Return of Queen Nkamba wa Nyakayenze

Return of Queen Nkamba wa Nyakayenze

Nzuri sana mkuu una moyo saana wa kutuburudisha wewe siyo mchoyoo hongera saana nakufatilia saanaa endelea mkuu
 
Kitabu cha majira kinatakiwa kitunzwe na wanangwa wa Buhungukila. Huko ndio vitabu vyote huwa tunavitunza. Pale nyota itakapozaliwa kutakuwa na dalili, Mvua itanyesha kubwa huku jua likiwaka sana. Ndipo mjue sasa mtoto kazaliwa wa kike atakaye leta ukombozi kwenu.


Watu walikuwa wanasikiliza kwa makini na huku waandishi wa mfalme walikuwa wakiandika maelezo hayo. Walikuwepo wandishi kumi na mbili wa mfalme wakiandika jinsi mfalme alivyo kuwa alieleza.

Mke wa falme (Nyandalo) alikuwa yupo kwenye kiti chake amekaa na akimusikiliza kwa umakini mfalme alipokuwa akielezea hayo yote.

Mke wa mfalme alikuwa na wasaidizi wake saba wa kike (Ngole/Bagole). Hao ndio walikuwa wasaidizi na walizi wa mke wa mfalme. Walikuwa wamepitia katika mafunzo mabalimbali njisi ya kuweza kumlinda mke wa mfalme. Wagole wote walikuwepo siku hiyo nao walikuwa wakisikiliza kwa makini jinsi alivyo kuwa akielezea mfalme.


Baada ya mfalme kumaliza kutoa maelezo hayo kulikuwa na sherehe kubwa sana. Wanangwa wote walikula na mfalme na kubadilishana mawazo ya hapa na pale.

Mbiu ilipigwa askari wote walikusanyika kwaajiri ya maonesho mbalimbali. Kulikua na maonesha namna askari walivyo na ubora wa kurusha mishare, Namna ya kutumia mikuki, visu nk. Alionesha umahili wao kweli vijana walikuwa na ujuzi wa hali ya juu.
Mkuu mtunzi Ni wewe??
 
Yasni najiona niko karne hiyo,mtunzi hongera,ila Kuna ka ukweli fulani,wakina mzee Lubala wangekuwa hai na chuo Chao, guess who ange ji enroll Humu ndani?
 
Watu wa Ngaya walipata huzuni sana baada ya jitihada zao kizimwa kirahisi. Walirudisha majeshi yao mpaka nchini kwao na kwenda kujipanga upya.

Mkuu wa nchi ya Ngaya aliamua kwenda kutafuta ushauri Kalungu kusini zaidi ya nchi yake.

Watu wa Kalungu walikuwa na wataalamu wa kusoma tawala mbali mbali na kujua majira ya tawala hizo.

Mfalme wa Nagaya na watu wake walifika huko Kalungu na kukutana na wataalamu wenye uwezo wa kusoma majira ya tawala mbali mbali.

Mfalme alipofika tu mkuu wa kitua cha usomaji wa majira na tawala alitambua.

Alimwita pembeni na kuanza kumwambia hakika nilikuwa nasubiria ukio wako kwa mda mrefu sana. Ninajua kabisa huwezi kushindana na Basambilo maana wananguvu kubwa mno. Huwezi kwenda kuwavamia kichwa kichwa tu na uweze kuwashinda.

Wewe unataka uchukue sehemu ya Busambilo sawa kabisa, lakini mimi nataka kukuambia wewe huwezi kuchukua sehemu yeyote mpaka uwe na mipango ya mda mrefu.

Inatakiwa uhakikishe unaipata fimbo ya Falme na kile kitabu chao cha kusomea majira na kujua dunia ilivyo.

Baada ya kuwa na hiyo fimbo hakuna yeyote atakayeweza kukuzuia katika nchi zot echini ya jua.

Kitu cha pili hakikisha unapeleka watu wako wakafundishwe kwenye chuo chao kikuu na kujua mbinu mbali mbali za kujihami na kujenga nchi. Kwenye chuo hicho sio wachawi tu wanaofundishwa ila kuna wataalamu wa kilimo, ufugaji, Kutengeneza majembe na wataalamu wa vita.

Kwa hiyo kazi unayotaka kuifanya sio ndogo ni kubwa sana, Unatakiwa uwe na watu wako ndani ya hiyo nchi wa kukuletea habari. Ila ukumbuke kuwa watu wako itakuwa ni rahisi sana kujulikana kule kulingana na wanavyoongea.

Sasa basi itabidi uchukue kundi la watu wajifanye kwamba wamefukuzwa. Kwakuwa watu wa busambilo sio wachoyo na ni wakarimu watawakaribisha. Itabidi mfanye namna yoyote ile wawe na mazoea na watoto wa mfalme. Halafu nasikia mfalme amefariki na amempa utawala mtoto wake.

Kwahiyo basi watu wa huko wanapenda sana wanawake weupe. Kwahiyo basi tafuta familia yenye watoto wazuri wapelekwe huko ili waweze kuishi huko na kuchunguza siri zote za huko hatimaye utawala wa huko mtaanza kuuangusha taratibu.

Lakini mkianza kutumia vita hatimaye basambilo watakuja kwenye nchi yenu na kuwafukuza na kuliangamiza jeshi lenu.

Kitu kikubwa ni kwamba hakikisheni mnaipata hiyo fimbo na kile kitabu maarumu.
 
Kitu kingine Kuhusu Kummaliza Gindu. Gindu ana siri moja rahisi sana lakini unatakiwa umzoee. Huyo mtu anapenda sana kula nyama ya kondoo. Kwa hiyo ili uwe rafiki yake hakikisha unampelekea kondoo kila wakati. Na ukifikisha mara tano basi utakuwa karibu naye na unaweza ukamfanya chochote sasa.

Gindu kichwani anaunywele mmoja unarangi yeusi sana. Ule unywele ndio unaompa nguvu huyu mtu. Ni vigumu kidogo kuuona maana amesuka lasta na mara nyingi huwa amefunga kiremba nywele zake.

Basi ukiweza kuuona huo unywele na kuukata basi utakuwa umemaliza nguvu zake kwa wakati huo mpaka utakapoota. Kadri unavyokuwa ndio nguvu zake zinaongezeka. Hakikisha ukimkata huo unywele unamuua hapo hapo maana unywele ukiota na anajua kabisa aliyeukata ni nani atafuatilia mpaka atajua huyo mtu ametoka wapi na ametumwa na nani.

Lakini nasikia kuna mtaalamu mpya yupo kule ambaye kwa sasa ni mkuu wa chuo cha huko. Mfalme akajibu ndio jina lake anaitwa Lubala.

Hawa wakuu wa chuo mara nyigi hawajui kupigana huwa wanahuruma sana tofauti na mtu kama Gindu huyu hana huruma hata kidogo.

Hivi ulishawahi kumuona Gindu, mtaalamu aliuliza. Mfalme akasema hapana huwa nasikia tu habari zake.

Gindu ni mzuri sana wa sura, ni mrembo haswa na ameolewa yupo na mtoto mmoja wa kike na huyo mtoto ni mzuri haswa. Umri wa Gindu ni mkubwa sana lakini bado anaonekana kama binti tu. Wanawake wengi wa busambilo ni warefu na wanajidai sana kwakuwa kwao chakula tele.

Mimi nitaungana na wewe tuna hakikisha tunauangusha utawala wao. Ila tutakapo uangusha huo utawala. Watu wangu hawa waweze kuishi katika nchi hiyo ya neema na tuweze kutawala wote kwa pamoja.

Kwahiyo basi rudi nyumbani ukaanze kuwapa mazoezi watu wako huko na kuwaeleza nia ya nchi yako ni nini. Uwape mbinu za kuweza kuwateka watu wa busambilo kiakili. Nitakupatina kitabu cha mafunzo. Itakuchukua mwaka mmoja kufundisha watu 15 kwaajiri ya kazi hiyo sawa?

Mfalme wa Ngaya aliitika sawa. Na kisha wakaanza safari ya kurudi.
 
Masanja alipofika nyumbani kwakwe mke wake alimlaki kama kawaida yake huku akiimba wimbo. Watu wote kwenye hiyo familia walitoka na kumlaki mzee Masanja.

Alipofika tu akaulizia Nyamhidi yupo wapi? Nshoma akasema yupo anaongea na ndugu zake. Basi baada ya kumalima mazungumzo na ndugu zake namuhitaji aje.

Nshoma aliandaa chakula kama kawaida yake. Kisha akamwita Masanja kupata chakula. Baada ya chakula Nshoma alimuuliza kuhusu safari yake, kuhusu msiba na mambo mengine yaliyotokea kule.

Masanja alimusimlia mke wake mambo yote. Kisha kamwambi Nshoma naomba umwite Nyamhindi aje anisalimie maana tangu nije sija muona.

Nshoma alienda kumwita Nyamhindi. Nyamhindi alienda kuvaa gauni alilo nunuliwa na babu yake wakati alipo kuja kuwatembelea. Nyamhindi alipendeza sana. Kisha bibi yake akamwambia umependeza sana.

Nyamhindi alienda kumuona babu yake. Alipo muona babu alitabasamu na kusema malikia umependeza sana.

Nyamhindi alimsalimu babu yake na kupiga magoti mpaka chini. Kisha babu akamwambia basi keti mjukuu wangu unanipa faraja sana nikikuona.

Je umesikia taarifa kuhusu babu yako.

Nyamhindi akasema sina uhakika lakini moyoni mwangu najisikia kama babu yangu amefariki hebu babu niambie kama kweli niweze kuamini moyo wangu.

Masanja alikohoa kidogo kisha akaendelea unajua wewe binti ni mtoto wa pekee sana. Mara yangu ya kwanza kukuona hakika nilifurahi sana, Wewe unaakili sana kama mama yako.

Mjukuu wangu moyo wako hauwezi ukakudanganya. Kila ulichokipata moyoni ndio mimi nimetoka kumzika babu yako. Na Mjomba wako mkubwa Kapera amechukua nafasi ya babu yako. Kwahiyo sasa mfalme wetu sasa ni Kapera.

Nyamhindi akamuuliza kwanini babu alinipatia hiyo fimbo na kitabu wakati mimi ni mtoto mdogo?

Mjukuu wangu babu yako na mimi tunakuamini sana kwamba ndio wewe tu katika uzao wako utakaye weza kukomboa nchi yetu. Nikianza kukufundisha utaelewa mengi yameandikwa katika hicho kitabu. Ila unatakiwa mtu yeyote asijue kuwa una hivyo vitu maana huwezi kujua nani mwaminifu. Niamini mimi tu na mama yako. Hata bibi yako usimwambie kitu.

Nyamhindi akauliza hata Ntemanya?

Babu akasema ndio usimwambie chochote maana akibanwa kidogo tu na mama yake anaweza kusema siri zote.

Nyamhindi akasema basi mimi babu sitamwambia mtu yeyote nitatunza siri hii lakini babu naomba Ntemanya awe mwanangu maama anateseka sana.

Najua unamuhurumia sana wewe ni wajibu wako kumlinda Ntemanya kwa hiyo mlinde asije akadhurika na chochote sawa.

Nymhindi akasema sawa.

Basi nenda kalale kesho tunaanza kujifunza sawa?

Sawa.
 
Karibu sana. Siyo hii tu zipo nyingi.
Mkuu mm pia Ni story and script writer, but naandika story za maudhui tofauti Na yako, nimependa story hii, Nina project ambayo naandaa lengo kubadilisha kabisa hii industry ya film hapa bongo, niko Na mazungumzo Na Wazungu flani kuona Kama wanaweza kuja kuwekeza kwenye film za kibongo, Kama unaweza kuwa interesting tunaweza kujoin mkuu! Tukabadilisha kabisa huu utumbo wa Bongo movie unaofanywa sasa.
 
Mkuu mm pia Ni story and script writer, but naandika story za maudhui tofauti Na yako, nimependa story hii, Nina project ambayo naandaa lengo kubadilisha kabisa hii industry ya film hapa bongo, niko Na mazungumzo Na Wazungu flani kuona Kama wanaweza kuja kuwekeza kwenye film za kibongo, Kama unaweza kuwa interesting tunaweza kujoin mkuu! Tukabadilisha kabisa huu utumbo wa Bongo movie unaofanywa sasa.
Hapo umenena. Basi tutafutane. Kwa upande wa Hadithi na Riwaya nadhani najitahidi.
 
Masanja alianza kumfundisha Nyamhindi vitu jinsi ya kukisoma kitabu alichopewa na babu yake.

Kwanza alianza kumfundisha alama zilizo juu ya kitabu hicho.

Kitabu kilikuwa na rangi nne Bluu, Zambarau, Nyeusi na Nyeupe.

Kila rangi ina maana yake na kila moja inamatumizi yake.

Tukianza na rangi ya bluu; hii inahusika na hekima, elimu, maarifa na ujuzi. Kwa hiyo sasa tunaanza hatua hii ya kwanza kujua rangi na maana zake.

Rangi ya zambarau hii inahusika na utawala, Nguvu na mamlaka.

Rangi nyeusi inahusika na Utisho, Mauaji, Vita au hukumu.

Rangi nyeupe inahusika na Amani, furaha, sherehe upendo na rehema.

Pia hapa juu ya kitabu hiki kuna umbo lenye pembe nane na ndani ya hilo umbo kuna mishale nane inayo elekea katika kila pembe.

Hilo umbo lenye pembe nane linamaanisha pande nane za dunia. Na nane maana yake ni mwanzo mpya. Na ukiangalia kwa makini hiyo mishale inatengeneza maumbo ya pembe tatu. Hayo maumbo yanamaanisha vitu vya duniani. Ukisoma ndani ya kitabu utakuta sehemu inayoelezea hizo pembe tatu. Zinatakiwa kuunganishwa mbili mbili kiustadi sana na kuwa na maana ya vitu vya duniani ambavyo ni Moto, Maji, Hewa na Ndunia.

Kwahiyo basi hiki kitabu kipo na kurasa 33 na kila ukurasa una maana yake. Na unasiri iliyo ndani yake. Hakuna hata mmoja aliyeweza kukisoma na kukimaliza na kuelewa maana yake, Mimi hapa nitakufundisha kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka wa tisa. Ndani ya miezi sita utakuwa umejifunza kmpaka ukurasa wa tisa na baada ya hapo utaenda chuo huko Busongo utakaa kule miezi sita tena utajifunza ukurasa wa kumi hadi 21 utarudi hapa na nitakufundisha vitu vingine ukijiandaa kwenda Seke kuonana na Gindu atakaye kufundisha ukurasa wa 22 mpaka 24 mda wa miezi sita. Unanielewa lakini?

Nyamhindi akasema nakuelewa babu. Haya ninayo yasema ni muhimu sana uyaelewe. Baada ya kumaliza kufundishwa na Gindu utaenda Ntuzu kule kuna mzee mmoja utakutana nae huko utakaa mwaka mmoja ukifundishwa ukurasa wa 25. Watu wengi mno walishindwa kuelewa huu ukura maana una siri kubwa sana na wengi waliishia kufa. Kwahiyo unatakiwa uwe makini sana. Ni mmoja tu aliwahi kuweza ni huyo mzee pekee yake. Kwahiyo unatakiwa uw makini.

Baada ya hapo itabidi uende Bunyankole nchi jirani nay a kwetu tunasaidia nao mambo mengi sana. Kule utaenda kujifunza vitu tofauti tofauti kwa ajiri ya maandalizi ya kujifunza ukurasa wa 26 mpaka 30.


Basi kwa leo tunaishia hapa kesho nitaanza kukufundisha namna ya kuandika kabla hatujaanza kujifunza kitabu sawa?

Nyamhindi akasema sawa.
 
Baada ya miaka miwili Kapera alikuwa akiliongoza Taifa lake vizuri hakuna chokochoko yoyote ilikuwa inajitokeza.

Tayari Nyamhindi alikuwa yupo Bunyankole akijifunza kufanya biashara na Lugha mbalimbali.

Akiwa kule Bunyankole mkuu wa chuo aligundua msichana huyo alikuwa na uwezo mkubwa sana akiwa darasani. Kwa sababu mkuu wa chuo hicho alikuwa anajuana na Masanja ilibidi atume wajumbe waende kwa Msanja kumuomba kwamba Nyamhindi aende misri akajifunze falsafa ya namba.

Masanja alituma ujumbe kwamba huyu msichana bado hajamaliza kusoma kitabu kwahiyo ni muhimu akarudi kwaajiri ya kumaliza hatua hiyo ya kusoma kile kitabu. Kwa kuwa zilikuwa zimebaki kurasa tatu tu ili amalize.

Mwalimu mkuu wa chuo cha Bunyankole alikubaliana na Masanja lakini alituma wajumbe kumuuliza kuwa ni nani sasa anaye weza kumfundisha ili ajue hizo kurasa. Maana watu wanaojua hizo kurasa walishapotea na hawajulikani wapo wapi.

Kurasa hizo tatu ni ngumu sana maana zinahusika na kumuwezesha mtu kusafiri kwenda kwenye ulimwengu wa juu zaidi na kupata maarifa.

Ukurasa wa 31 unahusika na mbinu za kumwezesha mtu kwenda ulimwengu wa pili mpaka wa tatu, Ukurasa wa 32 unafundisha namna ya mtu kwenda ulimwengu wa nne na watano na ukurasa wa 33 wenyewe unahusu kwemda ulimwengu wa sita na saba.

Katika ulimwengu wa sita na saba ukifika huko na kurudi hakuna nguvu yeyote duniani inaweza kukuzuia. Huko watu ni wastaalabu wapo juu sana kimaendeleo, wanafuraha na uwezo wao upo juu sana.

Mwalimu mkuu wa Bunyankole akamwambia nadhani huko akienda anaweza akaelekezwa wapi anaweza kuwapata walimu wakuweza kumfundisha.

Baadae Masanja alikubali na kumwacha Nyamhindi mikononi mwa mwalimu mkuu wa Bunyankole ili aandae taratibu za Nyamhindi kwenda Misri kujifunza falsafa ya namba.

Baada ya mwezi mmoja Nyamhindi alianza safari ya kwenda huko misri.
 
Leo ijumaa kuu nadhani wengi hatuendikazini basi ngoja niendelee....
 
Back
Top Bottom