheka kuwapiga. Walirudi kwa mkuu wao na kutoa taarifa kwamba tumewapiga ile mbaya na kila mmoja anatoa damu.

Mkuu akasema kwa kipigo hicho tukienda kuwahoji lazima watatueleza ukweli kwanini wamemvamia na kumpiga yule bosi wa nyumba ya wageni.

Nyamhindi akasema hapa tusipokuwa makini hawa wajinga wanaweza kutuua. Kwahiyo ni mda sasa wa kuanza kujitetea. Sawa?

Wote wakasema sawa huku damu ikiwavuja kila sehemu na minundu kibao kwenye nyuso zao.

Basi Nyamhindi aksema kwa sauti kubwa “Kambaaaaa Katika”, Kamba zote zilizokuwa kwenye mikono yake zikakatika.

Kisha akawafungulia wenzake. Walijituliza na kujifanya kwamba bado wamefungwa.

Baadae wale askari walikuja tena huku wakicheka. Walikuwa wawili wamejazia miili yao miraba manane. Wakafungua mlango huku wamebeba fimbo za maana mikononi mwao.

Walipofungua mlago tu kila mmoja alikutana na kichwa cha Nyamhindi. Kichwa cha msichana huyu kilikuwa kimekomaa kama jiwe.

Wale askari walibabaika na kuanza kuona maluwi luwi. Huku wakipiga kelele nimepigwa jiwe nimepigwa jiwe. Nyamhinndi aliwapa kichapo cha mbwa mwizi. Baadae akawafunga kamba.
 
Mkuu kwa kweli stor bomba sana ziachie mfululizo mkuu
 
Mkuu kumbe hujarudi tuu?? tupe vitu vyakutafutia ucngizi aisee
 
Back
Top Bottom