Wachawi wote wa mji huo waliitwa kuja kwaajiri ya kushindana na Nyamhindi.
Baada ya wachawi hao kuja. Nyamhindi akasema nawaomba tukalale kwanza halafu tutaendelea kesho maana sisi tumechoka na safari tunahitaji kupumzika.
Mkuu akasema hapana mimi ninataka tuanze sasa hivi maana unaweza ukakimbia.
Nyamhindi akasema mimi sina ugomvi na nyie kabisa sisi sote ni binadamu si vyema kuanza kufanyia vitu vibaya.
Mkuu akasema ona sasa huyu anaogopa kufa ameona tutamchinda.
Nyamhindi akasema naomb basi wenzangu wakapumzike mimi nibaki hapa kwaajiri ya pambano.
Mkuu aksema hapa hatoki mtu yeyote.
Nyamhindi akakunja uso na kusema wewe wewe weweeeee!! Uatlipa haya yote!! Wewe subiri.
Basi wachawi wa mji huo wakaanza kuonesha madoido yao. Mmoja akamwaga Kamba nyingi chini na Kamba hizo zikageuka kuwa nyoka. Wakatokea nyoka wengi sana wa kila aina.
Mkuu akafurahi sana na kumwambi huyo mchawi amuru hao nyoka waweze kumuuma huyu binti.
Kweli nyoka waliamuliwa na kuanza kumfuata Nyamhindi. Nyamhindi alitupa fimbo yake chini Likatokea Joka kubwa na kuanza kuvimeza vijoka vya huyo mchawi.
Mkuu alistaajabu sana na akasema fanyeni jambo, Fanyeni Jambo jingine haiwezekani.
Yulee mchawi alianza kutetemeka na kushangaa imetokeaje.
Baadae joka lilibadilika na kuwa fimbo tena na Nyamhindi akaichukua fimbo yake.
Mchawi mwingine akakasirika sana nakusema niruhusu nimuue huyu binti na wenzake wote.
Mkuu akasema unaruhusiwa.
Nyamhindi akasema ukija vibaya nitakuumiza.
Mchawi huyo aliyekuwa amevlia mapembie ya Nyumbu kichwani, huku amevaa nguo nyeusi yenye madoa doa mekundu. Macho yake yalikuwa yamepakwa rangi yeusi tii.
Aliinama chini na kuchukua mchanga na kuurusha angani.Kisha akafungua kitambaa chake na kukitandika chini.
Baada ya kukitandika chini kitambaa hicho kilibadirika na kuwa dubu na mchanga aliourusha anagani ulibadirika na kutokea ndege wa ajabu wenye meno makali, wakiwa na macho manne, vichwa vyao mithili ya kichwa cha simba, wakiwa na mabawa makubwa sana.
Ndege hao walikuwa wane, wakiwa wanatoa sauti ya kutisha, huku dubu akiunguruma kwa sauti nzito.
Wale dubu na ndege hao wakajipanga kwaajiri ya kumfuata Nyamhindi.
Nyamhindi akasema wewe mchawi usiye na akili nitakuumiza na usipate wa kukutibu. Unatumia mbinu za uchawi kiwango cha nne ambacho ni kidogo sana.
Machawi akapaza sauti kuu na kusema hapa lazima tukumalize huwezi ukatuaibisha hivyo.
Nyamhindi aksema liwalo na liwe sina namna.
Wale ndege na yule dubu wakaanza kusogea kumfuta Nyamhindi huku wakipiga kelele na kuunguruma kwa sauti yakutisha.
Nyamhindi alipaza sauti na kusema Njoooooooo! Huku amenyosha fimbo yake angani.
Ghafla giza nene lilitoke watu wakawa hawaonani, sauti za dubu na hao ndege wa ajabu zikabaki zikisikia. Mvua kubwa ilitokea na ukimya ulitawala mji mzima.