Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,874
Mfalme alisimama mbele ya watu wake na kuelezea jinsi utabiri ulivyo kwenye utawala wa Basambilo.
Aliwaeleza kuwa nyota ya mashariki itang’aa sana kwa kipindi hiki cha miaka 100 ndipo utawala wa Basambilo utakapogawanyika vipande vipande. Mtu atatoka nje ya basambilo kuleta ungomvi na kuwa gawanaya watu. Utawala utagawanyika na kuanzisha koo zao.
Sasa hivi mnaniona mimi hapa nipo na nyie tuko na furaha nipo na wajumbe mbali mbali kutoka pande zote za Basambilo. Nipo na wanangwa kutoka Nindo, Salawe, Nela, Buhungukila, Busumabu, Buyombe, Bukoli, Buchosa, Kalumo, Mwigalo, Nsalala, Bulima, Ndagalu, Itilima, Ntuzu, Seke, Badi, Segelema, Ng’wagala,Busiya,Meadu na wengine wote ili kuwaeleza.
Hapa Basambilo ndio asili yetu wote kule mliko. Lakini pale nyota ta mashariki itakapozima mtasambaratika wote na kuanza kupigana ninyi kwa ninyi. Nyota za kusini zitang’aa na kuja juu yenu na kuwapoteza wote.
Kwa wale wataoutunza utabiri huu wataziona dalili za utawala wa Basambilo utakavyo anguka.
Nyota ya mashariki ni nyota ya kushoto inatakiwa mjue ambayo ndio inayong’aa sasa. Kipindi nyota hiyo itakapozima kuna dalili mtaziona. Mtoto wa kike wa mfalme asiye wa kwenu ataletwa kukaa kwenye kisima cha maji yanapotokea. Ndipo mtoto mkubwa wa mfalme ataamua kumuoa. Muonapo hivyo jitahidini sana kutunza ujumbe huu.
Mimi sasa hivi nimezeeka sitaweza kuwa na nyie kwa kipindi chote. Lakini aliye na akili ayaweke maneno haya. Kuna maneno mengi tuliambiwa na sisi na wazee wa zamani ya meandikwa kwenye kitabu chetu cha majira. Tafuteni mtu mwenye akili ya kuweza kusoma kitabu hicho mtajua mengi.
Baada ya miaka ya mateso katika ukoo huu wangu mkono wa kuume itatoka nyota ya magharibi itang’aa na kuleta ukombozi. Haitakuwa rahisi maana Busambilo itakuwa imepotea kabisa. Wenye kusoma majira wataelewa.