Return of Queen Nkamba wa Nyakayenze

Return of Queen Nkamba wa Nyakayenze

Mwalimu mkuu wa Bunyankole alimpatia Askari watatu watakao msindikiza kwenda huko misri.

Walisafiri siku nne njia. Wakafika mji unaoitwa Malakal. Asilimia kubwa ya watu wa sehemu ile ni wezi sana. Wanatumia njia mbali mbali kuweza kumwibia mtu.

Basi kwa sababu ilikuwa ni jioni na hawajui hili wala lile. Kwakuwa Nyamhidi alikuwa amefundishwa lugha mbalimbali alikuwa anajua lugha 12 kwahiyo aliweza kuongea na watu wa kule.

Baada mda watu wawili wakaja Nyamhindi akaongea kwa lugha yao “Apwoyo binowu” (habari zenu). Nawenyewe wakaitikia hivyo hivyo.

Akasema “Itye nining?”(Hamjambo?) wakajibu “Atye maber” (Hatujambo).

Baadae akaendelea kuongea nao na kuwauliza kama wanaweza wakapata sehemu ya kupumzika. Wale jamaa wakaona hapa sasa ni dili yaani mbuzi kafia kwa muuza supu.

Wakaitikia haraka sana kwamba wanaweza wakawasaidia. Wale jamaa wakaitana pembeni na kunong’onezana. Sasa hapa dili tunapigaje.

Wakakubaliana hawa jamaa wapo na kabinti kadogo sasa tunatakiwa tukaite watu wengi waje tuwavamie halafu haka kabinti tunakauza mbali kabisa na sisi tunapata pesa.

Wakakubaliana basi wewe nenda kawastue washikaji waje wakati mimi nawazubaisha hapa.

Poa.

Jamaa akaondoka kwenda kuwaambia wenzake kuwa kuna dili kali imeibuka kwahiyo waende kuifumua. Basi njemba nane ziliungana na jamaa zikabeba marungu, panga na fimbo.

Zile njemba zilikuja zina kimbia huku zinapiga kelele wakamate wale wanaume tunawaua msichana tunaenda kumuuza. Njemba zinakuja mbio mbio.Ha kuona hivyo Nyamhindi akawaambi jamani tukimbieni maana hapa sio salama. Wakaanza kukimbia ili kuwa kimbia hao jamaa. Lakini njemba zilikuwa na mbio kama nini.
 
Nyamhindi akaona huu ujinga akasimama na kuwageukia. Nao wakasimama. Akasema hivi nyie mnataka kuumia?

Akapiga mstari atakaye weza kuvuka mstari huu basi mimi mnanichukua na kunipeleka kokote.

Njemba zika cheka, haka katoto kanatuchezea hebu kakamateni haraka.

Nyamhindi alisimama kuwasubiri. Alikuwa akikumbuka namna mafunzo aliyo kuwa anafundishwa na Lubala jinsi ya kupigana pasipo kutumia uchawi.

Alikumbuka Jinsi ya kurusha mateke, ngumi na kutumia kichwa. Baada ya kukumbuka yote alijiweka sawa kwaajili ya kukabiliana nao.

Wale watu waliomsindikiza wenyewe wako mbali wakichungulia kwenye vichaka kuona kitu gani kitatokea.

Walejamaa wakaja mbio kumkamata kila akisogelea mstari alipigwa ngumi ya pua na kuanguka chali. Wote walipigwa ngumi za pua.

Aaah baada ya kuona hivyo wakasema kumbe wewe binti ni mtukutu wakataka sasa kuleta ugomvi ili wapigane naye. Nyamhidi aliwapa kipondo cha mbwa mwizi wote walitoka damu na kila mmoja alilia na kusema tusamehe tusamehe.

Akawauliza mnakaa wapi? Wakasema mjini sasa twendeni wote huku mnaimba malikia malikia ameingia.

Huku kila mmoja anasikilizia maumivu yake walianza kuimba huku wakielekea mjini.

Watu walishangaa sana mana hilo kundi la wezi lilikuwa linasifika sana na watu walikuwa wanaliogopa. Mpaka serikali ya huko ilikuwa inaogopa sana kundi hilo. Na wakiliona hilo kundi walikuwa wanajificha.

Basi watu wamji huo walitoka majumbani mwao na kuangalia ni nani anaye imbwa kuwa ni malikia. Baadae waliona kasichana kenye umri kama miaka 14-15 hivi. Walishangaa sana ina maana hako kasichana wanakaita malkia. Hawa watu si huwa wanauza wasichana nchi za mbali? Iweje leo hii wanaimba hivyo. Halafu ona wote wanaonekana wamepigwa vibaya sana. Watu walibaki midomo wazi bila kuelewa nini kimetokea.
 
Nyamhindi alisimama juu ya meza na kusema kuanzia leo hakuna mtu kufanya fujo kwenye mji huu. Yeyote atakayeleta fujo au ugomvi nitamshikisha adabu kama nilivyo washikisha hawa.

Mimi jina langu naitwa Nyamhindi, Mjukuu wa falme wa Busambilo. Watu wote walipiga magoti na kuanza kusujudu. Wakisema Malikia, malikia wewe ni mkombozi wetu hapa.

Akasema mimi sio wa kusujudiwa ni binadamu kama ninyi, ila nimezaliwa kwaajili ya kuleta ukombozi kwenye jamii zetu zote. Haitakiwi kuchukiana sisi sote ni wanadamu hakuna aliye juu ya mwenzake. Inafaa kusaidiana wote kwa pamoja, aliye na shida msaidieni. Kuanzia leo sitaki kusikia wizi. Inabidi kufanya kazi kwa bidi kila mmoja.

Basi wakuu wa serikali walikuja na kusikiliza Nyamhindi alivyokuwa akiongea.Kamishina mkuu wa mji huo akapita mbele ya watu na kuuliza huyu binti amepata kibali wapi kuanzisha mkutana hapa?

Wale wezi wakamwambia huyu ni malkia wetu kwa hiyo huna ruhusa ya kufanya lolote kwa sasa. Ananguvu sana ameweza kutupiga sisi sote tulipokuwa tunajaribu kumdhuru. Kwa hiyo kwa heshima yako nakuomba huyu ndiye anauweza mji huu.

Kamishina alibaki kimya baada ya kuona jinsi wale wezi walivyo pata kipondo. Na serikali yao inavyowaogopa.

Nyamhindi akasema mimi nitakuwa kwenye mji huu kwa mwezi mmoja. Nataka mji huu unyoke kabla sijaondoka. Sawa?

Watu wote waliitikia sawa huku wakiwa na nyuso za furaha

Wakati huo watu kutoka Asosa walikuwa wamepanga kuja kuvamia serikali ya Malakal. Na jeshi la Asosa lilikuwa na nguvu sana.

Asosa ipo mashariki mwa Malakal. Watu wa Asosa wanauwezo wa kurusha mikiku maana nchi yao ipo kwenye vilima vilima.
 
Nyamhindi alikuwa akitembea na fimbo yake ameifunga mgongoni. Lakini wakati mwingine huwa anaishikilia mkononi. Kila sehemu akienda anaenda nayo.

Basi siku kama mbili hivi askali wa Malakal alikuja mbio kwa kamishna na kumwambi watu wote mpakani wameuawa na askari wa Asosa wanakuja. Askari waliokuwa mpakani wote wamechinjwa nimebaki mimi tu na nimeleta habari hizi. Jeshi la Asosa lina nguvu sana kwahiyo inabidi tukimbie twende Kadugli huko tutakuwa salama.

Nyamhindi alisikia mazungumzo hayo.

Baadae alimfuata Kamishna na kumuuliza unampango gani sasa kuhusu habari ulizozipata. Maana ninavyojua mimi kutoka hapa mpaka ufike Kadugli ni siku tatu. Je upo tayari kuwakimbia raia wako?

Kamishna akasema kwakweli mpaka sasa hivi sijawa na jibu lolote.

Nyamhindi akasema mimi nitakusaidia, lakini ninataka uniandalie askari 20 tuende nao.

Kamishna akasema askari 20 ni wachache sana maana jeshi la adui yetu ni kubwa lipo na askari mia mbili.

Wewe usijari kuhusu idadi kinachotakiwa ni mbinu. Idadi na umarufu hauna maana yoyote. Wewe ukikimbia nchi yako basi utakuwa tayari kuwa mtumwa na kuuza watu wako kwa bei chee.

Ni bora ukafa kwa kutetea nchi yako kuliko kufa bila faida. Kwani unauhakika gani kuwa utafika unakotaka kwenda? Ni vyema ukafikiria watu wako kuliko kufikiria kukimbia. Uongozi sio kuamlisha watu wafanye unayotaka tu, Uongozi ni pamoja na kuwalinda watu wako na mali zao.

Wale watu wa Asosa unaowasikia hao nakuhakikishia watakua mchanga kabla ya jua leo kuzama.

Kamishna alifanya kama Nyamhindi alivyo muagiza aliandaa askari 20 ili waongozane na Nyamhindi kukabili kundi kubwa la askari kutoka Asosa.

Nyamhindi aliwaambia kila mmoja anatakiwa kuchinja askari 10 au zaidi mimi hapa nitawalegeza wote. Nitawatia upofu wasione na nyie jitahidini sana kuchinja haraka haraka sawa. Wakasema sawa.
 
Nyamhidi alikumbuka alivyofundishwa na Lubala jinsi ya kutengeneza upepo wa pili pili.

Nyamhindi akawaambia sasa kila mmoja ajifunge kitambaa cheusi kichwani. Na kila mmoja ajichore mistari minane kwenye tumbo lake yenye rangi nyeusi kisha tuanze safari.

Nyamhindi aksema hizi nawapa mbinu za Busambilo huku nadani bado mko nyuma kidogo. Hawa wanaokuja hawa hamtawasikia tena katika maisha yenu.

Jifungeni vitambaa vyeupe usoni ili pili pili isiingie kwenye macho yenu.

Baada ya hapo Nyamhindi alivaa nguo nyeusi na kuwaambi twendeni. Alikuwa amebeba upinda na mshale mmoja huku mgongoni amefunga fimbo yake.

Walipo karibia akwaambia sasa ni mda wa kukomboa nchi yenu jiwekeni sawa. Basi tulieni hapa. Alipanda juu ya mlima, na kuhakikisha askari wa Asosa wanamuona. Alipiga mluzi “Swiiiiiiiiiiiiiiiiiii!” Askari wa Asosa waka mtazama nasema kwa sauti ya juu. Leo hii askari wa Asosa wote watakuwa mchanga.

Kisha akachomoa mshale!, akauweka kwenye upinde!, akajikuja!, akauvuta!, kuelekea angani!, akauachia shwaaaaaaaa!!!.

Baada ya hapo upepo mkali ulianza kuvuma.

Nyamhindi kasema kwa sauti kuu, Twendeeeee!!

Upepo ulikuwa na pili pili. Pili pili iliingia machoni mwa askari wa Asosa wakawa hawaoni, macho yanauma, Upepo unavuma, kelele za miti kuvunjika.

Basi Nyamhindi alikaa kwenye jiwe na kuangalia namna gani vijana walikuwa nao wanafanya kazi. Alikuwa ameshikilia mkononi hindi la kuchoma akila taratibu, huku akiangalia kazi inavyofanyika.

Baada ya kubaki mtu mmoja Nyamhindi akasema mwacheni huyu ili apelike taarifa.

Nyamhindi aksema nenda kamwambie falme wenu mimi ni Nyamhindi sawa. Askari huyo alitoka nduki kupeleka taarifa.
 
Askari alipofika kwa mfalme huku akiwa anahema sana “hohihohihohihohihohi!!!”.

Mfalme aksema nini mbona mbio hivi.

Mfalme hawa watu wamepata nguvu kuna msichana naitwa Nyamhindi huyu ananguvu sana hatumuwezi Askari wote wamekufa mimi tu nimeleta habari.

Mfalme Abemereki akase nini!!!. Yaani msichana ndio kawa ua wote. Askari akasema yule msichana ananguvu za jabu alirusha mshale angani kisha upepo wa pili pili ukaja tukashindwa kuona. Askari wachache wa Malakal waliwachinja askari wote kirahisi.

Mfalme alishituka. Akasema ajabu hizi nguvu tunasikia zinapatikana katika nchi ya mbali sana ya busambilo ina maana na hawa wana uwezo huo?

Askali akasema sijui mfalme lakini amenituma pia kwamba uende ukaonane naye yupo porini anakusubiri.

Mfalme alianza kutetemeka na kusema sasa mimi nifanye nini!!?

Wazee washauri wake wakamwambia Mfalme unatakiwa uende huenda hayo ni mazungumzo ya Amani.

Mfalme na watu wake wakaanza safari kuelekea porini ili kuonana na Nyamhindi.

Baada ya kukaribia, Nyamhindi alikuwa amepanda juu ya mlima.

Akasema kwa sauti kuu simameni, mmekuja kwa shari au kheri?

Mfalme akanyosha juu mbendera nyeupe.

Baada ya Nyamhindi kuona hivyo akasema mnaweza kuja.

Nyamhindi alishuka juu yam lima na kumfuata mfalme. Kisha akaanza kusema. Mimi jina langu naitwa Nyamhindi nadhani umesikia habari zangu kupitia askari wako huyu.

Mimi ni mjuu wa mfalme wa Busambilo. Mfalme Abemereki baada ya kusikia busambilo alianza kutetemeka sana. Nyamhindi akasema Mfalme mbona unatetemeka hivi.

Mfalme akasema sikujua kuwa wewe upo huko ninaomba unisamehe sitarudia tena kuonea watu.

Nyamhindi akasema mbona unanikatisha katisha ninapoongea? Akamtazama usoni hivi wewe kwa nini unatesa watu na kuamrisha majeshi kwenda kuvamia nchi jirani?

Je unashida gani katika nchi yako. Maana nchi yako ni nzuri mpo na mazao mazuri mnalima mnapata mazao. Sasa shida yako ni nini?

Mfalme akasema ni tamaa tu ya kutaka vingi.

Nyamhindi akasema rudi kwenye nchi yako, ishi vizuri na jirani zako kisha utamea kama mmea kondeni.

Mfalme na watu wake walirudi wakiwa na furaha iliyochanganyikana na huzuni.
 
Je kuna mtu yeyote anajifunza kitu juu ya hii series?
 
Hakuna hata mmoja mwenye wazo kuhusu hii riwaya?
 
Najifunza juu y mila n desturi y watu weusi n nguvu z giza kua zipo zitakuwepo tu!!!
 
Naiandaa vizuri nitarudi jioni msiwe na wasi wasi.
 
Kwakweli hadithi yako iko poa, nasubiri urudi!
 
Nakuja ndugu

Umenikumbusha kijiji kimoja kinaitwa ntulya kipo mpakani mwa misungwi na kwimba, nyumbani kwa marehemu mtoto wa Dandu.

Kuna makazi ya mchawi mmoja aliekua mashuhuli sana enzi hizo, moja ya kielelezo chake alichokiacha ni kupanda minyaa juu ya mwamba (hii nimeishuhudia kwa macho yangu)
 
Hakuna hata mmoja mwenye wazo kuhusu hii riwaya?

Story ni nzuri kwa maana imebeba maudhui ya jamii za kiafrika asilia........
Kila kitu ni cha kiafrika NA hii inakupa utofauti na story nyinginezo
, kama utaenda mbele zaidi NA kutengeneza series au movies..
NItakuwa wa kwanza kununua ili nikuunge mkono mtanzania mwenzangu....
NIMEUKUBALI UBUNIFU WAKO
***TANZANIA KWANZA*****
 
Yasni najiona niko karne hiyo,mtunzi hongera,ila Kuna ka ukweli fulani,wakina mzee Lubala wangekuwa hai na chuo Chao, guess who ange ji enroll Humu ndani?
Yaani mimi sio msukuma but ningekuwa wa kwanza kujiunga yaani on top of the table ya enrollment
 
Back
Top Bottom