Nyamhindi ni mzuri wa sura, sauti yake nyororo ya kuvutia alifanana kabisa na mama yake. Alikuwa napenda sana usafi wa mwili na mazingira yake. Meno yake meupe pee mithili ya mafungu ya pamba iliyo chambuliwa ki ustadi.
Japo kuwa alikuwa ni mdogo uzuri wake hakika hauwezi kufichika. Mwendo wake wa mikogo ulipendezesha sura yake na urefu wake aliokuwa nao.
Mashavu yake nyororo na alikuwa anapenda sana kuzitunza nywele zake za kuvutia utadhani manyoya ya mbuzi weusi wakitoka mtoni kuoshwa.
Kadri alivyozidi kuongea na Ntemanya, Ntemanya alijikuta anatabasamu na kusema sawa nimekubali uwe mama yangu. Ntemanya aliuliza je mama akificha chakula unaweza kunipikia.
Nyamhindi akasema mimi najua kupika sana nitakuwa nakupikia chakula kizuri sana alichonifundisha mama. Mama alikuwa nampikia baba na baba alikuwa akifurahi sana akila chakula cha mama. Mimi nitakupikia usiwe na wasi wasi.
Mama yake Mgoyela alikuja kwa hasira sana. Alipofika akamkuta Nyamhidi akiongea na Ntemanya. Baada ya kumuona Nyamhindi alirudi kwa hasira maana aliogopa kuongea chochote mbele ya Nyamhidi.
Aliporudi akamwambia Mgoyela nenda kamwite Ntemanya nahitaji aje hapa haraka.
Mgoyela alipofika kwa kujificha ficha akamwambia Ntemanya unaitwa na mama. Nymhindi akasema bado tunaongea atakuja tukimaliza.
Basi Mgoyela alirudisha taarifa kuwa Nyamhindi amesema mpaka wamalize kuongea ndio ataenda.
Mama alikasirika na kuanza kupigiza pigiza mguu wa kulia chini. Hivi haka katoto kananitakia nini haka mbona kamekuja jana tu kanataka kunipanda kichwani. Hebu ngoja azoee atanijua mimi nani.Kwanza nina hakikisha anarudishwa kwako.