secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 21,119
- 43,023
Nasubiri madini hapa...
19 is enough..Kaka jioni ya leo nimeona namba fulani, halafu za dogo wa 2007 hapo sio poa.
Kaka ngoja niku onyeshe hizo namba, ili tuumwe wote19 is enough..
2019 huko nilikutana na mtoto hata chuo hajaingia ila yupo hired kutengeneza app. Ila ni kutokea zile familia za baba na mama wote seniors kwenye corporate.
Sawa 😁😁Kaka ngoja niku onyeshe hizo namba, ili tuumwe wote
Tayari chekiSawa 😁😁
Platform zipo nyingi, kwamfano mdau ametaja hapo juu Upwork, fever, freelancer, pia kuna Turing ambayo hii mwanzo ilikua inawafanyia vetting developers na kuwaunga na makampuni mbalimbali yanayotaka watu wa stacks zao ila sasa hivi nimeona imeongeza vipengele so haideal na developer tu pekee bali hata watu wa fields zingine like digital marketing in general, content writing na kadhalika.Wakuu, naomba msaada wa mawazo kutoka kwa wadau wenye uzoefu wa remote work au work from home nikiwa hapa Tz.
Nina hamu ya kuanza kujifunza na kuanza kufanya kazi za online kama njia ya kuongeza kipato kiasi cha pembeni ya shughuli zangu za kawaida.
Niningepend kusikia uzoefu halisi kutoka kwa waliowahi au wanaoendelea kufanya remote work.
Naomba kufahamu:
Platform zinazofanya vizuri kwa Watanzania
Jinsi ya kupata kazi au task hasa kwa mara ya kwanza
Skills zenye demand kubwa kwa sasa hasa mimi kama mTz
Njia rahisi za kupokea malipo
Na changamoto mbalimbali
Naomba kuwasilisha🙏
Shukrani sana mkuu info zimenyooka ngoja nianze kufanyia kazi.Platform zipo nyingi, kwamfano mdau ametaja hapo juu Upwork, fever, freelancer, pia kuna Turing ambayo hii mwanzo ilikua inawafanyia vetting developers na kuwaunga na makampuni mbalimbali yanayotaka watu wa stacks zao ila sasa hivi nimeona imeongeza vipengele so haideal na developer tu pekee bali hata watu wa fields zingine like digital marketing in general, content writing na kadhalika.
Mimi client wangu wa kwanza wa kazi za remotely nilimpata Facebook (najua watu wengi huwa wanaudharau huu mtandao ila ni mtandao ambao uko na watu wengi tofauti tofauti so pia unaweza kuanza nao)
Coz kwenye hizo platform huwa kuna ushindani mkubwa na watu huwaajiri watu ambao wako na rate nzuri pamoja na reviews nzuri kutoka kwa watu waliowahi kufanya nao kazi so unaweza ukafungua account huko then ukawa unatembelea kurasa za Facebook zinazohusiana na field yako then ukawa unabid huko ukifanikiwa kupata client na kufanya nae kazi unamwambia akarate na kukupa review nzuri kwenye account yako iliyopo kwenye hizo platform (Turing hawana hii ya rate wala nini ni wanakufanyia interview then ukipass wao ndio wanakutafutia kazi so wakipata kazi inayoendana na wewe wanakuwekea kwenye profile yako then wewe unaapply kisha utapangiwa trh ya interview utafanya interview ukipass unaajuriwa, pia lazima ujue hawa kazi zao niza mkataba wa kuanzia angalau mwaka mmoja, ingawa juzi kati nimeona kazi ya miezi kadhaa nayo imewekwa pia).
Pia LinkedIn ni nzuri, na kule kuna kazi nyingi sana zinapostiwa Kila siku Kila saa so ni wewe kuwa na profile nzuri na kuhakikisha ulichoweka kwenye profile yako ndicho unachokijua kweli pia utatengeneza cv yako na kuiupload pale na utawasha zako notification Kila wakipost kazi inayoendana na taaluma yako utakua unapata notification so utaenda kusoma vigezo na kuapply ukipita utacheckiwa na kuanza mchakato wa interview.
LinkedIn ni platform rahisi pia kupata client wako wa kwanza so unaweza kuanza nayo then ukitoka hapo unamwambia akakupe rate na review nzuri kwenye Upwork or fever au freelancer.
Cha kuzingatia hapo ni kuwa na mwanzo mzuri coz kupata client kwenye hizo platform sio shughuli ndogo hasa ukiwa mtu mpya ndio maana ni muhimu kuhakikisha unatembelea hizo platform na kuangalia bei za watu wanaofanya kile unachoenda kuoffer kisha angalia namna walivyoandika description zao na kadhalika then na wewe ufuate huo mtindo ila tofautiana nao kwenye bei so kuwa chini kidogo ili angalau uweze kupata clients then baadae ndio uweke kiwango unachostahili.
Hizo platform huwa zinatumia escrow accounts so pesa inafikia kwao then wanaihold kwa muda fulani mostly huwa ni kuanzia wiki hadi wiki mbili then baada ya hapo wanakutumia hiyo pesa yako, directly au kupitia wallets kadhaa ambazo utaziona pale.
So chagua niche then ifanyie research kwenye hizo platform.